Sumaye atoa siri

Kuhusu kushtushwa that is simply an understatement, Sumaye alitaka kujikojolea!

Kama unaweza kupata mkanda wa jinsi alivyokaa katika kiti unaweza kuelewa, jibaba lilikaa katika kiti kidogo lakini lilijifinyanga kwenye kona moja kama mtoto wa shule anayemsubiri mwalimu mkuu.

Hizi habari za kukataa ni porojo za fake humility ya wanasiasa tu.
 
Huyu Bwana tunamjua,Ben alimjua...ila nilitegemea kwa kipindi alichokaa nje ya siasa,labda 'kungembadilisha kidogo!!'lakini hamna chochote amejaa habari nyepesiX2 tuuu!!
**Anakiri kuwa wabunge walikuwa ni changamoto kwake,ktk miaka5 ya mwanzo ya uwaziri mkuu Mishahara na marupuX2 ya wabunge ndilo tatizo kuu lililomsibu na kama basi Ben angemwepushia miaka mingine5 iliyo msababishia 'chuki' kutoka kwa 'waheshimiwa wabunge',huenda leo hii angekuwa Mkuu wa nchi,je angeiweza nchi kweli huyu??labda kwa mtazamo wake; NCHI=(A 'happy' Cabinet + 'happy' MPs)period!!
 
Mijitu kama hii isiyojiamini hulazimishwa ili ipate kutumiwa,sasa huyu unafikiri angeweza kumshauri Mkapa asifanye biashara pale Ikulu ,tena kama haitoshi ndio inayotumika kuiua Nchi ,hivi ungetegemea mtu kama huyu apelekewe waraka wa ulaji wa Mkapa atie saini angeliweza kukataa ,maana akiambiwa ni mradi wa mzee basi hapo anakenua na kuanza kutoa shikamoo hata mkapa mwenyewe hayupo.
 
Ndio maana Bwana Sumaye akupita katika mchakato. Wazungu wanasema: " Leadership in not for the faint-hearted"
 
Attachments

  • The Law of Inverse Proportion.doc
    35 KB · Views: 72
Niliwahi kusikia stories mbali mbali za enzi za Mwalimu alipokuwa anawaita Ikulu ili kuwapa taarifa watu mbali mbali aliowateua katika kazi mbali mbali za serikali wengi walikuwa wakienda Ikulu roho zikiwa juu juu wakiwa na wasiwasi wameshavurunda nini tena. Na joto la Dar wengine walikuwa wanalowa mpaka suruali kwa wasiwasi na wengine hawakusita kuanza kujitetea pamoja na kuwa hawajui kosa walilotenda. Story nyingine zilikuwa zinatoka midomoni mwa wahusika walioteuliwa kwa kweli nyini zilikuwa zinanivunja mbavu.
 
Alichaguliwa kwa ajili ya udhaifu wake, five year down the line hakuwa amefanya lolote akaogopa nakujua atatemwa lakini watu wana akili zao, wakampa tena ili wale, for 10 years aliyoukwa waziri mkuu sikuona chochote, ni kama kulikuwa hakuna waziri mkuu...

Huyu jamaa fake kweli kweli eti alikataa uwaziri mkuu, mbona alikuwa kifua mbele anakimbilia urais juzi tuu hapa, na ninajua hajachoka bado atagombea urais tena, hawa jamaa wanatupiga mchanga wa macho, they are all the same
.

NCHI ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO.

iM OUT
 
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametoboa siri nzito ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, jinsi alivyomteua mara mbili kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa waziri mkuu pekee aliyelitumikia taifa kwa mihula miwili mfululizo.

Sambamba na hilo, Sumaye alisema kwa jinsi mambo yanavyokwenda nchini, anamshukuru Mungu kwamba alishindwa katika Uchaguzi Mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano.

Sumaye alisema hayo juzi katika mahojiano maalumu na kipindi cha ‘Jicho Letu' wiki hii, kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM. Mahojiano hayo ya Sumaye, yanatarajiwa kurushwa na kipindi hicho Jumamosi ijayo.
Bila kufafanua kwa undani, Sumaye alisisitiza kuwa kwa jinsi hali ya mambo inavyokwenda kiuchumi, kisiasa na kijamii, hajutii kabisa kuikosa nafasi hiyo iliyokutanisha wagombea wengine 11 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuibuka mshindi.

Katika mahojiano hayo, Sumaye alitoboa siri ya mshituko alioupata siku alipoitwa na Rais mstaafu Mkapa, na kujulishwa nia ya kutaka kumteua ili awe waziri mkuu.

'‘Kusema ukweli, sikuwa na habari hadi saa 7:30 ya siku ya uteuzi, ndipo Rais Mkapa aliponidokeza nia yake ya kutaka niwe waziri mkuu. Sikutegemea wala sikuota kama naweza kuwa waziri mkuu na hakuna mtu yeyote aliyejua mpango huo, kwani hakuna habari zilizovuja kabla," anasema.

Alisema siku hiyo, akiwa nyumbani kwake amejipumzisha, alipata taarifa za kuitwa Ikulu na Rais Mkapa.

'‘Wala sikutegemea habari ya kuwa waziri mkuu, maana hata Mkapa mwenyewe sikuwa nimezoeana naye," alisema.

'‘Mwanzoni nilifikiri labda ni mambo hayo ya Baraza la Mawaziri, pengine anataka kuniambia nitakuwa au sitakuwa kwenye Baraza la Mawaziri. Nikaenda, nilipofika, akaniambia ameniteua, nilishtuka sana aliponiambia, nami nilimwambia kwamba, sidhani kama kazi hii naiweza," alisema.

'‘Nilimwambia, kwanini usitafute mtu mwingine, lakini yeye aliniambia, ahaaa! hapa hakuna majadiliano tena, jina nimeshapeleka kwa Spika, wakati huo (Pius Msekwa) na saa 11 atakuita, nakupa taarifa tu ili ukajiandae na hakuna habari za kupatana hapa, tayari nimeshaamua," alisema.

'‘Wakati ule alikuwa hapa Karimjee. Nilipata shida sana, nikaondoka, nikapita ofisini, sekretari aliponiona nimechanganyikiwa, akaniuliza kuna nini bosi, nikawa sisemi na mtu, nikaondoka, nikaenda nyumbani," alisema Sumaye.

Alipofika nyumbani na kukutana na mke wake, Sumaye alisema: '‘Nilimwambia mke wangu, rais ameniteua kuwa waziri mkuu, na kitu cha kwanza akaniambia, usikute umekubali. Ugomvi ukanzia hapo, nikamwambia, nimejaribu kukataa, lakini amening'ang'ania," alisema Sumaye, huku akicheka.

Kuhusu uteuzi wa awamu ya pili uliowahi kuzua gumzo nchini, Sumaye alisema kama ilivyokuwa mara ya kwanza, safari hii hakutarajia kabisa kuendelea na nafasi hiyo.

Alisema hakutarajia kwa sababu mara baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano, alikwenda kumuaga Rais Mkapa, kwani hakutaka kurejea tena kwenye nafasi hiyo, hasa kutokana na misukosuko mingi aliyokutana nayo katika kipindi cha miaka mitano ya muhula wa kwanza.

Alisema, lakini baada ya uchaguzi kufanyika, Rais Mkapa alimpigia tena simu na kumweleza nia yake ya kutaka aendelee na nafasi hiyo.

'‘Safari hii nilikataa kwa nguvu zangu zote, kiasi cha kugombana naye, niligoma kweli kweli. Nilimwambia Rais Mkapa kuwa safari hii, sipendi kuendelea na nafasi hii, kwa vile nimegombana sana na wabunge," alisema.
Alisema alikorofishana na wabunge kwa sababu alikuwa akipinga hoja zao za kutaka kuongezewa mishahara na marupurupu.

'‘Nikamwambia, ukipeleka jina wale wabunge watakaa kulipitisha, hivyo ni bora safari hii umchague mtu mwingine," alisema.

Kwa mujibu wa Sumaye, Mkapa alimlazimisha aende, na kama wabunge watamkataa, basi itajulikana hapo na atajua la kufanya.

