Steve Kanumba: Historia; Kazi zake na Mengineyo

Allien

JF-Expert Member
Jul 6, 2008
5,546
1,861
Kanumba%20%2861%29.JPG


Kamumba hatunaye tena, lakini kazi zake zitaishi na ataenelea kukumbukwa kwa mengi. Katika thread hii napenda tuzungumzie yote yanayomhusu Kanumba ikiwepo Historia yake, kazi zake, Awards, Kazi za Kijamii, mahusiano yake na jamii, Kanumba kama Kioo cha jamii nk.

Kanumba%2089.JPG



Kwa kuanzia hii ni Profile yake kutoka katika Website yake:

Steven Charles Kanumba (born January 8, 1984), is a multi award winning Tanzanian actor, with a career spanning more than a decade. Kanumba has received numerous awards, including; Best Actor of the Year, 2006, Best Actor in Tanzania Award, 2007, Best Artist of the Year Award, 2007/2008.


Kanumba began acting at an early age, acting in as many church plays as he could, until he had the opportunity after leaving school to act and train with the Kaole Sanaa Group and receive special training with Dr Nyoni at the University of Dar es Salaam which served as a major stepping stone for his mainstream acting career.


Kanumba began his acting career with appearances in a host of local Tanzanian soap operas like, Jahazi, Dira and Tufani just to name a few. He then expanded his horizon by venturing into the film industry, his first movie being Haviliki, which was just the beginning of great journey, for "The Great".


Not only is Kanumba a Tanzanian household name, but he's also acted in Nollywood (Nigeria) with some of the greatest names on the Nollywood scene which expanded his career and experience from just being a Tanzanian star to an African star with ambitions of acting in Hollywood.

Having achieved so much before the age of thirty, Kanumba feels that he's only just begun. He looks forward to a long and fruitful career in every area of the film industry.


Not only is he a successful film star and producer, he is also very active in philanthropy. He has recently been named the OXFAM GROW ambassador for Tanzania.

Kanumba extends his love and gratitude to each and everyone that has helped along the way in his career; "first and foremost The Lord God, My Family especially my Mother, Chrissant Mhengga, Kaole Sanaa Group, Mr & Mrs. Mtitu G Game, Sharifa Kalala, Sanura Husein, Vicent Kigosi, Producers, Directors, Artists, Friends and Loved ones and last but not least my fans all around the world".
 
Baadhi ya Kazi zake:


moses.png



Cast: Steven Kanumba, Shazy Sadry, Upendo Moshi, Ndumbagwe Misayo and Bakari Makuka.
Director: Steven Kanumba
Writer: Ally Yakuti
Rating: PG-18
Running Time: 110 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2011.

Synopsis:

Moses is grown man that hates women, but it is all because of his rough background and childhood, his parents did some things that made him hate all women.


Moses becomes a philosopher and workaholic that do not believe in GOD, but only in the books he reads and widens his horizon from.
 
devile.png



Cast: Steven Kanumba and Ramsey Noah
Director: Steven Kanumba
Writer: Ally Yakuti
Rating: PG-18
Running Time: 120 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2011.

Synopsis:


A young man working hard to have it all in life but isn't very successful, looks at his peers which are multimillionaires and doesn't stop asking himself why he isn't as successful as they are. He begins questioning GOD, and wondering if is he not praying as much as the others and as a result he is not as rich!


He starts a church but it doesn't generate much income, and so he asks one of his millionaire friends how he can be successful like them. His friend opens up and tells him it's not the work of GOD but that of another power. He tells him that if he wants to be like them he has to join their secret society. He agrees and they give him everything; healing power, an increase in the number of church members, money and the good life but in return he has to make some sacrifices! After some time he is required to sacrifice an albino, which he finds impossible, so the secret society tells him to sacrifice his parents instead, he then tries to quit but they tell him there is no getting out - once you're in, you're. So he goes back to his church and kneels before GOD
 
the%20shock.png



Cast: Steven Kanumba and Shaz Sadry.
Director: Steven Kanumba
Writer: Ally Yakuti
Rating: PG-15
Running Time: 113 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2011.

Synopsis:


A lady is involved in a long distance relationship because her man is always traveling on business. The lady gets tired of that, she gets involved with another man and dumps her longtime lover.


Some time passes and the lady goes on a business trip to South Africa. While she is out there working her new boyfriend finds another girl and decides to dump her, so the new boyfriend begins a new relationship but soon finds out that his new lady is a prostitute and so the man decides to dump her and to find his past girlfriend. Sadly the girl had gotten back together with her first boyfriend and was already pregnant by him. So the man lost everywhere and ends up with no one to love.
 
young%20billionaire.png



Cast: Steven Kanumba, Aunty Ezekiel and Patcho Mwamba
Director: Steven Kanumba
Writer: Steven Kanumba
Rating: PG-18
Running Time: 112 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2010.

