Suleiman Kova :Ninatoa onyo kali dhidi ya maandamano ya MAT na baraza la kiislamu

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam,Suleiman Kova ameonya juu ya maandamano yanayoratibiwa na jumuiya ya madaktari pamoja na yale ya baraza la kiislamu.Kamanda Kova ameamuru kutofanyika kwa maandamano hayo kwani ni ishara ya uvunjifu wa amani kwani masuala yanayowafanya waandamane yapo chini ya mahakama.Kamanda Kova amesisitiza kwamba kama wanataka wafikishe ujumbe kuhusu kulaani kitendo alichofanyiwa Dr.Ulimboka basi wakae kwenye hall,wawaite waandishi wa habari kisha wauwasilishe ujumbe kwa njia hivyo kwani hata yeye ndivyo anavyofanya huwa haandamani.Pia Kova amedokeza juu ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa Genge la Gangster linalomilikiwa na mtu mmoja maarufu kwa jina la SILENCER. Ameongezeka kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi na anahojiwa na polisi. source-Cloudz(taarifa ya habari,jioni ya leo) My Take:Nini jukumu la jeshi la polisi kuhusu maandamano na sheria inasemaje?
 
Nilijua watayazuia tu!!!! Hongera kova!!!!!! Je ukimaliza utaingia siasa kama aliyekupisha? Karibu kwa wananchi kwa kura za maoni!!!
 
basi tutaandamana kumpongeza jk kwa msimamo wake!HAYO NAYO UTAPIGA MARUFUKU?polisi=ccm
 
Hapo kwenye GANGSTER, ungetufafanulia.[/QU GANGSTER ni kundi la kihalifu nchini Kenya na huyo mshukiwa ni raia wa Kenya.Kundi hilo linaendesha shughuli zake za utekaji nyara,utesaji na mauaji kisha wanalipwa na mtu anayewakodi kufanya shughuli hizog
 
Back
Top Bottom