Kujadili dini ni mojawapo ya mijadala inayokwepwa na baadhi ya wanajamii ili kuepusha shari na kudumisha amani. Lakini linapokuja swala mahusiano hususan pale watu wawili wenye imani tofauti za kidini wanapotaka kuoana, unaweza kuzuka mjadala mzito miongoni mwa ndugu na jamaa wa wapenzi hao na wakati mwingine hata marafiki hutokea kupinga muunganiko huo.
Ninao mfano unaonihusu. Mdogo wangu anayenifuatia kuzaliwa alipata mchumba (mume) mwenye imani tofauti na imani yetu, jambo hilo lilizusha mtafaruku katika familia yetu kila mmoja akisema lake. Ilitokea tu mimi na baadhi ya ndugu zangu akiwemo baba tuliafiki ule muunganiko wao na ndoa ikafungwa na sasa ndoa yao ni imara na imetimiza miaka tisa mwaka huu wakiwa na watoto watatu.
Ukweli ni kwamba jambo hili limekuwa likileta mtafaruku katika baadhi ya familia na wakati mwingine familia hujikuta ikisambaratika hasa pale ambapo familia moja inashindwa kukubali utashi wa mtoto wao kuolewa au kuoa mtu mwenye imani tofauti na mara nyingi hii hutokea katika familia zenye msimamo mkali wa kidini. Kama inavyofahamika mapenzi ni kitu cha ajabu sana. Pale ambapo penzi linapochipua hufunika imani zetu kiasi cha kujikuta wakati mwingine tunazisaliti imani hizo ambazo hata hivyo baadhi yetu hazikuwa utashi wetu bali tu tumejikuta tukiwa humo kwa sababu ni imani ambazo tumezaliwa na kukuta wazazi wetu wakiwa ni wafuasi wa imani hizo.
Huu ni mtihani mgumu sana kwetu na mara nyingi waathirika wa mtihani huu wengi wao ni wanawake na watoto ukilinganisha na wanaume. Wakati mwingine huwa najiuliza inakuwaje mtu anampata mpenzi anayempeda sana na mwenye sifa azitakazo lakini anashindwa kufunga naye ndoa kwa sababu ya kuwa na imani tofauti? Lakini pia wapo ambao wanalazimika kufunga ndoa na wapenzi wao sio kwa sababu wamependana, bali ni kwa sababu tu imani zao zinafanana !
Kuna wanawake wengi sana wa kiasi cha kutosha wanalazimika kuishi katika ndoa ngumu kwa sababu ya imani zao, kilichowavuta kuingia katika muunganiko huo ni imani zao lakini sio upendo. Lazima tukubali kwamba mapenzi ni kitu kingine na imani ni kitu kingine. Kuingia katika ndoa kwa kigezo cha imani kunakuwa na changamoto zake ambazo mara nyingi hazina matokeao mazuri.
Naamini hata humu JF wapo ambao wamewahi kukabiliana na mtihani huu au wako katika hati hati ya kukabiliana na mtihani huu. Hebu tupeane uzoefu juu ya jambo hili linalowatatiza wengi.
Swali: Iwapo wewe ni single, Je uko tayari kufunga ndoa na mtu mwenye imani tofauti na imani yako? Je umejiandaaje kukabiliana na changamoto za wazazi, ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla watakapopinga muunganiko wenu ?
Nisingependa mjadala huu uwe ni wa kidini.
Nadhani mmenielewa.........
lakini vipi Mlutheri na Mkatoliki kuna tatizo?
Mkuu baba yako angekua mdini angeoa Mkristo? Au una maanisha ni mshika dini? Maneno mengine angalia mkuu ukikosea kidogo tu unaleta tafsiri nyingine.
Wote ni makafiri, hakuna mwenye dini hapo. Ndoa ilifungwa msikitini au kanisani? Najua haikufungwa popote pengine ni ya kiserikali. Wanapohitaji msaada au ushauri wa kiroho wanaenda wapi?mi sikubaliani na wewe hata kidogo,hizo ni hadithi tu za kufikirika,mi baba yangu ni muislam na mama yangu ni mkristo na ni mdini kweli kweli na wapo kwenye ndoa yao zaidi ya miaka 40....kwa ushahidi huu wa wazazi wangu unafikiri mi ntakuunga mkono?
Sometimes kuna shida..labda kama wote wazazi ni watu wa dini rasharasha. Lakini ukikuta mlutheri kweli kweli itakuwa ugomvi maana hatataka watoto wake wakabusu sanamu. Na mkatoliki atalazimisha mwanae akabusu masanamu.Mkuu hapa hakunaga shida hata chembe...haya madhehebu ni ndg kabisa haya.
Yaani eti nianze tu kufunga ndoa na jini la kiislamu???? Haiwezekani
Uko sahihi kabisa!Swala Dini kwenye ndoa ni suala muhimu sana, katokana mambo yafuatayo
1. Kuwalea watoto katika mstari na kuwahimiza kumpenda Mungu.
Watoto wanaplekwa Msikini wana ambiwa "Mkristo ni kafili," na wengine wanaplekwa kanisani wana ambiwa "Yesu ni njia ya kweli na uzima" Wote wakirudi nyumbani ,Wana wauliza wazazi wao upi ni ukweli? kulingana na mafundisho kila mtu aliyoyapata.Wazazi wanabaki kuangliana . Hii inaleta picha mbaya kwa watoto.
