Style ya kulala na tabia ya mtoto

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,893
Wakuu hivi nikweli kuwa tabia ya mtoto/ binadamu yeyote inaweza kujulikana mapema kutokana na style ya kulala kwa huyo mtoto.

Sina uhakika sana wapi niliiona hii kitu kama ni kwenye mavitabu au humu Jf hivyo kama kuna mtu anachochote anisaidie ili niweze kuanza kumsoma mwanangu kipenzi!!
 
Hebu fafanua vizuri hii style gani unayozungumzia? kifudifudi,chali,kulala kwenye banko au nini?
 
vyote ulivyovitaja hapo z

Basi haina uhusiano wowote! Tabia unatokana na malezi na mazingira(umasikini,utajiri,uswazi,geti kali,hali ya ndoa,masuala ya dini,elimu n.k).
Na tabia ya mtoto huwa inatengenezwa/inajengwa kuanzia mimbani mpaka miaka 5.
 
kWA MAANA YAKO MTOTO WA Jeet Patel atakuwa fisadi?
Mtoto wa Sita atakukuwa kigeugeu?
Mtoto wa Anna kilango atakuwa mropokaji?
Mtoto wa Simba atakuwa anatukana sanaaaaaa?
au
 
kWA MAANA YAKO MTOTO WA Jeet Patel atakuwa fisadi?
Mtoto wa Sita atakukuwa kigeugeu?
Mtoto wa Anna kilango atakuwa mropokaji?
Mtoto wa Simba atakuwa anatukana sanaaaaaa?
au
Sina maana hiyo,Ngoja nitoe mifano.nikisema umasikini nachukulia mfano wa ombaomba wa barabarani,ni rahisi sana wale watoto kujengewa mazingira ya ujambazi,uvivu,uchangu n.k tofauti na mtoto wa reginad Mengi ambaye hana hatari kubwa kama hiyo.
Nikichukulia mfano wa uswazi,maisha ya watu wa kule ni ya kutojali,kwangu mimi sio mazingira mazuri ya kulea watoto.watoto wa kule ni wanatukana hawana heshima,ni kucheza muda wote hawataki kusoma.Japo kwenye geti kali kuna hatari ya kuharibu tabia ya watoto lakini ni rahisi kudhibiti.
sijui nimeelewka?
 
Back
Top Bottom