Suala la posho za wabunge

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
kwa Taarifa zisizo na shaka toka chanzo maalumu, suala la posho za wabunge limeleta mtafaruku katika kikao cha wabunge kupata muhutasari wa kitakachojadiliwa bungeni.kikao hicho kinaendelea sasa hivi. Muda huu wabunge wote wameungana kumtukana ZITTO ambaye ametoa hoja posho zifutwe madaktari walipwe, kuanzia SPIKA hadi PINDA wote wanamuattack ZITTO na wengine kadhaa wanamtukana JANUARI MAKAMBA.

nitawapasha kitakachoendelea, ZITTO kawaambia hamnifanyi lolote na ukweli ndo nishawaambia hivyo.
 
PINDA kawahakikishia wabunge kuwa posho zao mpya zitalipwa kama kawaida, kikao hicho kimemalizika muda huu na ZITTO amesema liwalo na liwe historia ndio itaamua kuwa nani na nani walikuwa wanafiki hapa duniani.

Kwa nilio yaona leo hapa ama kweli watanzania mmkwisha hawa viongozi wenu kuanzia PINDA, MAKINDA na wengi wa wabunge ikiwamo RAGE hakuna mwenye kuwajali zaidi ya matumbo yao.

MADAKTARI GOMENI WENZENU WANAPANDISHIWA POSHO BUNGENI
 
Mimi nilijua tu hawa watoto/vijana watapata matatizo ,Tatizo la Nchi hii wazee ndo wao wanjua kila kitu.Vijana ambo mko Bungeni achane na fikira za kizamani Jaribuni kulitetea Taifa letu ,kweli linaangamia wewe unasikia watu wanosema ukweli wanatishwa kulishwa sumu.Ya mwakyembe,Mwadosya,Sitta wote hawa sio wazima,sitta mwenyewe kila wakati Jasho linamtoka sijuwi ndo basi tena.
Naomba Zitto nawezako kazeni boot tuondoe huu umafia na ubabe wa hao .
 
zitto alichofanya kama taarifa yako ni sahihi ni chema sana. Lakini kusema wabunge wote wanamtukana, nadhani ni vema ukafafanua walikuwa wakina nani. Ina maana hata wabunge ambao yeye ni N/katibu mkuu wao wamemtukana? Hebu nyoosha maelezo!
 
Tunajua fika kuwa Pinda hakuwa na dhamira ya dhati katika kutatua tatizo la madaktari na ndio maana akatumia ubabe katika maamuzi yake,hivi Pinda huyu huyu si aliwahi kujifanya kukataa kukutana na madaktari?Kilichomfanya ajifanye anatambua mgogoro toka mwanzo na kushindwa kuchukua hatua ni nini?
Shame on you viongozi wote wachumia matumbo yenu na Mungu atawalaani.
 
kama waliweza kuwalipa wabunge kwanini washindwe kulipa madakitari
laki mbili kwa kukalisha makalio yao hapo kwenye sofa hata awana aibu
yaani wao ndiyo mafisadi number mmoja wanalojadili akuna wanabaki
kutukamua madakitari wana hoja jibuni hoja na msiwatishe watatuuwa
hao,

kwanza wenye wake wajawazito hakuna haja ya wasi wasi akitaka kujifungua
msaidie ajifungue kwani kama uliweka kwani nini ushindwe kumzalisha wanaume
tusitishike jipange sawa sawa msaidie mkeo kama mkishindwa basi wasiliana na ngamia
mzee kw a msaada zaidi
 
Narudia tena kusema kwa masikitiko makubwa kwamba katika suala hili la posho CHADEMA wamenisikitisha sana. Mtihani wa posho wameushindwa kabisa na wamedhihirisha wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi, wamejidai kwamba kataa posho ni ajenda ya chama kumbe wamemuachia Zitto peke yake.
 
Bila shaka huyu pinda,makinda....hawa sio watanzania,warud kwao plz..pinda n makinda rudisheni 280000/
 
Unafiki.! Unafiki.! Unafiki mtupu, Pinda anajifanya ana huruma mbele za watu kumbe Loh.! Roho yake inafanana na sura yake.! Hivi wabunge kujimwagia mipesa kiholela eti kwa kisingizio cha kupanda gharama za maisha kama sio matusi, kejeli na dhihaka kwa watanzania ni nini.?

Wengi wa wabunge ni vihiyo wasiojua hata kujenga hoja, kazi kutetea matumbo yenu tu, mkishikwa na minyoo kidogo haoo India, wapiga kura wenu hamuwakumbuki tena, Wabunge mnatutia hasira sana.. HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA SIASA KUWA NI BIASHARA, WAPUUZI WANATAKA KURUDISHA PESA WALIZOHONGA WAKATI WA UCHAGUZI.

Je tuwaache waendelee??
 
Wabunge wote wa chadema wanaoshabikia posho by 2015 wote chali nikianza na Joseph Roman Selasini......, bro Ben u knw what im saying!!
 
Narudia tena kusema kwa masikitiko makubwa kwamba katika suala hili la posho CHADEMA wamenisikitisha sana. Mtihani wa posho wameushindwa kabisa na wamedhihirisha wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi, wamejidai kwamba kataa posho ni ajenda ya chama kumbe wamemuachia Zitto peke yake.

Katika suala la upambanaji lazima aonekane kinara, kwa hivi kwa maoni yangu si sahihi sana kuwatuhumu wabunge wa CDM kuwa kaachiwa Zitto pekee kwa posho za wabunge, kumbuka hata mgomo wa madaktari Dr Ulimboka kajitoa sana na si kwamba yuko peke yake hapana! Wabunge wote wapenda watanzania wako nyuma ya Zitto na Januari, na siye pia watanzania tuko nyuma yao.
 
Wabunge wote wa chadema wanaoshabikia posho by 2015 wote chali nikianza na Joseph Roman Selasini......, bro Ben u knw what im saying!!

Wachumia matumboni wote wanaoiasi torati ya CHADEMA kwa kuungana na wana wa magamba katika kutaka kuendelea kuchukua marupupu huku wakisahau kuwa ni kodi za mvuja jasho, next election {2015} wote nusu kaputi kuitimiza ilani iiteteayo kodi ya mvuja jasho.
 
Watanzania tuache upumbavu, anae waraumu chadema ni mjinga, maana kila mtu anajua kinacho endelea badala ya kukemea hizi posho wewe unaenda kujadiri ee chadema nao wanachukua huu ni ujuha na upumbavu, ndo huyuhuyu anangonjea eti kila kitu lazima dr Slaa aandamane badala kila mtu awe responsible tuache mambo ya ugamba tuwe serious na siyo eti tusubiri chadema
 
Back
Top Bottom