2.Kuepuka migogoro ya ndoa hasa pale Mzee yupo kwenye Mfungo wa Ramadhani na mama yupo kwenye Mambo ya Kiinjili (kanisani)
3.Mafundisho ya Dini ni tofauti kila fundisho la dini moja,linakashifu dini nyingine.
Mfano. Waislam wanasema Wakristo ni makafili, na mafundisho ya kiislamu yanasema Muhislamu safi hawezi kushare vitu na Kafili hasa .Tendo la ndoa na some times Chakula.NB. Baadhi ya mafundisho ya Dini fulani yanakataza kula baadhi ya vyakula e.g kitimoto.
Na Baadhi ya Dini inasemekana kwamba Wanafuga Majini, Ibada za kikristo zinafukuza Majini.
kwa Mtaji huo nyumba Haiwezi kusettle.
Muhimu: Watu watakaa kwenye ndoa wakiwa na dini tofauti if and only if.Watahamua wote kuweka Dini zao pembeni na kuamua kujiunga na Dini nyingine ya Upagani(fiftyfifty uisilamu na aukristo) lakini huwezi ukuwa Mkristo Deep au Muhislamu Deep, ukiishi kwenye ndoa kama hiyo.
Kwa hiyo natoa ushauri, ndoa iwe za watu wenye imani moja!! unless kila mtu aache misingi ya Dini yake. waamue kuwa Wapagani.
Regards,
jangakuu
Mtimti, ebu chunguza vizuri maisha ya wazazi wako, itakuwa lazima kuna mmoja si muumini wa kweli yaani hayuko serious sana na dini, kama mmojawapo anazingatia imani yake.
Lakini kama wote ni waumini watiifu ki kweli kweli kwa dini zao, shida ipo sana tu!
Kutojali kwa mmojawapo wa wazazi wako ndo kumesaidia katika hilo!
Huyo ni mjinga anatafuta kisingizio,kwani kuna shida gani wote ni wa Yesu?Mie mrutery, mchumba RC, yeye tunapendana sana, ila wakati huo hataki kwenda kinyume na matakwa ya wazazi wake. tumejaliwa mtoto, ila ndoa imekwama kwa sababu ya msimamo huo wa matakwa ya wazazi. najua nawa confuse kwa kusema tunapendana ila dini zinatutenganisha, kuna mengine ya ndani yanayoashiria hayo ila kwa kusimulia uta conclude kuwa hakuna upendo hapo!
Hivi ni Dini ndizo zikakazowafanya muone Mbingu? Au ni Yesu ambaye wote wawili mnamtumikia na kumuabudu kuwa ni Mkombozi wa maisha yenu? Sijaelewa hapa.Mie mrutery, mchumba RC, yeye tunapendana sana, ila wakati huo hataki kwenda kinyume na matakwa ya wazazi wake. tumejaliwa mtoto, ila ndoa imekwama kwa sababu ya msimamo huo wa matakwa ya wazazi. najua nawa confuse kwa kusema tunapendana ila dini zinatutenganisha, kuna mengine ya ndani yanayoashiria hayo ila kwa kusimulia uta conclude kuwa hakuna upendo hapo!
Umeandika nilichokiwaza. Thanks.Huyo ni mjinga anatafuta kisingizio,kwani kuna shida gani wote ni wa Yesu? Hajaelewa bado imani ni nn!
Uko sahihi kabisa. Imani gani inayozungumziwa? Kama imani ya dini basi ukiona kuna mgawanyiko, elewa uelewa ni mdogo kwa mmoja wao. Kama uelewa ni mkubwa, Dini haitakiwi kuwa jambo la kumhusu mwingine tofauti na wewe.mi sikubaliani na wewe hata kidogo,hizo ni hadithi tu za kufikirika,mi baba yangu ni muislam na mama yangu ni mkristo na ni mdini kweli kweli na wapo kwenye ndoa yao zaidi ya miaka 40....kwa ushahidi huu wa wazazi wangu unafikiri mi ntakuunga mkono?
very true, i have the same experience, so mm sioni shida watu wakipendana, dini si kigezo cha kuachana km wawili wanapendana.mi sikubaliani na wewe hata kidogo,hizo ni hadithi tu za kufikirika,mi baba yangu ni muislam na mama yangu ni mkristo na ni mdini kweli kweli na wapo kwenye ndoa yao zaidi ya miaka 40....kwa ushahidi huu wa wazazi wangu unafikiri mi ntakuunga mkono?
very true, i have the same experience, so mm sioni shida watu wakipendana, dini si kigezo cha kuachana km wawili wanapendana.
dini or dhehebusi sababu ya kufunja mapanzi ya dhati, ni jins ya kufanya chaguo lako sahihi tuu vile unataka . kama mtu aona ana msimamo mkal na dini or dhehebu lake, fanya kumtafuta yule unaedhani atafata ule upande ulioko wewe, so in the future wasije kutulilia hapa JF -MMU, au siyo jaman.