Suluhisho si kuondoa mawaziri tu

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Nimekuwa nasikitishwa na uongozi wa serikali ya awamu ya nne ya Tanzania kwa jinsi inavyoshughulikia mambo ya msingi kabisa yanayohusu masilahi ya watanzania kwa ujumla. Utendaji wake hauna tofauti na mwindaji porini aliyejificha katika kichaka kusubiri ni mnyama gani atakaejitokeza ampige rungu la utosini apate kitoweo. Mwindaji wa aina hii hana hakika anakwenda kuwinda aina gani ya mnyama.

Serikali imekuwa ikiambiwa na wananchi mumuondoe fulani madarakani kwa kushindwa kufanya kazi za umma au kuiba mali. Wananchi wameiweka madarakani serikali ili iweze kufanya ulinzi wa mali ya umma. Kama serikali itasubiri wananchi wawataje wezi basi itakuwa imeshindwa kutekeleza majukumu iliyopewa maana serikali inavyombo vyote muhimu kama Usalama wa Taifa, Takukuru, Maadili ya Utumishi wa Umma, Polisi, CAG n.k

Hakuna mtanzania asiyejuwa madudu yaliyoibuliwa bungeni yanayowahusu baadhi ya Mawaziri wachafu wa serikali iliyopo madarakani, ni wiki ya pili sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kama ambavyo zinavyochukuliwa kwa wezi wengine wa mtaani na hata wale wa maofisini zaidi ya kusikia ngonjera tu za kuwahadaa wanachi kila kukicha. Taratibu za kazi zinajulikana wazi kuwa yeyote anaebainika kuwa na tuhuma za wizi hatua ya awali kabla ya yote ni kumsimamisha kazi kutoka katika majukumu aliyonayo ili asiweze kuathiri uchunguzi.

Nadhani ingekuwa busara zaidi kama mawaziri hawa wasingekuwepo ofisini hata kabla Rais hajawavua vyeo vyao. Uwepo wao ofisini mpaka sasa ni dhahiri kuwa wamepewa muda wa lala salama kila mmoja aweze kuchuma anachoweza ikiwa ni pamoja na kuondoka mpaka na fenicha za ofisi.

Pili, tatizo la wizi wa mali ya umma halipo tu kwa mawaziri, ni muda muafaka kwa serikali kuwawajibisha watumishi wote wa umma wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kuongoza kupokea rushwa ikiwa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa majiji, Halmashauri na Manispaa (hawa ndio kama miungu watu), mahakimu, Polisi, Uhamiaji na kwingineko.

Kuondoa mawaziri pekeyake haitatibu kansa iliyopo katika serikali hii.
 
Back
Top Bottom