Synopsis:


A wealthy young man gets tired of getting his heart broken by women and decides to settle down with a beautiful girl he falls in love with.


The lady is a superstar that is always in the media because of all the scandals she gets caught in. The young man does not know about all her scandals and gets blinded by love. He ignores everything he is told by everyone including his best friend who tries to show him that she is not the right woman for him. The lady keeps cheating on him but he still wants to marry her. All goes well until on the day of the wedding he catches her sleeping with his best friend
 
deception.png



Cast: Steven Kanumba, Rose Ndauka, Patcho Mwamba and Bakari Makuka.
Director: Steven Kanumba.
Writer: Elizabeth Chijumba
Rating: PG-18
Running Time: 109 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2011.

Synopsis:


A story of a beautiful married woman who decides to cheat with a handsome young man. The young man dates married women because they can provide for him.


One day when they are out enjoying themselves the lady dies and everyone thinks that it is the handsome young man that killed her, the police get involved and an investigation carried out. In the end they find out that her husband is the murderer.
 
offside.png



Cast: Steven Kanumba, Vicent Kigosi and Irene Uwoya.
Director: Vicent Kigosi
Writer: Ally Yakuti
Rating: PG-18
Running Time: 111 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2010.

Synopsis:


A story about two young men and their father. They argue a lot about their father's decision to bring another woman into the house and start living with her as his wife. The first son tries to understand his father's decision but the second one refuses and a fight breaks out in the family. The second son decides to have an affair with his father's lover. Together they plan to kill him and succeed. The second son then suspects that there is something not fishy about his father's death and then starts looking into it.


When the lover learns that the first son is investigating his father's death, she decides to seduce him as well. One day the second son catches them together and he gets furious knowing that he and his brother are having an affair with the same woman, their father's lover. The woman then kills the second son too and the first son learns truth about his father's death. In the end they find out that they are related, she was the daughter of their father to a woman he had abandoned a long time ago.
 
uncle%20jj.png



Cast: Steven Kanumba, Hanifa Daudi and Othman Njaidi
Director: Steven Kanumba
Writer: Steven Kanumba
Rating: All Ages
Running Time: 102 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2010.

Synopsis:


Uncle JJ is a man living in the rural areas with his niece and nephew. He believes that educating a girl is just waste of time and money, so he only takes the boy to school and he leaves the girl at home.


Their neighbors do not agree with him and try to advise him otherwise but he doesn't listen to them. The girl starts fighting for her rights to have an education and that sparks war in the house. Uncle JJ eventually gives in and decides to take the girl to the city to one of his relatives so that the girl can go to school there. He leaves everything in the boy's care. On his return he's shocked to find that the boy has sold their house and property and has he disappeared.
 
this%20is%20it.png


Cast: Steven Kanumba, Hanifa Daudi and Othman Njaidi
Director: Steven Kanumba
Writer: Steven Kanumba
Rating: PG-10
Running Time: 101 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2010.

Synopsis:


A story about an Uncle that tries to raise his late sister's kids (a girl and boy). Living with them has become an issue because of the little girl's behavior.


The little girl starts doing weird and scary things, and even kills someone. The uncle decides to take the young girl to hospital so she can get treatment, when the doctors discover that she don't have mental problems they try any they can on her but with no success. The uncle takes a further step and gets a priest to pray for her thinking it might help. They find out from the priest that the girl's mother had resorted to witchcraft in order to get pregnant as she was barren. As a result her daughter was born demon possessed. After a lot of prayers from the priest the girl is delivered from the demons and becomes a sweet little girl.
 
weka video clips ndio nitakukubali zaidi..kial siku naona mikamera ila sijui hizo video clips zinaishai wapi
 
more%20than%20pain.png



Cast: Steven Kanumba, Lisa Jensen and Rose Ndauka
Director: Steven Kanumba
Writer: Ally Yakuti
Rating: PG-18
Running Time: 102 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2010.

Synopsis:


Two teenagers studying at a seminary school fall in love and start messing around, the girl gets pregnant and she gets expelled from school. Soon the boy responsible gets caught and he also gets expelled from school, and they soon start living together.


Life get harder and harder for them and the boy tells the girl he cannot take care of her and the child so he suggests they get an abortion. The girl refuses to get an abortion and they get into an argument, after which the boy tricks her into drinking something that causes her to miscarry. Before long they learn that the girl is pregnant again which makes the boy furious, he punches her on her belly which causes her another miscarriage. Soon after that she falls pregnant again, this time the guy chases her away and tells her he never wants to see her again. Years pass by and the guy gets married and becomes successful but isn't able to have any more kids. His wife leaves him and he decides to look for and reconcile with the lady he chased away long ago when she was pregnant with his child.
 
Awards:

jwiaward.png




2011, Best Actor Of the Year (Baab Kubwa Magazine Awards)

2011, Best Movie Of the Year (Baab Kubwa Magazine Awards)

2011, The Best Film (Mini Ziff Film Awards)

2010, BEST MALE ACTOR FilamuCentral Bora za 2010 Awards

2010, BEST FILM PRODUCER FilamuCentral Bora za 2010 Awards

2010, Clouds FM's Best Actor

2010, Best Actor (Smiling Face Company)

2010, African Stars Entertainment (ASET) Certificate Of Appreciation

2008, Best Artist of the Year 2007/2008 (Federation of Artist in Tanzania, SHIWATA)

2008, Honorary Award (Tanzania Film Vinara Awards)

2007, THE BEST ACTOR (Hollywood John Wayne International Awards)

2006, BEST ACTOR of the Year(Baab Kubwa Magazine Awards)

2006, IJUMAA Sexiest male bachelor of the year (Global Publishers Tanzania)


 
dev1.png


Msome Kanumba Mwenyewe anavyoandika:

Ndugu mashabiki wangu ile filamu yetu niliyomshirikisha Ramsey Nouah toka nigeria ''Devil Kingdom''imeingia katika tamasha la kimaifa la filamu nchini ghana lijulikanalo kama Festival of Films Africa(FOFA). Tamasha hili litaanza tarehe moja mwezi March hadi tarehe 4 March jijini Accra - Ghana ambapo mastaa mbalimbali wa movie toka Africa na nje ya Africa watakuepo, katika tamasha hili filamu nyingine toka Ghana, Nigeria, Africa Kusini, Kenya, Diaspora nk nazo zimeingia humo.
 
Steven Kanumba

From being a normal person in Ngokolo-Shinyanga to become the most successful actor in Tzee film industry. Here's our fourth highest earner in 2011 ni Steven Charles Kanumba.

attachment.php


Tollywood heartthrob grossed more than TZS 280 million between November 2010 and November 2011 kupitia filamu za "Devil Kingdom': "Moses': "Offside': "Deception""Uncle JJ': and "Because of You" (all produced by his own film company), pamoja na endorsement deals kutoka Star times, Zantel and TSN Supermarket.

attachment.php


Kanumba who said to have a plan ya kugombea ubunge mwaka 2015 katika jimbo la Shinyanga mjini, kwa sasa tayari ameshawajengea nyumba wazazi wake, he has 3 plot in Dar, na ndani ya mwaka jana pekee "Young Billionaire" superstar ametumia zaidi ya million 100 kununua vifaa vya production for his film company, zikiwemo proffessional cameras,cranes, lights, monitors na usafiri.

The Great who's ex-flame of Wema Sepetu, just recently aliongeza idadi ya his classy rides baada ya kuvuta mkoko mpya aina ya Land cruiser V8 yenye thamani ya millioni 70 za kibongo.
 
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kamaKaole Sanaa Group.

Kanumba alijibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzaniana amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.

Alikuwa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to Lagos, She is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.
 
kanumba%2BS.jpg



Kanumba.jpg



Steven Kanumba a.k.a Denzel Wshington wa Bongo (Tz), alitembelea Hoolywood, Marekani ambayo ni sehemu inayoongoza kwa mambo ya filamu diniani kote. Kanumba akiwa Hoolywood ametembelea studio kadhaa kama vile Warner Brothers na Universal studios. Hakika Kanumba kwa sio tu kwamba alijitangaza yeye lakini pia aliitaitangaza nchi yetu ya Tanzania na kujulikana katika ulimwengu wa filamu.
 
"SERIKALI ITUUNGE MKONO"-STEVE KANUMBA October, 22, 2007


Filamu za kitanzania zina historia ndefu tofauti na wengi wanavyofikiria. Kama mtakumbuka (kwa waliokuwepo enzi hizo) kuliwahi kuwepo na filamu kama vile Fimbo ya Mnyonge (1974), Harusi ya Mariam(1983) na Yomba Yomba(1983) na nyinginezo ambazo ziliwahi kutamba sana enzi hizo. Baadaye idara ya filamu ikapotea kabla ya kupigwa kikumbo na sanaa ya maigizo(wataalamu wanasema kuna tofauti kubwa kati ya maigizo na filamu). Lakini hivi karibuni enzi za filamu za kitanzania zimerudi,tena kwa kasi. Kama kulivyo na Hollywood (Los Angeles, USA), Nollywood (Lagos, Nigeria) na Bollywood (Mumbai, India), hivi leo inasemekana kuna Bongowood (Dar-es-salaam,Tanzania).
kanumba4bc1.jpg


Mmoja kati ya waigizaji wengi wa filamu nchini Tanzania ambao wanasaidia kuzirudisha enzi hizo ni kijana Steven Charles Kanumba. Kwa wafuatiliaji wa filamu za kitanzania, hili jina na sura (pichani) sio geni hata kidogo.Lakini Kanumba ametokea wapi na anaelekea wapi?

Yeye mwenyewe anapasha kwamba alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 8 January mwaka 1984. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Bugoyi huko huko Shinyanga. Baadaye alijiunga na shule ya sekondari Mwadui ambapo alisoma kwa miaka miwili tu kabla ya kuhamia katika shule ya Dar-es-salaam Christian Seminary alipomaliza elimu yake ya awali ya sekondari. Baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari Jitegemee kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

Ingawa alianza kuigiza tangu utotoni, safari yake katika fani hii aliianza rasmi mwaka 2002 alipojiunga na kundi maarufu la sanaa za maigizo la Kaole. Hivi karibuni tulifanya naye mahojiano ambapo tulizungumza naye mengi kuhusu kazi yake ya uigizaji na maisha yake kwa ujumla. Tulipomuuliza kuhusu habari iliyokuwa imetawala kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania miezi michache iliyopita kuhusiana na uhusiano wake na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu na pia "beef" kati yake na msanii mwenzake aitwaye Frank inayosemekana kusababishwa na wao wawili kumgombea mrembo huyo,hakusita kutupatia majibu yake. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC : Kanumba karibu ndani ya BongoCelebrity
SK : Ahsanteni sana.

kanumba2bc.jpg


BC : Kwanza kabisa tungependa kujua, kuna tofauti gani kati ya Steve Kanumba muigizaji na Steve Kanumba wa kawaida, huyu tunayeongea naye hivi sasa ?

SK : Steve Kanumba unayeongea naye ni tofauti kabisa na Steve Kanumba muigizaji.Kwanza maisha anayoishi Kanumba ni tofauti kabisa na maisha anayoishi kwenye filamu au michezo mbalimbali ya kuigiza. Kanumba wa kawaida ni kijana mtanashati,anayejipenda,aliye na heshima kwa mkubwa na mdogo na pia anamheshimu na kumuogopa Mungu.Situmii kilevi cha aina yoyote ile.Sivuti bangi wala sigara.

Sasa kwenye filamu unaweza kukuta naigiza yote hayo niliyoyataja hapo juu na mengineyo.Ni uigizaji tu.

BC : Mpaka hivi sasa umeshashiriki katika filamu ngapi ? Unaweza kuzitaja ?

SK : Mpaka hivi sasa nimeshacheza filamu kama 16 hivi. Kati ya hizo 12 zimeshatoka na kuonekana wakati 4 bado hazijatoka ingawa zimeshakamilika na zipo mbioni kutoka.

Kwa majina filamu ambazo nimeshawahi kushiriki ni Neno,Riziki,Ulingo, Johari part I, Johari part II, Sikitiko Langu, Dangerous Desire,Dar 2 Lagos(hii nimecheza na Wanigeria),My Sister part I, My Sister part II,Penina na Cross My Sin. Hizo ni kwa upande wa ambazo zimeshatoka. Kwa upande wa ambazo bado hazijatoka ni A Point of No Return(hii nimecheza na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu), The Director(hii nimecheza na Wanigeria tena), Twins na Signs of Times.

kanumba6.jpg



Cover ya mojawapo ya filamu ambazo Kanumba ameshiriki.​

BC : Katika zote hizo, ipi ilikuwa ni ngumu zaidi kwako kuigiza ? Kwanini ?

SK : Kila filamu ina ugumu wake katika kuigiza.Lakini ambayo nadhani ilikuwa ngumu zaidi nadhani ni Cross My Sin.Sababu ni kwamba character niliyopewa ilikuwa ni character ambayo sijawahi kuicheza kamwe. Hapa niliigiza kama padri.Sasa kuna ugumu wa kuigiza kama padri ukilinganisha na tuseme kuigiza kama mchungaji. Hii inatokana na jinsi ambavyo mapadri wanavyoishi nk.

Nyingine iliyokuwa ngumu ni The Director.Hii ni kwa sababu filamu hii naweza kusema ni filamu ndani ya filamu(a movie within a movie).Katika filamu hii nashiriki kama muongoza filamu (director) wa filamu inayoitwa Paradise of Love wakati huo huo na mimi napigwa picha na director mwingine ambaye ndio original director wa filamu yenyewe. Hii ilikuwa ngumu sana kuigiza kwani ilihitaji ufundi wa ziada.

BC : Baada ya kuwa umeshashiriki katika filamu nyingi kiasi hicho, unaonaje maendeleo yako kama msanii tangu ulipoanza mpaka hivi sasa. Una mabadiliko gani katika uigizaji wako ? Na je unadhani mchezo au filamu gani ndio haswa unaweza kusema imekufikisha hapo ulipo ?

