Steps kuelekea ndoa

Bukijo

JF-Expert Member
Jul 28, 2010
208
71
Wadau naombeni mnijuze steps zinazofaa unapoanza Mahusiano na mtu ambaye mmekutana katoka mikoa Tofauti,yaani mfano mmoja anatokea Mwanza na Wewe kwenu ni Arusha halafu mmekutana Dar Mkapendana!.Mnaanza upande gani kutambulishana?
Pia ningependa ufafanuzi kidogo juu ya POSA,posa ni nini? Ni vitu gani vinawekwa kwenye posa na ni nani anaruhusiwa kupeleka Posa,maneno gani husemwa wakati wa kutoa posa?.
Ntashukuru kwa maelezo yenu!
Asanteni!
 
:confused2: Ngoja nisubirie wataalamu waje Asprin, Kaizer, Mkeshahoi, NN mko wapi
 
Wadau naombeni mnijuze steps zinazofaa unapoanza Mahusiano na mtu ambaye mmekutana katoka mikoa Tofauti,yaani mfano mmoja anatokea Mwanza na Wewe kwenu ni Arusha halafu mmekutana Dar Mkapendana!.Mnaanza upande gani kutambulishana?
Pia ningependa ufafanuzi kidogo juu ya POSA,posa ni nini? Ni vitu gani vinawekwa kwenye posa na ni nani anaruhusiwa kupeleka Posa,maneno gani husemwa wakati wa kutoa posa?.
Ntashukuru kwa maelezo yenu!
Asanteni!
Mkuu Bukijo,

Unataka kufahamu mambo mengi sana at a time, ambapo kila moja wapo linahitaji details sana!
Lakini taratibu utafahamishwa, japokuwa najiuliza wewe unaishi sehemu gani ya dunia kiasi huelewi kabisa chochote!
 
huko bado sijafikia, hebu mwelezeni nami nipate ujuzi kabisa, isije fika kipindi nami nikauliza, bora jamaa kauliza
 
Yaani wewe unataka kuchumbia na then hujui mila zao? Kila kabila lina mila zake sasa nikikwambia za kwetu Mbulu utaelewa? Au kule kwetu Tarime lazima upeleke na mbegu za bangi ili ukubalike? We cha msingi uliza mila za kwao huyo mchumba wako then utajua nini kinatakiwa kufanyika.
 
Sasa unashangaa nini??!! Si ndiyo maana kaja hapa kuuliza mkuu
 
Wadau naombeni mnijuze steps zinazofaa unapoanza Mahusiano na mtu ambaye mmekutana katoka mikoa Tofauti,yaani mfano mmoja anatokea Mwanza na Wewe kwenu ni Arusha halafu mmekutana Dar Mkapendana!.Mnaanza upande gani kutambulishana?
Pia ningependa ufafanuzi kidogo juu ya POSA,posa ni nini? Ni vitu gani vinawekwa kwenye posa na ni nani anaruhusiwa kupeleka Posa,maneno gani husemwa wakati wa kutoa posa?.
Ntashukuru kwa maelezo yenu!
Asanteni!

nijuavyo kwa wengi wanaanza kujitambulisha upande wa mwanamke, kama wewe ni mwanaume bac inatakiwa uende kwa mwanamke kujitambulisha, ukiambatana na mshenga wako ambae ndio ataenda kujua mambo ya posa yanasemaje kutokana na kabila hucka, posa na mahatri nadhani havina tofauti, posa ni kitu/vitu/pesa/pombe ya kimila/blanketi...nk unayotoa kwa familia ya mwanamke kwa kushukuru wazazi kwa kutunza binti yao vema(kabila langu)....maneno yanayosemwa kwenye posa hayakuhusu wewe, yanahusu wazee au(mshenga) utakaeongozana nae/nao.
 
Ina maana nyie wote wawili hamna ndugu walioko kwenye ndoa? kwa nini msiwapigie simu muwaulize walifanyaje? hii ilikuwa haina sababu ya kuulizwa hapa unless una maana nyingine...
 
Sinamaana tofauti na hiyo ila ugumu wenyewe ni hivi-Ndugu wakaribu upande wangu wameoana kabila moja hivyo hapakua na complication, walisafiri kuelekea mkoa wao wakafunga ndoa bila shida yoyote!
Kwa upande wangu ni hv mimi natokea Kigoma na mchumba wangu anatokea Manyara!.Hivyo tumeshindwa kuelewa tufuate desturi za wapi kwani kwa ufupi zinatofautiana mno!
 
Sinamaana tofauti na hiyo ila ugumu wenyewe ni hivi-Ndugu wakaribu upande wangu wameoana kabila moja hivyo hapakua na complication, walisafiri kuelekea mkoa wao wakafunga ndoa bila shida yoyote!
Kwa upande wangu ni hv mimi natakea Kigoma na mchumba wangu anatokea Manyara!.Hivyo tumeshindwa kuelewa tufuate desturi za wapi kwani kwa ufupi zinatofautiana mno!
Basi hilo ndio lingekuwa swali? lakna ukiuliza general watu hatuelewi unataka nini kumbe mtu unajua hata kutofautisha kuwa mila zenu hazifanani? ushauri anza mila za binti ndo zije zako(ladies first)
 
Yaani wewe unataka kuchumbia na then hujui mila zao? Kila kabila lina mila zake sasa nikikwambia za kwetu Mbulu utaelewa? Au kule kwetu Tarime lazima upeleke na mbegu za bangi ili ukubalike? We cha msingi uliza mila za kwao huyo mchumba wako then utajua nini kinatakiwa kufanyika.

Ni vigumu kufahamu bila kuuliza,Dena Amsi we ndo wakunisaidia kwani yeye nadhani nikabila lako-Mbulu.So plz niaambie huko inakuwaje,utamaduni wenu ukoje inapotokea kabila tofauti na lenu anataka kuoa kwenu!
 
Basi hilo ndio lingekuwa swali? lakna ukiuliza general watu hatuelewi unataka nini kumbe mtu unajua hata kutofautisha kuwa mila zenu hazifanani? ushauri anza mila za binti ndo zije zako(ladies first)
Nashukuru sana,ngoja nianze kutafuta watu wa Huko(Manyara/Arusha) nadhani watanisaidia kwa hili!
 
bwananyie mnaleta complication za ajabu .kwetu sisi wachaga huwa tunamchukua mwamnamke tunamweka ndania asubuhi mzee anaamka na mbuzi anapeleka kwa wakwe ngomo inaishia hapo unakuwa tayari umeshaoa
 
Du!! Mkuu hiyo sidhani kama inawezekana kwangu,Kwani nataka Ndoa ya kanisani!
 
Yeye (mchumba) mwenyewe pia anaweza kukusaidia. akaulizie kwa ndugu jamaa na marafiki watamwelekeza mambo yanakuwaje kwa mila za kabila lao. na pia nadhani inatofautiana kati ya ukoo na ukoo. Mimi kwa mfano husband tunatoka kabila moja lakini mambo ya posa kwa ukoo wetu ni tofauti kidogo na kwao. so, mimi nilimwuliza bibi, akanitajia mtiririko wote, nikaenda kumdesesha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom