Suala la mmiliki feki dowans: Wahariri walihongwa

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mwanahabari mmoja kuwa wahariri walioalikwa kwenye press conference ya mtu aliyejitambulisha kama mmiliki wa Dowans walihongwa Sh. 500,000 kila mmoja ili kuhakikisha wanaipa uzito habari hiyo potofu. Inasemekana mialiko iliratibiwa na mhariri wa gazeti la Tanzania Daima ambaye ni swaiba wa Rostam. Bila shaka kuna wanahabari wengine wana taarifa zaidi kuhusiana na press conference hiyo, na maelezo ya kwa nini mmiliki huyo hakutaka kupigwa picha.
 
Huhitaji kutumia kichwa sana kufikiria kujua kuwa huu ndo ukweli kwani;
  • Habari ilikuwa ya kishabiki mno
  • Habari haikuwa na kichwa; kama kilikuwepo hakikuwa na macho
  • Vyombo vingi vya habari viliitoa kama leading headline wakati ilikuwa na mazonge zonge (Mtu hataki kupigwa picha, yet habari yake inaongoza)
  • Facts nyingi ambazo tayari zinajulikana kuhusu Dowans hazikuzungumzwa wala kuhojiwa
Yaani, it was like, watu wameambiwa kaandikeni hivi!!
 
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mwanahabari mmoja kuwa wahariri walioalikwa kwenye press conference ya mtu aliyejitambulisha kama mmiliki wa Dowans walihongwa Sh. 500,000 kila mmoja ili kuhakikisha wanaipa uzito habari hiyo potofu. Inasemekana mialiko iliratibiwa na mhariri wa gazeti la Tanzania Daima ambaye ni swaiba wa Rostam. Bila shaka kuna wanahabari wengine wana taarifa zaidi kuhusiana na press conference hiyo, na maelezo ya kwa nini mmiliki huyo hakutaka kupigwa picha.

Duh kweli hii balaa, na mwandishi wa mbowe (tanzania daima) nae amejiingiza kwenye ufisadi, kweli kuna safari ndefu ya ukombozi
 
Hawa wahuni wanadhani bado wanaweza kupeta kwa udanganyifu huu wa kijinga. Wanadhani yanayotokea Misri, Tunisia na sasa Libya hayawezi kutokea huku!

Utawala wote unaolea uovu na kulibeba kundi fulani la jamii huishia kuaibika na kuangushwa
 
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mwanahabari mmoja kuwa wahariri walioalikwa kwenye press conference ya mtu aliyejitambulisha kama mmiliki wa Dowans walihongwa Sh. 500,000 kila mmoja ili kuhakikisha wanaipa uzito habari hiyo potofu. Inasemekana mialiko iliratibiwa na mhariri wa gazeti la Tanzania Daima ambaye ni swaiba wa Rostam. Bila shaka kuna wanahabari wengine wana taarifa zaidi kuhusiana na press conference hiyo, na maelezo ya kwa nini mmiliki huyo hakutaka kupigwa picha.

Idadi ya wahariri walikuwa wangapi? Hii itatusaidia kujua jinsi Watanzania wanavyoweza kupewa senti kidogo na kuuza mpaka utu wao
 
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mwanahabari mmoja kuwa wahariri walioalikwa kwenye press conference ya mtu aliyejitambulisha kama mmiliki wa Dowans walihongwa Sh. 500,000 kila mmoja ili kuhakikisha wanaipa uzito habari hiyo potofu. Inasemekana mialiko iliratibiwa na mhariri wa gazeti la Tanzania Daima ambaye ni swaiba wa Rostam. Bila shaka kuna wanahabari wengine wana taarifa zaidi kuhusiana na press conference hiyo, na maelezo ya kwa nini mmiliki huyo hakutaka kupigwa picha.