SK : Mabadiliko yapo,tena makubwa sana.Kwanza utaona kwamba mimi nilipoanza nilianzia kwenye kucheza tamthiliya na hivi sasa nimeacha kucheza tamthiliya na badala yake nacheza filamu peke yake.Kwa maana hiyo nimekaa kibiashara zaidi. Hii ni tofauti na hapo awali ambapo bila malipo yoyote kila mtu alikuwa anaweza kuniona kupitia tamthiliya za kwenye luninga. Hivi sasa ili aone ninachofanya inabidi anunue filamu.

Mabadiliko mengine ni kwamba katika filamu kila mara nacheza kitu kipya kila mara tofauti na kwenye tamthiliya ambapo role inakuwa ile ile kwa muda mrefu sana.Kisanii pia nimeongeza ujuzi,nimeweza kucheza na kwa mfano waigizaji kutoka nchini Nigeria ambao kimsingi ni wazoefu zaidi katika mambo ya uigizaji. Hili limenipa changamoto zaidi katika kuboresha kazi zangu.

Filamu ambayo nadhani ndio ilinitoa zaidi ni filamu ya Johari (zote mbili yaani part I na II).Sababu ni kwamba kwanza filamu yenyewe ilikuwa ni nzuri na ilishirikisha mastaa wengi sana wa filamu nchini Tanzania. Pia promosheni ya filamu yenyewe ilikuwa ni ya nguvu jambo ambalo lilipelekea mashabiki kujitokeza kwa wingi kutaka kuiona na kwa bahati nzuri wakatokea kuipenda pia.

BC : Umaarufu huwa unaambatana na mambo mengi sana, mengine mazuri na mengine mabaya. Kwa upande wako unajisikiaje kuwa muigizaji maarufu nchini Tanzania mpaka hivi sasa na je familia yako inakabiliana vipi na umaarufu wako ?

SK : Mimi binafsi najisikia faraja kuwa muigizaji.Uigizaji ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu.Pia nashukuru kwamba uigizaji ndio umenisaidia kuwa hapa nilipo hivi leo.Uigizaji huo huo umeweza kunijengea sifa na heshima mbele ya makundi mbalimbali ya watu wakiwemo viongozi wa kiserikali,mataifa mbalimbali na jamii kwa ujumla.

Kuhusu jinsi ambavyo familia yangu inakabiliana na umaarufu wangu ni kwamba kwanza kabisa nashukuru kwamba familia yangu inanielewa na inaelewa kwamba nikiingia ndani ya nyumba naingia kama mtoto na mwanafamilia na sio staa au muigizaji.Katika raha na shida tunashirikiana kama wanafamilia.Lakini pia nashukuru kwamba familia yangu akiwemo mama yangu mzazi anaelewa kwamba kutokana na kazi zangu kuna wakati nakuwa busy sana kiasi kwamba naweza hata kushindwa hata kuhudhuria baadhi ya shughuli za kifamilia nk.Familia yangu inaelewa kwamba kikitokea kitu kama hicho kinakuwa sio kwa makusudi.Nawashukuru sana kwa hilo.
kanumba5bc.jpg


BC : Katika ulimwengu wa uigizaji imeshawahi kutokea mara nyingi sana watu waliogiza katika sinema moja kama wapenzi wakatokea kupendana kikweli katika maisha ya kawaida. Je wewe imeshawahi kukutokea hiyo ? Kama hapana unawezaje kuzuia hisia zako hususani kama unaigiza na msichana ambaye unavutiwa naye kimapenzi ?

SK : Mimi binafsi haijawahi kunitokea. Nadhani inakuwa ngumu kitu kama hicho kutokea kwa sababu kwanza anayeigiza pale anakuwa si mimi bali Kanumba muigizaji ambaye anakuwa amepewa jina lingine na kila ninachokifanya pale ikiwemo ninachokiongea kinakuwa kimeandikwa katika script ambayo kama muigizaji sina budi kuifuatilia.Kwa maana hiyo ninachokifanya pale kinakuwa sio hulka yangu wala hisia zangu binafsi bali script inavyonielekeza na pia maelekezo kutoka kwa waongozaji(directors). Hayo ndio maoni yangu.Lakini mbali na hapo kama ikitokea watu wakapendana hiyo inakuwa ni makubaliano yao wenyewe ambayo sio lazima yaanzie kwenye kurekodi filamu.Kama unavyojua love does not ask why.

BC :Je imeshawahi kutokea ukacheza character ambayo kwa namna moja au nyingine unaona ilifanana sana na ulivyo wewe mwenyewe kama Steve Kanumba ? Ni ipi na ilikuwa ni katika filamu gani ?

SK : Ndio nadhani ishawahi kutokea katika mchezo mmoja wa kuigiza ambapo niliigiza kama mtoto kipofu ninayenyanyaswa na kuteswa na mama yangu wa kambo. Hiyo nadhani iliakisi kwa kiasi fulani maisha yangu binafsi kwani kitu mithili ya hicho kishawahi kunitokea hapo zamani.

BC : Katika uigizaji wa filamu mara nyingi inabidi upakwe make-up kwa sababu ya taa na mambo kama hayo. Kama kijana wa kiume wa ki-Tanzania make-up sio utamaduni wetu. Ilikuwaje kwako mara ya kwanza ulipopakwa make-up na je kitendo hicho kilikuathiri kwa namna yeyote ile hususani siku hizo za mwanzo ?

SK : Unajua fani ya uigizaji unapoiingilia ni kama vile mtu anayeingia shuleni.Kuna sheria na taratibu zake.Unaambiwa hapa utavaa suruali ya khaki na shati jeupe.Sasa wewe unaweza ukawa hujazoea kuvaa vitu kama hivyo lakini ili upate ulichokifuata (elimu) huna budi kufuata masharti ya shule.Hali ilikuwa ni hivyo hivyo kwangu nilipoingia kwenye masuala ya uigizaji filamu.Ilinibidi nifuate sheria na taratibu za uigizaji ili picha ziwe na ubora unaotakiwa na mambo kama hayo.Kisaikolojia haikuniathiri sana kwa sababu nilijua nilichokuwa nikikifuata.Kimwili ndio, kwa sababu mwanzoni nilikuwa sijui vizuri make-up zipi zinaendana na ngozi yangu na zipi haziendani kitendo ambacho wakati mwingine kilinisababishia vipele usoni.

BC : Suala la ubora(quality) wa filamu za Tanzania zikilinganishwa na filamu za kutoka Hollywood (USA), Nollywood (Nigeria) na hata Bollywood (India) bado linalalamikiwa na wapenda sinema wengi. Kwa maoni yako, unadhani wenzetu mpaka leo,hususani wanigeria kwa mfano, wanatushinda nini ? Nini kifanyike ili tuongeze ubora wa filamu zetu hususani kwenye mambo kama sauti na upigaji picha kwa ujumla ?

SK : Kwanza kabisa ni vifaa wenzetu wanavyotumia.Vifaa vyao kidogo viko advanced ukilinganisha na vyetu.Lakini naomba nieleweke kwamba hapa sisemi kwamba movie industry nzima ya Tanzania haina vifaa vyenye ubora,la.Hapa nchini pia tuna makampuni yenye vifaa vizuri mno na wanatengeneza movies zenye viwango vizuri tu wakati mwingine kuliko hata hizo nchi ulizozitaja.

Wakati huo huo hata katika hizo sehemu zingine ulizozitaja na hususani Nigeria (hawa ndio tunaonekana kushindana nao zaidi) sio kila movie yao ni yenye viwango.Kuna movie nyingine za Kinigeria ukianza tu kuitazama unakuwa huna hata hamu ya kuendelea kuitazama.Hali ni hiyo hiyo hata Hollywood au India.Kuna movies ambazo hazina viwango kabisa.Kwa hiyo tatizo la ubora halipo Tanzania tu au Nigeria tu bali ni kila sehemu. Kwa hiyo, kwa sababu movie industry ya Tanzania ndio kwanza inaanza kukua inakuwa rahisi sisi kufananishwa na wenzetu hao uliowataja na wakati mwingine hata kukatishwa tamaa kwamba hatuwezi kuwafikia wenzetu.

Mimi naamini kwamba tunakua kisanii, kivifaa na production kwa ujumla.Mabadiliko yanaonekana na ninafikiri baada ya miaka michache tutakuwa tumesonga mbele sana.Kwa hiyo mimi napinga mtazamo kwamba filamu zote kutoka Nigeria zina viwango.Zipo nzuri na zipo mbovu.Hali itakuwa hivyo hivyo hata hapa kwetu,sio kwamba baadaye kila filamu itakayokuwa inatengenezwa itakuwa yenye viwango bora.Kuna nyingine zitakuwa hivyo na zingine zitabakia kuwa za kawaida au mbovu kabisa.

BC : Unadhani ni kwanini basi Wanigeria wameweza sana kujitangaza kimataifa kuliko sisi ?

SK : Cha kwanza ni support wanayoipata wenzetu kutoka katika serikali yao.Mimi nimeenda kule Lagos, Nigeria na kujionea mwenyewe.Serikali ya wenzetu nadhani imeona kabisa jinsi movie industry inavyoweza kutumika kuitangaza nchi,kutoa ajira kwa vijana na watu wazima kwa ujumla.

Nitakupa mfano mmoja,hapa nchini hatuna hata tuzo ambazo ni kutoka serikalini.Serikali yetu bado haioni umuhimu wa movie industry. Kupata location(sehemu) ya kufanya shooting bado ni tatizo kubwa sana.Ukitaka kwa mfano kushoot filamu maeneo kwa mfano pale Coco Beach unakatazwa,ukitaka kufanya hivyo hivyo uwanja wa ndege, mahakamani huruhusiwi.Wenzetu wa Nigeria kwa mfano wanapewa mpaka magwanda ya polisi au jeshi kwa mfano ili kuonyesha ile reality.Sisi hapa ni marufuku kabisa.Kibaya zaidi ni kwamba mtu huyo huyo anayekunyima vitendea kazi kama hivyo anakuja anakuambua nyie movie zenu haziwezi kufikia za Hollywood nk.Zitafikia vipi kama uzalendo hakuna ndani ya nchi na wala serikali yenyewe haitoi support ? Serikali ndio baba wetu,haina budi kujitokeza kikamilifu na kutuunga mkono kwa hali na mali kwani isitoshe sisi ndio tunasaidia sana kuitangaza nchi yetu hivi sasa.Kupitia movie mtu anaweza akaona mbuga za wanyama,milima nk na hivyo akashawishika kuja kuitembelea na mambo kama hayo.
kanumba7.jpg


Cover ya filamu ya Dar 2 Lagos ambayo Kanumba alicheza kwa kushirikiana na waigizaji wa Nigeria.

BC : Unaongeleaje suala la malipo ya kazi za usanii wa kuigiza filamu nchini Tanzania ? Malipo yanaridhisha ? Vipi kuhusu suala la piracy.Mnakabiliana nalo vipi ?

SK : Naweza kusema japo malipo ni kidogo lakini tunashiba.Movie industry hapa nchini bado ni changa.Kadiri siku zinavyozidi kwenda itazidi kukua na hivyo mapato nayo yataongezeka.

Suala la piracy mpaka hivi sasa bado ni suala la kibinafsi. Mpaka hivi sasa imekuwa kama ni jukumu la mtu mwenyewe kuilinda kazi yake isichukuliwe kwa matumizi yasiyoruhusiwa(piracy). Hapa pia serikali haina budi kuingilia kati katika kutekeleza sheria za haki miliki ilizoziunda. Bila kufanya hivyo ni wazi kwamba kazi za wasanii zitaendelea kuibwa jambo ambalo linaua industry nzima.

kanumba3bc.jpg


BC : Umesema umewahi kwenda na kufanya kazi na wenzetu wa Nigeria. Ulijifunza mambo gani ulipokwenda Nigeria na kufanya kazi nao ?

SK : Nimejifunza mambo mengi sana.Cha kwanza ni kama nilivyosema hapo juu,nimejifunza jinsi serikali ya wenzetu inavyowasaidia wasanii wao kiasi kwamba wamewajengea kabisa eneo moja kubwa kwa ajili ya shughuli zao za kisanii.Nimejifunza kuhusu ushirikiano miongoni mwa wasanii.Nimejifunza zaidi jinsi ya kusimamia malipo ya wasanii.Nimejifunza pia mambo mbalimbali kuhusu kuongoza filamu na jinsi ambavyo wenzetu wanafanya.Kwa mfano wenzetu hivi sasa wanatengeneza movie hata kwa kutumia helikopta !Nimejifunza pia jinsi ya kuwa commited katika kazi. Lakini cha muhimu zaidi nimejifunza mengi zaidi katika fani yangu ya uigizaji filamu.

BC : Katika fani ya uigizaji sinema ni waigizaji gani, kimataifa na nchini Tanzania ambao unapenda zaidi kazi zao ? Kwanini ? Kati ya hao ni wapi ambao ungependa kufanya nao kazi katika siku za mbeleni ?

SK : Kwa kimataifa napenda kazi za Ramsey,Genevive,Desmond Eliot na Mercy Johnson(wote hawa kutoka Nigeria).Nawapenda hawa kwa sababu nawaona kuwa waigizaji makini na pia wakipewa role fulani wanajikita ndani yake kisawasawa.Yaani wanajivika ile role vilivyo na sio kijuu juu.Kwa upande wa Tanzania wapo wengi lakini kwa uchache tu navutiwa zaidi na Ray na Monalisa. Ningependa kufanya kazi na Ramsey na Genevive.Nimeshafanya kazi na baadhi ya hao niliowataja.

BC : Sasa naomba uniruhusu tuongelee kidogo kuhusu habari mbalimbali kuhusu maisha yako binafsi. Kumekuwepo na habari nyingi sana kuhusiana na ugomvi wako na msanii mwenzako Frank kuhusu Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. Unaweza kutueleza chochote kuhusu suala hilo ? Ukweli uko wapi ?

