Suala la Magufuli ni VITA YA URAIS 2015!

Habari zenu wana JF!

,Mnavyosoma kichwa cha habari hapo juu 2015:Raisi Magufuli,Membe Balozi na Lowassa Mkuu wa Mkoa!
Sina Nia Mbaya ya Kumsema Mtu vibaya au Nimetumwa Kumsifia Mtu flani...,Bali nimefanya Utafiti,Upambanuzi na Kupima hawa mafahali watatu na Kupata Jibu lenye kichwa cha Habari hapo Juu!

Kwanini ninasema kwamba 2015 Rais Mh.John Pombe Magufuli..Why /Kwanini?
Tanzania Tunahitaji Mh.John Magufuli Atuongeze Kama Rais katika Kupunguza kasi ya Umaskini,Kuinua Uchumi,Kupinga Ufisadi na Ubadhirifu katika serikali Pamoja na Kusimamia Shughuli za Kiserikali ipasavyo! ninaweza Kumfananisha Mh.Magufuli na Mh.Paul Kagame Raisi wa Rwanda kwa mitazamo,uchapakazi, na kusimamia sheria na mipango ipasavyo!

Siku zote watanzania tumekuwa watu wa kutofata sheria,natural ni watu wapole,wakarimu na sifa yetu kubwa ni kuchangia sana kwenye maharusi na masherehe kuliko kwenye shughuli za kimaendeleo...ni watu wa kulalamika sana,hatupendi kujituma na kufanya kazi ipasavyo zaidi kuilemea serikali! tunahitaji Kiongozi Ambaye ni Mbabe,Asiye cheka na Mtu na Asiye Fisadi..na kumwangalia Magufuli sifa zote hizo anazo kwa kuangalia utendaji wake serikali kuanzia 1995 paka 2011...,siku zote ameonyesha jitihada katika utendaji wake...hebu tujikumbushe
+Mh.John Magufuli alikuwa ndio kiongozi wa kwanza serikalini kama nafasi yake kama waziri kulipua uozo wa magari ya serikali kugeuzwa magari ya watu binafsi
+kuanzia mwaka 2000 paka 2005 mh.john magufuli aliiongoza wizara iliyokuwa na mafanikio makubwa kuliko wizara nyingine..wakati huo alikuwa anaongoza wizara ya miundombinu! hadi kuweza kukipa nafasi chama chake cha CCM kupata kura nyingi mwaka 2005 kwenye uchaguzi wa raisi...,kutokana na uchapa kazi wake hadi mh. raisi kikwete kumrudisha tena kwenye wizara hiyohiyo
+Na alipokuwa wizara ya uvuvi,kilimo na mifugo...,mh.John Magufuli alioongoza zoezi la kupinga uvuvi haramu na alifanya mwenyewe kwa vitendo
Jamani yako mwengi mazuri tu kuhusu huyu bwana hana kesi yeyote ile ya ufisadi zaidi ya lile suala la nyumba ni kama anaekewa zengwe kisiasa! tukimpa nchi magufuli watanzania tutaacha uvivu...nchi itakwenda kwa mipango na sheria

+Tukija kwa Mh.Membe! huyu anafaa kuwa balozi...,kama tunavyojua CCM wanastyle ya kupeana mashavu mara kiongozi anapoanguka...,Mh.Membe amekuwa ni mchapakazi pamoja na Public Figure nzuri sana kwa Tanzania nchi za nnje! pamoja na Msimamo wake dhidi ya Mataifa ya Magharibi Kama juzi kati alivyopinga suala la ushoga pamoja na kupinga kuingunga mkono libya...huyu Mheshimiwa atatufaa sana kuwa balozi hasa nchi za marekani na uingereza iwapo ataposhindwa kupenyeza kwenye duru ya uraisi...

+Tukija kwa Mh.Edward Lowassa! Sio Siri na Ni jambo linalojulikana...,Mheshimiwa ni mchapa kazi na kiongozi hodari sana...tatizo ni kashfa za ufisadi pamoja na ujilimbikizaji mali...,itakuwa ngumu kama mh.EL atapewa nafasi kubwa kama Rais ni bora kumpa nafasi nzuri kama ya Mkuu wa Mkoa ambayo itamwezesha asiijihusishe na mikataba mibovu ya rushwa pamoja na kashfa itakayoweza kuzicost taifa ! Kwa hiyo bila shaka Kama M.EL atashindwa kwenye Duru ya Uraisi...,Mh.John Magufuli ataweza kumfariji na nafasi ya Ukuu wa Mkoa! ili apambane na watendaji katika halmashauri pamoja na kusimamia ipasavyo miradi na majukumu mbalimbali ya serikali...,!