MzeePunch,

Nilimsikiliza Mhariri Machumu (wa Citizen/Mwananchi) akiongea na Charles Hilary (BBC) - Alisema kuwa wana-habari walialikwa na "Editors Forum". Na hii "Editors Forum" ndiyo ilikuwa na mandate ya nani wa kumualika na kutomualika. Kwahiyo ninavyoona mimi huyo Mwenyekiti wa hiyo "Editors Forum" anayo majibu mengi sana kuhusu Adawi/DOWANS/ROSTAM na kuhusu "kutopigwa picha"!
 
Hivi mwenyekiti wa hiyo Editors' Forum ni nani? Simsikii Sakina Datoo siku hizi, bado yupo?
 
Ghafla nimeukumbukaule wimbo ..japo siyo kwa mistari sahihi
" hapa nilipo ni katikati ya msitu na nyika,
mbele yangu kuna simba
nyuma yangu kuna nyati
kulia kwangu kuna faru......sijui nifanyaje nipate kuokoka...."
Jamani waandishi mlioshiriki hiyo 'press conference' semeni neno kuhusu kauli ya MzeePunch. Ni kweli?????
 
hyu hapa jamaa mwenyewe
_40194912_dewji203ok.jpg
 
ni kweli tulisikia RIZ 1 amesafiri kwenda Dubai tena kwa ulinzi mkali kama mtoto wa Ghadafi vile..lol kumbe alikuwa anakwenda kumleta huyo msaniii
anything can be possible in tz
MzeePunch,

Nilimsikiliza Mhariri Machumu (wa Citizen/Mwananchi) akiongea na Charles Hilary (BBC) - Alisema kuwa wana-habari walialikwa na "Editors Forum". Na hii "Editors Forum" ndiyo ilikuwa na mandate ya nani wa kumualika na kutomualika. Kwahiyo ninavyoona mimi huyo Mwenyekiti wa hiyo "Editors Forum" anayo majibu mengi sana kuhusu Adawi/DOWANS/ROSTAM na kuhusu "kutopigwa picha"!
 
Daily News na HabariLeo hawakuandika habari hiyo. Sijui hawakualikwa au ilikuwaje!
 
Kwa mtu mwenye akili timamu, ni dhahiri kwamba habari ya mmilki feki wa Dowans ilikuwa na kasoro nyingi za kiuandishi. Hata magazeti yaliyo makini kama Mwananchi yaliingizwa mkenge na kuwa na ushabiki. Eti mtu anakuambia anamilki kampuni yenye hadhi kubwa duniani halafu anasema hataki apigwe picha kwa kuwa ni “mfanyabiashara mdogo” na Mhariri anakubali kuandika hivyo. Kingine cha kutia aibu: hivi mwandishi makini au mhariri makini si angeweza kuipata picha ya huyo jamaa nje ya hicho chumba cha mahojiano? Au kampuni hiyo haina tovuti ambako picha ya mmilki wake yupo. Huyo jamaa anasema kwenye taarifa yake kwamba yeye NDIYE MMILKI PEKEE wakati Waziri Ngeleja alituambia wako watatu? Mbona alimtambulisha Stanley Munai kama Afisa tu wa kampuni hiyo na sio mwenye hisa? Pia tunaambiwa jamaa alianza biashara 1977, akiwa Brigedia. Hivi inawezekana? Hizo pesa alizipata wapi akiwa Mwanajeshi wan chi masikini kama Oman?
Kwa ufupi, waandishi na wahariri wa Tanzania wamechakachuliwa. Ni aibu sana. Lakini swali linakuja, kwani ni wapi hakujachakachuliwa?
 
MzeePunch,

Nilimsikiliza Mhariri Machumu (wa Citizen/Mwananchi) akiongea na Charles Hilary (BBC) - Alisema kuwa wana-habari walialikwa na "Editors Forum". Na hii "Editors Forum" ndiyo ilikuwa na mandate ya nani wa kumualika na kutomualika. Kwahiyo ninavyoona mimi huyo Mwenyekiti wa hiyo "Editors Forum" anayo majibu mengi sana kuhusu Adawi/DOWANS/ROSTAM na kuhusu "kutopigwa picha"!
Mwenyekiti wa hiyo forum ni nani?
 
Back
Top Bottom