SK : Kwanza kabisa naomba niseme kwamba sijawahi hata siku kugombana na mtu yeyote kwa sababu ya mwanamke. Kilichotokea ni kwamba Frank nilimuondoa katika filamu yangu ya A Point of No Return kutokana na utovu wa nidhamu.Nikiwa kama muongozaji msaidizi wa filamu hiyo(mimi ni muongozaji msaidizi katika kampuni ya 1st Game Quality) nilimchukua Wema Sepetu ili aigize katika filamu hiyo.Tukawa tumeshaingia naye mkataba na advance ya malipo tumeshampa.

Sasa Frank akawa anamsumbua Wema Sepetu kwa kumtongoza na mambo mengine kama hayo.Matokeo yake ikawa wazi kwamba Wema atashindwa kuendelea kucheza hiyo filamu kutokana na jinsi Frank anavyomghasi.Sasa kwa sababu nilikuwa nimeshaingia naye mkataba nikawa sina jinsi bali kumuondoa Frank ili kazi iendelee.Nikamwambia Frank mimi na wewe tutaendelea kufanya kazi nyingine ila kwa hii hebu tuepushe hii shari kwa sababu huyu msichana ndio kwanza anaanza kazi ya uigizaji.She has to be comfortable.

Nikamuomba Frank arudishe script,akagoma kufanya hivyo na kisha kuanza kunitumia maneno machafu machafu na kwenda kwenye baadhi ya magazeti na mambo kama hayo akisambaza maneno ya uongo.Frank amemjua Wema kupitia kwangu.Mimi ndio nilimtambulisha Frank kwa Wema. Kwa kifupi hicho ndicho kilichotokea.Kimsingi chanzo ni utovu wa nidhamu aliouonyesha Frank na wala si vinginevyo kama ambavyo amekuwa akidai.Nilimualika Frank kwa minajili ya kusaidiana kama vijana lakini naona hizi ndio fadhila.Yote namuachia Mungu,atajua la kufanya.

kanumba1bc.jpg


Steve Kanumba akiwa amepozi na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu​

BC : Hivi sasa unapendelea zaidi kuitwa « Kanumba The Great ». Nini chanzo cha jina hili na kwanini umeamua kujiita hivyo ?

SK : Hizi ni nick name tu za kisanii kama ambavyo wasanii wengi wanajiita. « The Great » ni jina ambalo nimelichukua kutokana na watu mbalimbali katika historia waliokuwa wanajiita « The Great ». Isitoshe kwa hivi sasa,kwa jinsi ambavyo mungu amenisaidia kufikia hapa nilipo, I feel Great.

BC : Je umeoa au una mchumba hivi sasa ?

SK : Sijaoa wala sina mchumba wala girlfriend.

BC : Mwisho ungependa kuwaambia nini washabiki wako ? Unazo project ngapi zinazokuja ? Watarajie nini ndani ya project hizo ?

SK : Kwanza nawapenda sana, kwa sababu wao walinipenda sana tangu mwanzoni na kunipa support tangu mwanzo.Nawasihi waendelee kununua kazi za nyumbani ili kuendeleza fani ya filamu nchini Tanzania. Filamu ambazo hazijatoka kama nilivyozitaja hapo juu ni moto wa kuotea mbali. Wajiandae kupata burudani ya aina yake zikitoka.

BC : Ahsante sana Steve kwa muda wako.Tunakutakia kila la kheri

SK : Ahsanteni na nyie.Mnafanya kazi nzuri sana.
 
Mgeni Wa Wiki


Source:
Mgeni wa wiki « Sundayshomari's Blog

sunday-random-2-868.jpg


Steve Kanumba "The Great" akiwa katika studio za televisheni ya Sauti ya Amerika- VOA.

Mgeni wetu wiki hii ni Steve Kanumba "The Great" alipotembelea VOA Washington Dc. Akiwa kwenye ziara yake maalum ndani ya Voa alifanya mahojiano maalum nami ambayo mtapata nafasi ya kuyasikia katika matangazo yetu siku za karibuni.

Kazi kama wengi mnavyofahamu ni mcheza filam bora 2010 Tanzania prodyuza, Director na pia mwanamuziki. Katika mahojiano yetu amedokezea ujio wa albam yake kwani pia ni mwimbaji kama ulikuwa hujui.

Kanumba alikuwa kwenye matembezi maalum hapa Washington ambapo pia alifanya ziara nyingine huko Los Angeles Carlifornia na New York.

Kila la kheri Kanumba katika kila ufanyalo. Kaa mkao wa kula kusikiliza mahojiano yetu radioni ntawapa taarifa zaidi hivi karibun

 
Back
Top Bottom