ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Science inaishinda religion katika kufanya uchunguzi, religion haina uchunguzi na in fact ukifanya uchunguzi katika conventional religion utaambiwa unafanya blasphemy. Religion, for the most part represent a closed conservative system with some fantastic and dogmatic ideas that are suppose to be taken by fiat.No proofs, no skepticism and no room for questioning authority.
Dini haitaki maswali, lakini inajidai kuwa na majibu karibu yote.
Science on the other hand, encourages the pursuit of knowledge, skepticim, questioning of authority.
Sayansi siyo tu inakubali maswali, inasisitiza uchunguzi na kuuliza maswali na ina maarifa ya kukubali kwamba haina majibu yote.
Labda kwa tafsiri hii ya "science vs Religion" inaweza kutoa upotofu wa moja kwa moja na kuifanya Sayansi ionekane ni zaidi ya Dini.
There is this quote from Albert Einstein ( a scientist):
"After religious teachers accomplish the refining process indicated, they will surely recognize with joy that true religion has been ennobled and made more profound by scientific knowledge."
Kwa tafsiri ninayoipata ni kuwa sayansi ni aina nyingine moja wapo ya dini kwani kiini na chimbuko la dini ni imani katika jambo fulani (hapa tukizungumzia uwepo au kutokuwepo kwa mambo fulani fulani ambayo wengine wanayaamni na wengine hawayaamini). Sayansi nayo kwa staili yake ya weza kuwa ndio dini ya kweli kwa wale wanaoiamini/wafuasi wake.
Sayansi kwa mapana yake ni ina jaribu kuwafanya waamini wa dini fulani waweze kufikiri zaidi katika mambo yanayowazunguka kwa kutumia utashi na pia uchnguzi wa kina, Sio kwamba dini haina uchunguzi wa kama ambavyo sayansi inafanya.
Ukichukua tafsiri ya dini kama "religion" na sio "religions" unaweza kuzuia upeo wa hoja. Kwani kwa mfani ndani ya dini ya Kikristu (Christianity), unaweza kuona wapo wafuasi wa dini wa milengo miwili (conservatives & liberal/traditionalists and progressives ). Kuna wale wanaoamini kuwa maneno katika Biblia ni vile yalivyo tokea mwanzo wa kund ikwa kwake, sasa na hata milele hayawezi kubadilika na kwamba Biblia haina makosa kwa kuwa imeandikwa kwa nguvu za Mungu.
Lakini kwa upande mwingine, wapo wale ambao wana amini uwepo wa Mungu na neno lake kwa kuchochewa pia na utafiti na uchunguzi wa kisayansi na ndio hao wanaoleta mapinduzi katika dini kwa kuamini kuwa hata maandiko ya Mungu walihusisha binadamu ambao kimsingi yangeweza kuwa na upotofu kulingana na mwandishi na mazingira ya wakati (historia, jiografia, sayansi) na kadhalika.
Kwa suala la uchunguzi pia, ukichukulia dini kwa mapana yake, unaweza kuona pia kuwa chimbuko la sayansi ni dini ambapo sayansi inaweza kutofautisha yale ambayo yanawezekana na yasiyowezekana kwa hitimisho la kidunia zaidi kwa kusema yapo nje ya uwezo wa mwanadamu (beyond/human being or universe) kwa mfano kuweza kuumba mtu na kumfanya aishi.
Lakini kwa upande mwingine, aina hiyo hiyo kushindwa kwa uchunguzi/ utafiti wa kujua ukweli katika dini kama ilivyo kwenye sayansi kunaweza kupelekea ya hitimisho kwa wafuasi wake hususan kwa yale wasiyoweza kwa kwa akili zao wenyewe na kusema hayo ni ya "Mungu".
Wanasayansi wanashindwa kusema/kutaja "very specific" ni nani anaweza kufanya yale yasiyowezekana na binadamu wa kawaida ili hali wafuasi wa dini wao wanaona kuwa hayo wasiyoyaweza yapo hivyo kutokana na kuwa kwenye mamlaka ya mtu mwingine mwenye uwezo zaidi yao na ambaye hawawezi kumuona kwa macho na akili zao (Mungu).