Sumaye alipua watawala Afrika

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
538
katika kipindi cha dk 45 cha ITV leo, ametumia neno nchi za kiafrika lakini ndani yake ameongelea tanzania "kinyemela",

kasema tatizo kubwa la nchi za africa wanatumia uraisi vibaya, akasema unakuta mtu alikua mtu wa kawaida tu lakini gafla

amekua raisi basi amekua tajiri, watoto wake matajiri, anasema matatizo makubwa ni ufisadi na matumizi mabaya ya uraisi.

kingine aliulizwa mbona amekaa pembeni huku akiona nchi inaelekea kubaya? akasema hawezi kwenda kumsaidia mtu bila kuitwa,

tena akasema hata mzee mkapa alishalisema hilo swala kwenye mkutano uliofanyika pale mlimani city.

my take: hiki chama chao kinawaka moto kichinichini, yani wanauana kinyemela nyemela....yangu macho.
 
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye anawalipua vibaya watawala wa Africa kwa ufisadi mkubwa na kukabidhi taasisi ya Urais kwenye familia zao.Wenye access angalieni sasa hivi ITV katika kipindi cha dk 45
 
anasema kuna takukuru lakini mbona wakati wa uchaguzi wengine hawakamatiki???? duuuuuuuuuuh another bomb...!!
 
katika kipindi cha dk 45 cha ITV leo, ametumia neno nchi za kiafrika lakini ndani yake ameongelea tanzania "kinyemela",

kasema tatizo kubwa la nchi za africa wanatumia uraisi vibaya, akasema unakuta mtu alikua mtu wa kawaida tu lakini gafla

amekua raisi basi amekua tajiri, watoto wake matajiri, anasema matatizo makubwa ni ufisadi na matumizi mabaya ya uraisi.

kingine aliulizwa mbona amekaa pembeni huku akiona nchi inaelekea kubaya? akasema hawezi kwenda kumsaidia mtu bila kuitwa,

tena akasema hata mzee mkapa alishalisema hilo swala kwenye mkutano uliofanyika pale mlimani city.

my take: hiki chama chao kinawaka moto kichinichini, yani wanauana kinyemela nyemela....yangu macho.
Mnafiki mkubwa huyu kada wa mfumokristo!.Mbona hakuzungumzia watu wanaokuwa mawaziri wakuu katika Afrika halafu muda si muda wakajenga majumba makubwa kila kona?.
 
Hivi yeye ana nyumba ngapi? Na pato lake lilikua ngapi?
 
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye anawalipua vibaya watawala wa Africa kwa ufisadi mkubwa na kukabidhi taasisi ya Urais kwenye familia zao.Wenye access angalieni sasa hivi ITV katika kipindi cha dk 45
Nami nakishuhudia kipindi. Inavyoonekana Sumaye ameamua kupumua kwa kupunguza dukuduku lake moyoni. Njia aliyotumia ni sahihi kabisa. Ameamua ku-generalize ili kwenye kapu hilo na mkuru aingie. Ukweli ni kwamba alimlenga mkuru mwenyewe.

Nami naungana na aliyesema kwamba ndani ya ccm kuna moto unafukuta. Siku ambayo mfukuto utakuwa mkubwa kiasi cha kutodhibitiwa, bila shaka mwangwi wake utateteresha chama na nchi kwa ujumla. Na hilo likitokea nchi itapata uponyaji. Yangu macho.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
ameponda pia swala la posho, amesema serikali imehamishia ofisini mahotelini....kasema yeye alipinga sana maswala ya posho kipindi chake akagombana na wabunge, lakini pia amesema kama wabunge wanabusara wapime jinsi ambavyo wananchi wanavyolalamika then ifanye maamuzi ya busara, kasema pia TRA wanakusanaya hela nyingi sana lakini kutokana na tabia ya wafanyakazi wa serikali kugawiana posho hovyohovyo ndomana hela inayobaki kwenda kufanya shughuli za kijamii/umma zinakua ndogo kabisa.

mi nasapot anachikizungumza hata kama yeye pia alikua mhusika au la.........
 
Dr Dr Dr Mwanajeshi aliyekimbia kambi, Professor to be, Mtuhumiwa wa ufisadi, Rais wa NEC, Alhaji Kikwete kazi anayo mwaka huu 2012, goma ndio limeaanza. Atakufa kwa presha za maandamano na midahalo mwaka huu. Ushauri wa bure iongezwe bajaji ya Ambulance kwenye msafara wake moja haitoshi.
 
amekuwa waziri mkuu kwa miaka mingi alifanya nini la kukumbukwa na watz?huyu mzee mnafiki sana halafu ni mwizi
 
Kweli, anachokiongea ni sahihi lakini siyo kile anachokiishi. Kuongea na kuishi maneno yako ni vitu viwili tofauti. Kama alikuwa waziri mkuu kwa muda wa miaka kumi na bado hakuwa na mchango mkubwa kiasi cha kulisaidia kuondokana na umaskini, ni kipi ambacho anakitaka sasa? Japo amekanusha kuwa hajapata wazo la kuwa rais, na kama akilipata atatangaza, ana mawazo gani mapya ambayo hakuwa nayo kipindi cha miaka kumi cha uwaziri mkuu wake?
Yeye na mwenzake mkapa ndio waasisi wakubwa wa sera ya uwekezaji iliyomaliza viwanda vya ndani na kutuacha tukitegemea wahisani na rais aliyopo madarakani kuwa omba omba akiwapigia magoti marais wenzake kama yeye si mwanaume!!!!
Shame on us tanzanians?
 
Sumaye amekua very technical kuishambulia serikali ya ******. Katumia Africa kumaanisha Tanzania. Kwamba watu wanatumia uraisi kifamilia na wangependa familia zao ziwarithi akimaanisha kinachondelea ndani ya CCM baina ya ****** na mwanae.

Pia indirecltly kamshambulia Pinda kuhusiana na swala la Posho. Yeye kajinasibu kuwa akiwa waziri mkuu alipinga swala la Posho na kwamba awamu ya pili ya Mkapa alimkatalia uwaziri mkuu kwa kua aliwapinga katika posho 1995-2000 lakini Mkapa akamshikia bango. Maana yake ni kwamba Pinda nae ni mshirika wa Posho na pia kwamba serikali imehamia mahotelini kwa semina na makongamano na yote hayo ni lazima yapate kibali cha Pinda.

Bravoo Sumaye hata kama wewe ni mshirika wa mfumo huo wa kishetani kwa kuwa na ujasiri wa kusema.
 
jamani ameona makosa yake ya miaka 10 akiwa pm,sasa amefumuka hakuna wa kumshika mdomo.......huu muda wa kufunguka tuuuuu..................akimaliza ataje ufisadi wake wa ardhi.........umenena ukweeeeeeeeehhhhhhhhhhh
 
Dr Dr Dr Mwanajeshi aliyekimbia kambi, Professor to be, Mtuhumiwa wa ufisadi, Rais wa NEC, Alhaji Kikwete kazi anayo mwaka huu 2012, goma ndio limeaanza. Atakufa kwa presha za maandamano na midahalo mwaka huu. Ushauri wa bure iongezwe bajaji ya Ambulance kwenye msafara wake moja haitoshi.

sijakuelewa hapo kwenye reddddddddd
 
sumaye amekaa magogoni miaka 10 hatujaona la maana leo anajifanya kutuletea matamko apa.hatudanganyiki.akawaambie kwenye vikao asitafute umaarufu kwenye public,au nae ni mlalamikaji
 
Sumaye ni mnafiki tu mbona hakumsema Mkapa wakati anafanya biashara ikulu,au haijui Annben?mbona wakati wakijiuzia nyumba za serikali yeye hakupiga kelele zozote naye mbona aliingia masikini katoka tajiri ,hivi sasa serikali inawalipia watu kukaa mahotelini kwa gharama kubwa kwa sababu yeye na Mkapa walijiuzia nyumba,Sumaye naye ni walewale au amesahau alivyokuwa anatuhumia kwa kujilimbikizia mali kula kona,hata kama ni tuhuma kwanini yeye atuhumiwe?na afunge bakuli lake anatutia hasira ni mchafu kama wenzake
 
Sumaye amefanya kile kinachoitwa right button @ the right time, ameipiga mawe Serikali ya JK kwa gia ya kujifanya kama alikuwa anazisema Tawala za Africa in General, ila kikubwa na cha umuhimu nilichokipata kutoka kwa Sumaye leo ni kwamba sio siri tena kwamba Nchi yetu imefirisika mwenye masikio na asikie!

Amesema wao katika utawala wao hawakuthubutu kuchapisha noti mpya ili kuziongezea kwenye mzunguko, na ukiona dunia hii nchi inachapisha noti kwa uhaba wa noti basi ujuwe nchi hiyo Imeshafirika, na hapo ndipo ilipo Tanzania yetu na huu ndio ukweli wenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom