Sumatra na Trafiki mko wapi Ubungo hadi Kibamba?

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Ndugu wana JF, nipeni nafasi pembeni ili nitoe kero hii ambayo imekuwa sugu kwa wakazi wanaoishi maeneo ya kuanzia Ubungo hadi Kibamba. Nidhahiri kuwa pengine Sumatra na askari polisi wameenda likizo au wameamua kwa makusudi kuachia wanachi wateseke au wao ndo wamiliki wa magari yapitayo barabara hii ya Morogoro.
Simaanishi kuwa maeneo mengine ya Dar es Salaam hayana matatizo, rahasha, hapa namaanisha huku maeneo haya tajwa yamekuwa zaidi ya Darfur. Ndugu zangu pengine niorodheshe matatizo yanayojitokeza kwa wakazi wanaotumia usafiri wa kiraia kupitia barabara iliyotajwa.
Kwanza ni uamuzi wa wenye daladala kuamua kuongeza nauli watakavyo bila ata kujali vyombo mhimu vikiwemo Sumatra na askali polisi wa usalama barabarani. Kwamfano, kabla ya nauli mpya za daladala ambazo ni Sh. 300 kuanzia Ubugo hadi Mbezi mwisho, Ubungo hadi Kibamba Sh 400 na Kimara hadi Kibamba ni Sh. 350. Na kwa mwanafunzi ni Sh. 150 kwa kituochochote aendacho.
Lakini mbali na kuwepo nauli halaili kwa mfano tu hizo zilizotajwa hakuna ata dereva na kondakta wake anailipisha nauli hii! Kwa mfano asubuhi au jioni sana Ubungo hadi Mbezi ni kati ya Sh. 300-600, Ubungo hadi Kibamba Sh 600-1200 na Kimara hadi Kibamba ni Sh. 600-1000. Pia hii hutegemea dereva na konda wake wameamuaje.
Tatizo lingine ni kutokuwepo na utoaji tiketi. Kwenye njia niliyokutajia hapo juu, madereva, wamiliki, makondakta nk, hawajawahi kutoa au kujishughulisha na utoaji wa tiketi. Ukiombwa Tiketi unatukanwa na kudharirishwa vibaya sana. Haya yote hayahitaji kufanya utafiti wa kuvizia, ata ukienda leo au kesho utayashuhudia.
La tatu ni suala la wanafunzi. Ni jambo la kusikitishya ukiona jinsi wanafunzi wanavyodhaliliishwa kwa matusi, kutozwa nauli za watu wazima, kuachwa vituoni hadi saa 5 au zaidi na kusukumwa, kufokewa na kukamiwa na makondakta. Ni mateso amabayo yanafanyika wazi wazi huku wakati mwingine wakiwemo polisi ndani ya daladala hizo ambao wanafanya kazi maeneo mbali mbali ya kuelekea barabara hiyo.
Tatizo linguine ni mgomo wa kusimama vituoni hasa asubuhi na jioni sana pale gari hizi zinapotokea kituo cha ubungo. Hawa jamaa wanawafanya abiria kuwa vituko. Wnaweza kupita bila kupakia kwa maana ya kuwachezea abiria na wnapoona wanakimbilia gari huwa wanafurahi na kuondoa magari.
Kibaya zaidi kinachofanya madereva na makonda wao kulifanya eneo hili kuwa kama Darfur ni ubabe. Hawa jamaa wao ni polisi na mahakama. Wanajiamini kiasi ambacho unaweza kuwa na wasi wasi hasa kama kweli hawana hisa polisi au Sumatra. Wanaweza kukushusha popote au kukufnaya lolote na kuondoa gari au kukupeleka hadi mwisho kwa kigezo cha kuwa wao wana magari yenye ruti ya mkoani. Ikumbukwe kuwa unapopanda hawakwambii kuwa ni gari la mkoani.
Hapa ni lazima tujue kuwa wananchi wananchi wengi ni WALALAHOI kama si WAKESHAHOI.
 
Back
Top Bottom