sugu

Angalizo kwa Sugu. Kula,kulala na kuendelea na marafiki wako wa kabla ya Ubunge hakutakuwa na maana kama utashindwa kutekeleza ahadi zako kwa wananchi wakati unaomba kura.
Kaza buti safari ni ndefu kuelekea mafanikio ya kweli.

samahani nje ya mada,wewe ndio ulikuwa unajiita SHY mwanzo au,sio kwa nia mbaya usinitusi
 
Tatizo viongozi wetu wengi wamekuwa "Waheshimiwa Sana" hadi vitu vya kawaida kama kujichanganya na Wananchi vinaonekana mambo ya ajabu...... Well Done Sugu... Keep it Up.

Mkuu,

Hivi ni nani alirejesha haya mambo ya kuitana “mheshimiwa” na “mtukufu rais”.

Siku za nyuma nakumbuka tulizoea kuitana “ndugu”. Na hii ilikuwa imekaa vizuri zaidi. Ilikuwa inaondoa hizi daraja za first class na second class.

Hivi leo tunawaita waheshimiwa hali ya kuwa wao hawatuheshimu,wanatufanya sisi takataka.

Mwenye kumbukumbu, atusaidie hapa.
 
Kuna wengine watasema hii ni populism politics.

Lakini wanaomjua sugu watajua tunaingia katika enzi mpya ya uongozi. Uongozi wa angalau kujaribu - kufanikiwa ni kitu tofauti kabisa- kuwa karibu na wananchi.

Habari zilizoko kwenye pipeline ni kwamba Sugu anasuka kitu kikubwa sana kwa watu wa Mbeya, na kama akipata ushirikiano kutoka kwa watu wa serikali anaweza kufanya makubwa sana katika muda mfupi sana.

Wasiwasi wangu ni kwamba watu wa serikali ya CCM wanaweza kutaka kuleta mambo ya siasa chafu.
 
Wengine wanaogopa kujichanganya kutokana na maovu yao wakuu,lazima waogope wakiangalia jinsi wanavyotafuna mali ya umma.
 
hata akienda tena karibia na uchaguzi 2015 hope watampigia kura, ni sera tuhiyo ndio politics
 
Back
Top Bottom