Kama hili jambo litaweza kutokea litaepusha Mpasuko ndani ya CCM! na vilevile kujenga safu nzuri ya Uongozi Tanzania...
 
Namkubali sana Magufuli. Nchi hii sasa inapaswa kuongozwa na watu wa aina yake. Tuache mambo ya ushkaji tuchape kazi ili tupige hatua kubwa ya maendeleo. Wasiwasi wangu ni kwamba sijui kama CCM wanaweza kulipitisha 'JEMBE' hili ligombee urais.
 
ndoto hizo kwa magufuli kuwa raisi alafu akawageuka wenzake msahau mabadiliko ya nchii hii yataletwa na dk slaa au mtu yeyote kutoka chama pinzani basi, lakini siyo kutoka ccmA na ccmB
 
Mungu anaipenda Tanzania...!
Ndio maana siku zote Nchi yetu imekuwa kisiwa cha amani ukilinganisha na nchi nyingine Afrika..!

Niwapongeze sana Mh.John Magufuli na Mh.Harrison Mwakyembe kwa kuonyesha kwamba nyie ni wazalendo wa kweli,viongozi ambao hili taifa linawahitaji,wenye kujituma na nyie ni Baraka kwa hili Taifa...,

Nyie ndio watu ambao mmekuwa mkimpa sapoti kubwa Mh.Dk.Jakaya Mrisho Kikwete huku baadhi ya mawadhiri na viongozi wakimtosa na kuanza mbio za uraisi..,lakini nyie mmeamua kuachana na ujinga wa uraisi na kufanya kile watanzania wanachokitaka..!

Achaneni na maneno ya watu..,

Mimi naamini Mungu yupo na sisi..,ili Tanzania iendelee tunahitaji Mh.Dk.John Magufuli awe rais na Dk.Harrisson Mwakyembe awe waziri mkuu 2015...! tuachanane na mafisadi wenye kutumia pesa chafu za wizi kuwahadaa watz...,
 
Magufuli hafai kabisa, ana kiherehere, visasi na wivu wa ajabu sana huyo anaweza kuwapeleka jera watanzania wote wanaonukia wali
 
Umetumwa au unatumika kama siyo kujikomba? Mambo ya magamba waachie magamba wenyewe. Rais mzuri hawezi kutoka Magamba piga ua. Kama unapenda sana rais toka Magamba basi mpendekeze Salma Kikwete au Anna Mkapa.
 
2015 ni CHADEMA , Hao watafaa wawe viongozi wakuuu wa chama kikuu cha upinzani yaani CCM ili tuwe na upinzani imara.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mungu anaipenda Tanzania...!
Ndio maana siku zote Nchi yetu imekuwa kisiwa cha amani ukilinganisha na nchi nyingine Afrika..!

Niwapongeze sana Mh.John Magufuli na Mh.Harrison Mwakyembe kwa kuonyesha kwamba nyie ni wazalendo wa kweli,viongozi ambao hili taifa linawahitaji,wenye kujituma na nyie ni Baraka kwa hili Taifa...,

Nyie ndio watu ambao mmekuwa mkimpa sapoti kubwa Mh.Dk.Jakaya Mrisho Kikwete huku baadhi ya mawadhiri na viongozi wakimtosa na kuanza mbio za uraisi..,lakini nyie mmeamua kuachana na ujinga wa uraisi na kufanya kile watanzania wanachokitaka..!

Achaneni na maneno ya watu..,

Mimi naamini Mungu yupo na sisi..,ili Tanzania iendelee tunahitaji Mh.Dk.John Magufuli awe rais na Dk.Harrisson Mwakyembe awe waziri mkuu 2015...! tuachanane na mafisadi wenye kutumia pesa chafu za wizi kuwahadaa watz...,



HIVI KWELI UMETUMWA ETI??? LAKINI kweli HAWA VIONGOZI wanajitahidi japo wamo ndani ya uchafu na hawa ndo bora kuliko magamba megine (hambu hambu).
 
Magufuli No! ana mbwembwe! anapenda misifa! aliuza nyumba za umma! hafai kuwa president!
 
Ndio maana siku zote Nchi yetu imekuwa kisiwa cha amani ukilinganisha na nchi nyingine Afrika..!


Acha kujidanganya wewe, kama kuna amani mbona mnaweka fence mpaka zinazuia nyumba? mbona mnaweka magrili mpaka vyumba vya kulala achilia mbali mlango wa mbele na nyuma?, acha ukasuku hapa hamna amani wala nini ni kautulivu kidogo tu.

Nchi zenye amani zilishakataza kuweka magrilli milangoni na madirishani ili iwe rahisi kuokolewa just in case of emergence.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom