Sultani Jamsheed hakukana kiti cha Usultani wa Zanzibar

sasa mwambie huyo qeen aje kuchukua ardhi yake uone kama atapewa!!!!!!! wansema hivyo kama sehemu ya historia tu, kiuhalisi hakuna mtu anaweza kusema anamiliki ardhi ama watu...............time will tell!!!!!!!!!

Kalaga baho.
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.
kama kuna kipengele ndani ya katiba ya SMZ au at least kwenye ilani ya CUF inayotoa nafasi kwa usultani kurejea zanzibar, ningekuomba utuwekee hapa, otherwise ningelikuomba uache porojo za kuchochea chuki.Zanzibar ni nchi inayolindwa na katiba yake na sio maelezo ya watu.
nawasilisha
 
Ndugu yangu haya ni maneno mazito. Tumejikita sana kupiga domo tunajisahau sisi ni kina nani. This life has a meaning and we cant know that meaning if we spend alot of our time on issues that don't add any value to us as individuals. Naogopa sana kuhisi hivyo, lakini mara nyingi wanasiasa wanatutumia kuhitimisha agenda zao za kupata madaraka, pengine bila kutoa msaada wowote kwetu baada ya kuyakwaa madaraka hayo. Hii ya Zanzibar hii haijakaa katika kutafuta mwelekeo mzuri tu wa siku za usoni, ila pia imebeba ajenda nzito ya baadhi ya watu kutaka kupata hayo madaraka kwa gharama yoyote ile. Ndiyo maana naona nguvu imeelekezwa kuufukia chini muungano ambao naona baadhi wanataka kusema ndiyo chanzo cha matatizo ya kisiasa ya Zanzibar.Mimi sitaki kuamini hivyo maana yale mapinduzi yalikuja kwasababu kulikuwa na matatizo ya kisiasa. Je nayo yaliletw na muungano?
ndugu.
maelezo yako ni mazuri lakini nimewahi kuongea sana hapa, unajua hali ya zanzibar tunaielewa zaidi sisi tunaoishi zanzibar, tunajua tulikotoka na tulipo,ni ukweli usiopingika kwamba wazanzibari wamekumbana na mengi yaliyowafunza katika maisha yao halisi (na sio magazeti).Hivi utaamini kwamba Zanzibar hata mtoto ambae hajafikia umri wa kupiga kura basi anaweza akadanganya umri ,ilimradi tu awakilishe hisia zake kwenye kisanduku cha kura(akapige kura)?, jiulize ni kwanini?.Wazanzibari tunaongelea hali halisi tunayokumbana nayo ,Watanzania bara munaiongelea Zanzibar kwa kuisoma magazetini au kuitembelea wiki moja.
nawasilisha
 
Pasco!!Huyo mtoto humjui? Si Maalim seif. Waulize akina Natepe watakwambia. Kizazi chao kiko Oman kwa akina Sultan Qaboos

Heeee Marigwa hiyo kali, tena munampa umwana wa Sultani Sefu Sharifu? He he he heeeeeeee!

Sefu Sharifu ni Mpemba 'fyoko' ule wekundu (sisi hatuiti weupe) ni kwa sababu kwa miaka mingi yuko kivulini na vile vile wako Wapemba wengi wenye rangi ile ambao hawana uhusiano wa karibu na Waarabu.
 
kama kuna kipengele ndani ya katiba ya SMZ au at least kwenye ilani ya CUF inayotoa nafasi kwa usultani kurejea zanzibar, ningekuomba utuwekee hapa, otherwise ningelikuomba uache porojo za kuchochea chuki.Zanzibar ni nchi inayolindwa na katiba yake na sio maelezo ya watu.
nawasilisha

Je, Sultani Jamsheed arudishiwe mali aliyonyang'anywa kufuatia mapinduzi ya 1964?
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

Hoja yako hii ni "historical streotape" ambayo nimeisikia zamani sana lenye lengo la kuwafanya tuamini kwamba wazanzibar hawawezi kusema NI kwa sultan mpaka wasaidie na wa tanganyika....gues what unatishia nyau, hakuna hoja kabisa hapa zaidi ni dharau kwa wananchi wa zanzibar..

a) Sultani hawezi kurudi zanzibar, kwasababu ni democratic country wala siyo kingdom based country.. kuna vyama vya siasa na viongozi watapatikana katika ushindani wa kisiasa

b) hakuna kitu hapo kutokana na jibu la (a)

c) Wishingfull thinking and fooling people on a wrong concepts and idea pole sana mzee

d) Wishng full thinking as I said in (c)

e) You are talking of non-existence entity so your whole hypothesis is null and void

Umeonyesha kiwango cha chini cha kufikiri kwasababu umesukumwa na emotions bila kuwa rational? Jiulize
1. What is so special kwenye muungano kiasi kwamba anayetaka kuulizia lazima apewe majina yasiyofaa?

2. Kama ni muungano wenye faida kwa pande zote mbili mbona easy tu weka mjadala wa kitaifa bila kuleta upupu wako tuangalie mbele na vizazi vijavyo

3. Sultani is the past history let us focus on the future, historia ya tanganyika unataka kusema na queen atarudi eti kwasababu xyz atakuwa rais? sikuelewi

Honestly "Hujaandika kitu hapa unapoteza muda wa watu"
 
ndugu.
maelezo yako ni mazuri lakini nimewahi kuongea sana hapa, unajua hali ya zanzibar tunaielewa zaidi sisi tunaoishi zanzibar, tunajua tulikotoka na tulipo,ni ukweli usiopingika kwamba wazanzibari wamekumbana na mengi yaliyowafunza katika maisha yao halisi (na sio magazeti).Hivi utaamini kwamba Zanzibar hata mtoto ambae hajafikia umri wa kupiga kura basi anaweza akadanganya umri ,ilimradi tu awakilishe hisia zake kwenye kisanduku cha kura(akapige kura)?, jiulize ni kwanini?.Wazanzibari tunaongelea hali halisi tunayokumbana nayo ,Watanzania bara munaiongelea Zanzibar kwa kuisoma magazetini au kuitembelea wiki moja.
nawasilisha

Brother umenena na hili ndio tatizo humu JF. Nilikuwa nataka kumjibu but majibu yako yanamtosha kwani atatafakari zaidi. Kuna mmoja alidai alipigwa mawe nimewahadithia washkaji wamecheka sana!!! Kwani wao ni wakristo na tulienda zanzibar kikazi maana niliwachukua washkaji walikuwa wanadhani zanzibar kama afghanistan nikawaambia twendeni zanzibar. Zanzibar ukitaka bar ipo, ukitaka night club zipo, ukitaka private club (hizi special VIP) zipo starehe zote zipo. Dada mmoja akanambia anaogopa watu wanaovaa vimini wanapigwa nikamwambie twende ukipigwa nipeleke mie polisi. Tangu nimpeleke imekuwa kila weekend yule dada anaenda kupumzika zanzibar akimaliza kazi zake.
 
irrelevant; ndiyo mambo mepesi mepesi ninayoyazungumzia. Kuwa na bar na kuvaa vimini ndiyo nini? Unafikiri kuna umuhimu kwa CUF na CCM Zanzibar kumtaka Sultani Jamsheed kule Portsmouth kukana kile anachodai ni halali yake yaani Usultani wa Zanzibar?
 
Nonsense, unaongelea mambo mepesi mepesi yanayotokana history, unarudiarudia ujinga kwasababu huna hoja nyingine ya kuulinda muungano, very sad!

Barbados iko chini ya queen wanashida gani, kuna visiwa chungu mzima ziko chini ya queen

Hii habari yako ni very irrelevant na unapotosha watu kwa makusudi kwasababu hakuna mtanganyika anaweza kueleza kwa haki anaitakia nini? zanzibar..kama wanataka ufalme so it be? inakuuma nini? ni choice yao
 
irrelevant; ndiyo mambo mepesi mepesi ninayoyazungumzia. Kuwa na bar na kuvaa vimini ndiyo nini? Unafikiri kuna umuhimu kwa CUF na CCM Zanzibar kumtaka Sultani Jamsheed kule Portsmouth kukana kile anachodai ni halali yake yaani Usultani wa Zanzibar?

Mkuu MKJJ,Hoja yako ni nzito,hata hivyo ni muhimu ukaweka wazi vielelezo zaidi vyenye kuonyesha kama kweli Sultan bado ana nia ya kurudi kwenye kiti chake cha enzi.
Hata hivyo kama ushauri wako kwamba Sultan aulizwe na both CCM na CUF kuhusu msimamo wake ukifuatwa,then tunaweza ku conclude one way or the other.
Pili,je ni nini haswa kinachomzuia Sultan kurudi kama ana nia hiyo?Je una imply kwamba ni muungano ndio kikwazo cha sultan Jamsheed kurudi?
 
irrelevant; ndiyo mambo mepesi mepesi ninayoyazungumzia. Kuwa na bar na kuvaa vimini ndiyo nini? Unafikiri kuna umuhimu kwa CUF na CCM Zanzibar kumtaka Sultani Jamsheed kule Portsmouth kukana kile anachodai ni halali yake yaani Usultani wa Zanzibar?

Kama ilivyo thread yenyewe, haina reference, data unadhani kuna kitu cha maana kinaongelewa hapa?

Zanzibar hakuna mtu anatime na sultani let alone kumjua huyo Jamsheed. Bora tuweke starehe maana kuna watu wamedai zanzibar wanapigwa mawe well mie as far as I know washkaji zangu wengi if not all wakiristo tena mmoja mlokole nikamuonyesha kanisa lilipo kwani alitaka kusali jumapili but life is good zanzibar kama una hela lakini kiukweli hali ni mbaya kwa watu wanaotegemea maisha yao hapo kisiwani na ukienda mashambani ndio worse case inasikitisha kwakweli!!

:rolleyes:
 
Mkuu MKJJ,Hoja yako ni nzito,hata hivyo ni muhimu ukaweka wazi vielelezo zaidi vyenye kuonyesha kama kweli Sultan bado ana nia ya kurudi kwenye kiti chake cha enzi.

Anayo nia ya kufanya hivyo. Ushahidi ni kuwa hajawahi kukana haki na uhalali wake wa yeye na wanawe kuwa watawala wa Zanzibar kama ilivyoanishwa katika makubaliano ya Uhuru ya 1963. Mojawapo ya mambo ambayo watu wanataka kule Zanzibar kwanza ni suala la Serikali ya Mseto. Pili ni kutambua Uhuru wa 1963 kutoka Mwingereza.

Ukweli ni kuwa uhuru ule ulipofanyika ulimretain Sultani kama Constitutional Monarch na hivyo kuwa Head of State. Hilo ni mojawapo ya mambo ambayo ASP iliyapinga sana. ZNP na ZPPP hawakuona tatizo hilo na wakakubali kuunda serikali ya Mseto chini ya Shamte.

Hivyo mapinduzi ya Januari 12 yalikuwa si kuiangusha serikali ya mseto hasa bali ni kuvunja utawala wa Sultani wa Zanzibar kama ulivyokubaliwa na ZNP na ZPPP. Hivyo, hata alipoondoka Zanzibar Bw. Jamsheed kukimbilia Dar na uzao wake hawakuondoka wakiamini kwamba wamefikia mwisho; walitambua kuwa siku moja wapenzi wao na wale ambao siku ile ya Mapinduzi ilikuwa ni ya majonzi watafanya mipango yote iwezekanayo ya kumrudisha Sultani.

ni kutokana na hilo Sultani wa Zanzibar hayuko Uingereza kama yupo yupo tu; la hasha yuko kule akiwa Uhamishoni yeye na wanawe na watu wanaomfahamu na kumtembelea kule na kufuatilia mambo yake ni watu ambao wanamtambua kama Sultani wao na wapo walioapa kumtambua hivyo mpaka kufa.

Mashabiki na masalia ya ZNP na ZPPP bado wapo leo Zanzibar na hawa hawana tatizo na utawala wa Sultani kwani hawakuwan nalo wakati wa Uhuru.

Kama kura ya maoni inaweza kurudisha serikali ya mseto au umoja wa kitaifa (kama ilivyokuwa baada ya uhuru); nina uhakika wa asilimia 100 kuwa kura ya maoni inaweza kuamua kama Sultani wa Zanzibar ahusishwekatika utawala wa Zanzibar.
 
Kama ilivyo thread yenyewe, haina reference, data unadhani kuna kitu cha maana kinaongelewa hapa?

Zanzibar hakuna mtu anatime na sultani let alone kumjua huyo Jamsheed. Bora tuweke starehe maana kuna watu wamedai zanzibar wanapigwa mawe well mie as far as I know washkaji zangu wengi if not all wakiristo tena mmoja mlokole nikamuonyesha kanisa lilipo kwani alitaka kusali jumapili but life is good zanzibar kama una hela lakini kiukweli hali ni mbaya kwa watu wanaotegemea maisha yao hapo kisiwani na ukienda mashambani ndio worse case inasikitisha kwakweli!!

:rolleyes:

mdondoaji mtu ambaye hajafika Zanzibar ndiye anaweza kusema hayo. Wengine tumefika na kuishi Zanzibar na tuna ndugu na jamaa wapo hapo kwa muda mrefu tu na sijasikia mtu kapigwa jiwe; ndiyo maana utaona sizungumzii mambo ya namna hiyo.
 
Anayo nia ya kufanya hivyo. Ushahidi ni kuwa hajawahi kukana haki na uhalali wake wa yeye na wanawe kuwa watawala wa Zanzibar kama ilivyoanishwa katika makubaliano ya Uhuru ya 1963. Mojawapo ya mambo ambayo watu wanataka kule Zanzibar kwanza ni suala la Serikali ya Mseto. Pili ni kutambua Uhuru wa 1963 kutoka Mwingereza.

Ukweli ni kuwa uhuru ule ulipofanyika ulimretain Sultani kama Constitutional Monarch na hivyo kuwa Head of State. Hilo ni mojawapo ya mambo ambayo ASP iliyapinga sana. ZNP na ZPPP hawakuona tatizo hilo na wakakubali kuunda serikali ya Mseto chini ya Shamte.

Hivyo mapinduzi ya Januari 12 yalikuwa si kuiangusha serikali ya mseto hasa bali ni kuvunja utawala wa Sultani wa Zanzibar kama ulivyokubaliwa na ZNP na ZPPP. Hivyo, hata alipoondoka Zanzibar Bw. Jamsheed kukimbilia Dar na uzao wake hawakuondoka wakiamini kwamba wamefikia mwisho; walitambua kuwa siku moja wapenzi wao na wale ambao siku ile ya Mapinduzi ilikuwa ni ya majonzi watafanya mipango yote iwezekanayo ya kumrudisha Sultani.

ni kutokana na hilo Sultani wa Zanzibar hayuko Uingereza kama yupo yupo tu; la hasha yuko kule akiwa Uhamishoni yeye na wanawe na watu wanaomfahamu na kumtembelea kule na kufuatilia mambo yake ni watu ambao wanamtambua kama Sultani wao na wapo walioapa kumtambua hivyo mpaka kufa.

Mashabiki na masalia ya ZNP na ZPPP bado wapo leo Zanzibar na hawa hawana tatizo na utawala wa Sultani kwani hawakuwan nalo wakati wa Uhuru.

Kama kura ya maoni inaweza kurudisha serikali ya mseto au umoja wa kitaifa (kama ilivyokuwa baada ya uhuru); nina uhakika wa asilimia 100 kuwa kura ya maoni inaweza kuamua kama Sultani wa Zanzibar ahusishwekatika utawala wa Zanzibar.

Hearsay? wishingfull thinking
 
MKJJ pamoja na huyo Lula kusema ukweli mmekuja na hoja nzito sana zilizonifanya niwe a union believer,ni hoja nzito,laiti CCM wangekuwa wanakuja na hoja kama hizi na si kufanya siri siri na wananchi hawajapigwa darasa tosha.
 
Jmushi.. Muungano ulikusudia kuzuia mara moja jaribio la kumrudisha Sultani kwa nguvu. Serikali ya Karume ilikuwa ni dhaifu sana mwanzoni na isingeweza kuhimili onslaught ya watetezi wa utawala wala wa ZNP na ZPP na Sultani.
 
Anayo nia ya kufanya hivyo. Ushahidi ni kuwa hajawahi kukana haki na uhalali wake wa yeye na wanawe kuwa watawala wa Zanzibar kama ilivyoanishwa katika makubaliano ya Uhuru ya 1963. Mojawapo ya mambo ambayo watu wanataka kule Zanzibar kwanza ni suala la Serikali ya Mseto. Pili ni kutambua Uhuru wa 1963 kutoka Mwingereza.

Ukweli ni kuwa uhuru ule ulipofanyika ulimretain Sultani kama Constitutional Monarch na hivyo kuwa Head of State. Hilo ni mojawapo ya mambo ambayo ASP iliyapinga sana. ZNP na ZPPP hawakuona tatizo hilo na wakakubali kuunda serikali ya Mseto chini ya Shamte.

Hivyo mapinduzi ya Januari 12 yalikuwa si kuiangusha serikali ya mseto hasa bali ni kuvunja utawala wa Sultani wa Zanzibar kama ulivyokubaliwa na ZNP na ZPPP. Hivyo, hata alipoondoka Zanzibar Bw. Jamsheed kukimbilia Dar na uzao wake hawakuondoka wakiamini kwamba wamefikia mwisho; walitambua kuwa siku moja wapenzi wao na wale ambao siku ile ya Mapinduzi ilikuwa ni ya majonzi watafanya mipango yote iwezekanayo ya kumrudisha Sultani.

ni kutokana na hilo Sultani wa Zanzibar hayuko Uingereza kama yupo yupo tu; la hasha yuko kule akiwa Uhamishoni yeye na wanawe na watu wanaomfahamu na kumtembelea kule na kufuatilia mambo yake ni watu ambao wanamtambua kama Sultani wao na wapo walioapa kumtambua hivyo mpaka kufa.

Mashabiki na masalia ya ZNP na ZPPP bado wapo leo Zanzibar na hawa hawana tatizo na utawala wa Sultani kwani hawakuwan nalo wakati wa Uhuru.

Kama kura ya maoni inaweza kurudisha serikali ya mseto au umoja wa kitaifa (kama ilivyokuwa baada ya uhuru); nina uhakika wa asilimia 100 kuwa kura ya maoni inaweza kuamua kama Sultani wa Zanzibar ahusishwekatika utawala wa Zanzibar.

Kwa hivyo mkubwa unataka kutwambia kuwa Jamsheed yuko Uingereza kama mkimbizi au?? Na je swali linakuja hao wanaoenda kumuona ni akina nani? Hebu nifahamishe alipo Uingereza maana nina safari huko nikamuulize ulize maswali ya zanzibar maana kama jina lilivyo napenda kudondoa nipate ukweli.

Swali lengine mie binafsi nadhani kama kuna watu wanategemea usultani utarudi wanaota (assuming kama wapo zanzibar) kwani zanzibar imechanganyika mno sasa nadhani usultani utakuwa mgumu hapo. Vilevile matabaka naona kama hayapo si shamba wala mjini. Ukienda sehemu za paje kule kuna mahalf cast wa kiitaliano utafikiri tupo rome sasa sijui nadhani reform itakayofanyika iangalie kwamba zanzibar ni ya wazanzibari na sio waarabu. na there is no such a thing as mzanzibari halisi sote ni wazanzibari.

Tuondokane na kasumba za mapinduzi kwasababu haya ndio sumu ya maendeleo zanzibar. Hivi mnajua hadi leo kuna watu wanaangalia wewe ni nani au baba yako alikuwa nani, nia na madhumuni kutrace kama wewe ni mshirazi au mhizbu, watu hadi leo hawapati kazi kisa kasumba ya umapinduzi iliyobadilishwa into ucuf Vs uccm, come on karne ya 21 si ya mambo haya bali karne ya maendeleo sijui tunaeleweka wengine.
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

Duuh hii ni fitna!
 
Back
Top Bottom