'‘Mkapa alikataa na kuniambia, kama watakutaa, basi tutajua la kufanya, lakini nionavyo, huwezi kukosa nusu ya kura za wabunge," alisema Sumaye.

Hata hivyo kwenye hatua ya kupitisha jina lake, Sumaye aliweza kupata kura nyingi, ni tatu tu ndizo zilizomkataa.

Kuhusu makundi yaliyochipuka wakati wa uchaguzi na kuendelea hadi sasa, Sumaye alisema yalishakufa na kuzikwa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu, huku yakitembea na matumaini ya urais mifukoni mwao.

"Makundi ya uchaguzi yalishakufa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu kutokana na umaarufu wa nafasi zao. Hao bado wanauota urais, na bado wanatembea na urais mifukoni," alisema Sumaye.

Mbali ya kutoboa siri ya uteuzi wake, Sumaye pia alizungumzia uwezekano wa kuwania tena nafasi ya urais katika uchaguzi ujao, suala tata la utaifa wa Zanzibar na dawa ya kumaliza tatizo hilo. Sehemu hiyo ya mahojiano itaendelea kesho.

Siku zote watu wanasema mke ndie anayejua udhafu wa mume kwa undani... sasa hapa oneni wenyewe... hata mama watoto alishamwona hafai ndio maana kitu cha kwanza alimhoji... usikute umekubali... kwi kwi kwi... hee hee kweli hapa ametoa siri ... hii ilitakiwa ibaki kuwa siri yake na mkewe
 
sababu za kitoto
 
Plagiarism you have to acknowledge the source i.e http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/29/habari1.php
 
Alichaguliwa kwa ajili ya udhaifu wake, five year down the line hakuwa amefanya lolote akaogopa nakujua atatemwa lakini watu wana akili zao, wakampa tena ili wale, for 10 years aliyoukwa waziri mkuu sikuona chochote, ni kama kulikuwa hakuna waziri mkuu...

Huyu jamaa fake kweli kweli eti alikataa uwaziri mkuu, mbona alikuwa kifua mbele anakimbilia urais juzi tuu hapa, na ninajua hajachoka bado atagombea urais tena, hawa jamaa wanatupiga mchanga wa macho, they are all the same
.

NCHI ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO.

iM OUT

Inawezekana una ukweli na unayosema. Lakini let us use our brains and ask ourselves, which choice was better between Sumaye and Lowassa?. Inawezekana wote ni wabaya lakini yupi alikuwa na afadhari kwa Tanzania. AMbaye alionekana kama hayupo na mabaye alionekana kuwa yupo kwelikweli.
 
sababu za kitoto

Mkuu Gembe mkeo asipoku-endorse nani tena??? Weye huoni alisema ugomvi ulizuka? Wajua huku Afrika ambako mfumo dume bado umetawala twafikiri wake zetu hawana mawazo ya kuweza kutusaidia. Hushangai kwanini anasema ugomvi ulizuka yakhe??????????
 
Sumaye kabla ya kuwa waziri mkuu, alikuwa ni mtu wa kawaida tu.

Alikuwa ni naibu waziri wa kilimo na hakuwa amepiga kitabu sana zaidi ya kuwa na diploma ya kilimo.

Sasa alivyokuwa akiishi kwa kutokuwa na makundi, upole na tabia yake ya ukimya, akaonekana (kwa mtazamo wa Mkapa na washauri wake) kwamba angefaa kuwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

Lakini hold on, hawa watu wawili Mkapa na Sumaye waliishi jirani sana kiasi cha kuweza kukutana ama Palm Beach au Leaders Club.

Kwa hio pia tunaweza kusema kwamba kulikuwa na pre-planned sketch ya nani atakuwa nani na kadhalika.

Tatizo kwa upande wa Sumaye, kwamba alipoona mlango wa opportunity umefunguliwa ndio akachanganyikiwa kwa kuona kila kitu amazing na kujisahau kuongoza serikali bungeni na hivyo kila kitu kwenda mtindo wa business-business pale magogoni.

Na ndio matokeo yake majority ya walliokuwa ndani ya serikali ya Mkapa wameula.

Sumaye eti nae anataka kufanya spinning, alaa!
 
Back
Top Bottom