Sugu Awaka, Amwaga Cheche Bungeni!

Vazi la taifa!! Mpaka huu utawala upite akina kusaga mabilionea! Clouds sasa hv wana justify ongezeko la bei ya umeme! Wanafanya kazi iliyowashinda TBC!
 
Pia amesema Nchimbi kaweka " washkaji" zake kwenye kamati ya vazi la taifa,hawana utaalam wowote

Pamoja na matatizo yote ya msingi tuliyonayo hii issue ya "vazi la taifa" sijui inatokea wapi? !! Hii kitu ingewekwa kando kwanza. Sioni sababu ya hii kitu kupewa kipaumbele kwa sasa mpaka kufikia kuunda "kamati". Kweli taifa masikini linaloendeshwa kwa misaada ya wafadhili linahitaji "vazi" kiasi hiki? Kila mtu avae chochote atakacho hata gunia mpaka tutakapojikomboa kwenye umasikini uliokithiri.. kamati... kamati...:smash:
 
kwanza vazi la taifa si ni rubega na kaniki kwa kina mama,sasa kamti ya nini kama si ufisadi tu.ni kweli watalazimiswa( ofisi za serikali) kulinunua kama gazeti la uhuru

Naamini mama Nyoni na Mariedo yake lazima wapewe hiyo tenda
Nchi hii ni ya ajabu,wakati mjadala wa malipo ya Dowans umepamba moto akaibuliwa Babu Ambilikile na nchi nzima ikahamia huko.
Sasa mjadala wa katiba unatupasua kichwa, tunaletewa vazi la taifa
 
Usidanganyike kijana kuwa kuna mwana siasa yuko pale kukutetea wewe, ile ni kazi yao ya kuwaingizia vipato vya ziada na kuwaongezea umaarufu. Wapi kwingine watapata coverage ya TV na kujiongezea umaarufu huku wanalipwa zaidi ya pale? fikiri.

Nnakuhakikishia hakuna hata mmoja anaegombea ubunge akawa yuko kwa nia ya kusaidia wengine, kwanza ni kujisaidia yeye mwenyewe. Wanafik tu, hawana lolote. Pale ni njia ya mkato.

Rais je? Anatutetea?
 
Kijana usiyekuwa na huruma kwa vijana wenzako,huyu Mh(MB) Mwanaharakati Mtetezi wa wanyonge a.k.a Sugu anawatetea wanyonge wewe unaona ka vile anapiga kelele,kuna siku utakuja kumkubali kwa haya mazuri anayoyafanya

Ng'wanza Madaso, usihangaike na huko 'kikongwe', muda woote kiko online (na si mobile - ni kwenye komputa)! Kinapika saa ngapi, kinakula saa ngapi au muhimu kinafanya kazi saa ngapi. Naona kiko kweye payroll ya magamba.
Kilipaswa kuwa tayari kimestaafu, lakini hilo neno ni msamiati kwenye chama cha mafisadi, hilo ni jambo ambalo haliwezekani.
Kwa taarifa yako huyu kikongwe mwaka 1954 alikuwa tayari ni mtu mzima mwenye akili timamu.
 
Hivi hilo vazi kuna watu watalivaa kweli?
Labda viongozi na wale watakao pewa kama nguo za msaada.
Me?
Over my dead boby.

Hilo vazi litakua so funny,yaani ni colours za bendera tu.Inshort ni beendera ndo kitambaa kinachotumika kushonea vazi hilo.Imagine unapita maeneo yenye population kubwa kama kariakoo,watu wote wamepiga vazi la taifa.Mabendera tu.Inapendeza eeeenh? so funny''''
 
sugu ni jembe! Jinsi anaoongea bila kigugumizi utadhani anamwaga mistari. Nimependa staili yake ya kuongea huku ananesanesa yaani hadi raha.
 
Sugu kawaambia kwenye kamati ya vazi la taifa kumejaa watu ambao hata hawana ujuzi na mambo ya mavazi wamewaacha wabunifu wa kimataifa wakina Mwanamboka, Mustafa Hasanali n.k wapo wakina Kusaga wataaramu wa matamasha!!
 
Wakati wa majumuisho, Nchimbi kaipangua hii hoja na kumopaka sana Sugu kuwa hawezi kuwateua watu makini eti tuu kwa sababu anajua fulani ana bifu na fulani. Pia akapaka hauwezekani ugomvi udumu zaidi ya miaka 10, ukishakuwa mbunge ni kiuongozi wa umma, hivyo sasa wewe ni kioo cha jamii, sahau yaliyopita songa mbele, haya ma bifu mpaka kuimbana na kutukanana matusi mpaka ya nguoni sio mambo!.

Word...!! Hii issue ya kila anapochangia
kuponda wakina Kusaga sidhani ka
inazidi kumjengea...
 
Miaka 50 ya bado tunatafuta vazi la taifa halafu unaleta mchakato wa vazi la taifa kwa wavaa mitumba wapi na wapi mambo mengine ni kutafutiana ulaji usiokuwa na tija yoyote ile...
 
Word...!! Hii issue ya kila anapochangia
kuponda wakina Kusaga sidhani ka
inazidi kumjengea...

sugu ndio waziri kivuri anayewakilisha bungeni, kama hao watu ndio vinara wa ufisadi kwenye iyo wizara unataka akae kimnya?
 
Wakati wa majumuisho, Nchimbi kaipangua hii hoja na kumopaka sana Sugu kuwa hawezi kuwateua watu makini eti tuu kwa sababu anajua fulani ana bifu na fulani. Pia akapaka hauwezekani ugomvi udumu zaidi ya miaka 10, ukishakuwa mbunge ni kiuongozi wa umma, hivyo sasa wewe ni kioo cha jamii, sahau yaliyopita songa mbele, haya ma bifu mpaka kuimbana na kutukanana matusi mpaka ya nguoni sio mambo!.

Of course kuna umuhimu wa kusameheana kwanza kama kiongozi,pili katika hali ya ubinadamu.Lakini kwa ishu ya kusaga na Sugu ina historia ndefu,tangu siku nyingi.Nchimbi ni rafiki wa kusaga thats open.Wakati nchimbi anamponda Sugu amesahau kwamba Clouds fm wako kwenye vita ya kudumu na Sugu,Always lazima wamponde,mara kwa mara na kila nafasi inapotokea.

Halafu kusameheana kunapendeza pale ambapo kila upande unarekebisha makosa yake.Lakini kuna hilli la studio iliyotolewa na JK Lakini Kusaga kajibinafsishia,hawezi kuiachia hiyo studio,kwa hio bado kutaendelea kuwa na mgongano.

Lakini pia nchimbi ameshindwa kujibu hoja na ku attack personality zaidi.Hoja ya Sugu ilikua kamati imeteuliwa kwa upendeleo,pia akapendekeza watu ambao ni ma designers ambao wangestahili kuwepo kama kina mustafa Hasanali na wengine.Nchimbi akaanza kuibua mengine " ooh miaka kumi ilyopita " n.k-in short taarab kama ulivosema hapo juu Pasco.
 
sugu ni jembe! Jinsi anaoongea bila kigugumizi utadhani anamwaga mistari. Nimependa staili yake ya kuongea huku ananesanesa yaani hadi raha.
Ananesa wapi? Katika wabunge wote, huyu ndiye kilaza number moja! Hana cha kuongelea? Kila siku lazima amtaje kusaga?
Nimependa kujembe alichopigwa na wazir, aache ujinga wa kuimbana! Wanaume wanapeana live, siyo kupigana majungu kwenye nyimbo
 
Dada yangu FF, kwani kwako Chadema wanajua kuongea?, wanaojua kuongea si ni CCM tuu?, Chadema wao si ni kupiga tuu kelele?.
Nchimbi katika majumuisho, amemkubali.

Kitu kimoja muhimu tukubaliane, sisi binadamu, sio tuu tunatofautiana uwezo wa kuelewa, bali pia tunatofautiana uwezo wa kiwango cha kusikia, wakati mwingine anasikia kikawaida kwa mwingine ni kelele kama ilivyo kulia na kucheka zote ni kelele!.

Mkuu Pasco;

Afadhali wewe ambae upande wako unafahamika lakini uko flexible na unaweza kusimama na kusema ukweli wa mambo,acha kasoro ndogo ndogo ambazo hizo lazima ziwepo.

Ndugu yetu FF pia ana aina yake ya hulka,anasimama hata kutetea 1+2=12 ingawa hata jibu sio hilo.
 
Ananesa wapi? Katika wabunge wote, huyu ndiye kilaza number moja! Hana cha kuongelea? Kila siku lazima amtaje kusaga?
Nimependa kujembe alichopigwa na wazir, aache ujinga wa kuimbana! Wanaume wanapeana live, siyo kupigana majungu kwenye nyimbo

huyo waziri wako na kusaga wanapiga masufuria?
 
Back
Top Bottom