Stendi ya daladala eneo hili itolewe?

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
attachment.php

Hili ni eneo la Nzovwe Mbeya (Njiapanda ya Itende) ambayo imekuwa kero kwa kutokea ajali za mara kwa mara na kuua watu kadhaa kwa kugongwa na magari. Kama picha inavyoonekana mbele ni mteremko halafu kuna mto Nzovwe na kisha mwinuko hadi stendi ya Iyunga. Mara nyingi magari hupita kwa kasi sana eneo hili la mteremko ili kupanda mlima unaofuata. Wakati huohuo kama unavyoona upande wa kushoto kuna stendi na upande wa kulia kuna stendi na wakati huo stendi ya upande wa kulia ni barabara inayoelekea huko Itende na Kalobe.

Kwa maoni yangu labda stendi katika eneo hili itolewe kabisa au la sivyo yawekwe matuta ili kupunguza mwendo.
 

Attachments

  • Image025.jpg
    Image025.jpg
    102.6 KB · Views: 166
Umenipelekea kukumbuka maeneo hayo nilipokuwa naelekea Mlowo, hapo ni karibu na Iwambe duuu..............Mbeya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom