steve nyerere kwny hili umechemka

nimemsoma michuzi leo asubuhi pale kwenye blog yake anasema kuwa the great hakuwa mnywaji wa pombe,na steve nae jana amesema alimkuta anakunywa,duuuuhhhh UTATA huuu.TUSHIKE LIPI?
 
kwa maoni yangu mastaa wengi wa bongo wana uwezo mdogo sana kwenye communication, hawajui kujieleza, hawajui waongee nini kwenye kadamnasi. hilo tatizo lipo sana tu. na chanzo ni wao kutopenda kujiendeleza kielimu, wanaridhika na vijisenti na misifa wanayopata.
 
nimemsoma michuzi leo asubuhi pale kwenye blog yake anasema kuwa the great hakuwa mnywaji wa pombe,na steve nae jana amesema alimkuta anakunywa,duuuuhhhh UTATA huuu.TUSHIKE LIPI?

kwani kinachonywewa ni pombe tu? yaweza kuwa maji, togwa, juice, kahawa nk.
 
wakati anajitahidi kuelezea jinsi alivyosikitishwa na kifo cha the great K, akajikuta anasema... ''yani juzi tu tumekutana maisha club sisi tuko chini yy yuko juu anakunywa pombe na kucheza mziki wa twanga...'' mi nadhani angeweza kusema mengine ya maana ukizingatia alikuwa anasikika radion. wasanii wajifunze uchaguzi wa maneno hasahasa wanapotoa maoni yao ktk vyombo vya habari.

Nyie ndo mmezoe kudanganywa majukwaani!
yeye ameeleza last moment kukutana na Marehemu,
sasa ulitaka akwambie wamekutana kanisani anacheza Gospel na kupiga kinanda ndo yangekufaa masikioni mwako!
ameeleza ukweli mara ya mwisho wamekutana wapi which ver true!
 
Jamani the Great alikuwa Muumini wa Kanisa la AIC (AFRICA INLAND CHURCH TANZANIA) alikuwa muimbaji wa kwaya ya Chang`ombe AIC miaka ya nyuma na alikuwa hanywi pombe kulingana na Imani ya Kanisa hilo! sasa Katika uchunguzi wa awali wa POLICE (Mwananchi) inasemekana alikuwa amekunywa WHISKY... sasa my take huyu jamaa bado alikuwa active Kanisani kwake? (Hawaruhusu pombe), kama ndiyo hivi mara ya mwisho alikwenda Kanisani kwake (Any AIC church) lini? kwa anyejua atujuze!
 
Kinywaji ni kinywaji na ndo burudani aloipenda....wala sio tabu kunywa bia kama wengine wasivyoona taabu kuywa juice aua soda.
 
Hajakosea mkuu,kunywa au kucheza kwa kanumba sio hajabu nyinyi ndio mtu akifa mnaanza kusema oh marehemu alikua mtu fresh sana wkt still una bifu nae la kufa mtu!

SI wengine huko maisha club hatukujuimi nilidhani labda huko juu twanga hawakuwepo!!!! ila kama ishu ni kusema kilichotokea wala hakuna shida kabisa.
 
Steve nyerere alimwelezea steven kanumba jinsi alivyo kutana naye mara ya mwisho kuwa jamaa alikutana naye maisha club wao wakiwa chini na kanumba akiwa juu akicheza muziki na kunywa pombe.nafikili amejitahidi kueleza kile anachokumbuka mara ya mwisho kuonana na kanumba.Jamani tusiingize siasa ambapa haitakiwi.tuwe wakweli kwani kuna ajabu gani kwa kanumba kulewa?alikuwa binadamu kama wengine.
 
tatizo watanzania wanapenda kudanganya, na kutokusema ukweli! Je unafikiri lulu akiulizwa unamkumbuka je marehemu mara ya mwisho atajibu je?
Mimi nimeamua kupambana na watu kama hawa wanao generalise mambo, watanzania, wabongo. Sasa hapa watanzania wanaingiaje mkuu?kwanini unasema watanzania wanapenda kudanganya? Mimi najijua na nawajua wengi tu wa kweli.

Cha kupinga hapa ni unafiki wa watu, huyu alitaka Nyerere sijui aseme nini.Huu ndio tunaita unafiki.Unamuona mtu yuko uchi humwambii yeye unawahi kupiga picha na kupeleka gazeti la udaku!
 
Wasanii wa Bongo bwana duh! stadi za mawasiliano badoo..waende shule!
 
Back
Top Bottom