Stella Manyanya amkaba koo Dr Slaa

Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,768
3,232
Stella Manyanya atema cheche Bungeni akimtuhumu Dr Slaa kwa kuwafundisha wananchi wasifanye kazi wakati yeye amewahamasisha wananchi wa kijiji chake (hakukitaja) wajitolee kufanya kazi za maendeleo, anasema ameudhiwa sana na kauli ya Dr Slaa kuwaambia wananchi wakisikia harufu ya chakula kizuri basi kinakuwa kimepikwa kwa mbunge.

Pia amemuonya anayeitwa Mchumba wa Dr Slaa kwa kumuandikia SMS za kumtukana, anasema eti alifuatilia hizo SMS akakuta zimetoka kwa Josephine Emmanuel.

Najiuliza hivi wabunge wa CCM hawana mambo ya kuchangia zaidi yakuingiza personalities?
 
leo ktk kikao cha bunge mbunge wa viti maalum amesema Dr. Slaa anaongea maneno ya uchonganishi na kuhimiza watu wasifanye kazi kuwa hafai kuwa rais pia akamwonya mchumba wa Dr. Slaa, Josephine aache kumtumia meseji chafu na matusi. Anasema alifanyia uchunguzi wa hiyo namba na kungudua mwenye namba ni Josephine Emmanuel mchumba wa Dr. Slaa
Source: TBC toka Bungeni
 
Oya hapo kwenye nyekundu atakuwa amekosea hivi kwani Josephine ameshamalizana na mumewe?
 
Nikiwa makini kabisa kuendelea kusikiliza mjadala wa bunge,Inginia Stella Manyanya amemtolea kashfa Dr pamoja na mkewe Josephine,adai Dr alienda kijijini kwake na kuwatangazia wananchi wake wasifanye kazi na kama pilau ikipikwa ote waende kwake.Amtuhumu pia mke wa Dr [Josephine] kuwa anamtumia ujumbe wa kukashifu kwa njia ya mtandao;akiwa ameshangiliwa na kupigiwa meza,Manyanya aongeza kuwa Dr Slaa hafai kuwa rais
My take;Kauli ya Manyanya sidhani kama inaukweli wowote zaidi ya kumchafua Dr na familia yake
 
Slaa naye kazidi! na hako kamchumba kake naona kanataka kujitafutia umaarufu!
 
Stella got it wrong on Slaa kuhamasisha wananchi wasifanye kazi, sijawahi sikia huu upuuzi, lakini suala la sms naomba tusianze kurusha mawe, slaa is a member of JF, so he can as well clarify kuhusu sms kutoka kwa josephine...
 
Stella Manyanya atema cheche Bungeni akimtuhumu Dr Slaa kwa kuwafundisha wananchi wasifanye kazi wakati yeye amewahamasisha wananchi wa kijiji chake (hakukitaja) wajitolee kufanya kazi za maendeleo anasema ameudhiwa sana na kauli ya Dr Slaa kuwaambia wananchi wakisikia halufu ya chakula kizuri basi kinakuwa kimepikwa kwa mbunge,pia amemuonya anayeitwa Mchumba wa Dr Slaa kwa kumuandikia SMS za kumtukana,anasema eti alifuatilia hizo SMS akakuta zimetoka kwa Josephine Emmanuel Najiuliza hivi wabunge wa CCM hawana mambo ya kuchangia zaidi yakuingiza personalities
Si aende polisi na ushaidi anao anasubiri nini...! kuhusu slaa a2elewe ni wapi na ni lini slaa alihamasisha huo upuuzi... si kuanza kuropoka kama yupo saloon...
 
Stella got it wrong on Slaa kuhamasisha wananchi wasifanye kazi, sijawahi sikia huu upuuzi, lakini suala la sms naomba tusianze kurusha mawe, slaa is a member of JF, so he can as well clarify kuhusu sms kutoka kwa josephine...

Kama nimekuelewa vizuri unataka Dr. Slaa amsemee mchumba wake?? assuming ni kweli Josephine alituma hizo sms, je ni lazima Dr. Slaa atakuwa aliziona ama unataka kusema ndiye alimtuma??

Hebu kuwa serious kidogo mkuu.
 
bunge la mwaka huu, hivi wanajadili bajeti au sms kutoka kwa josephine, nachoka mwenzenu sijui yatakwisha lini haya.
 
Stella Manyanya atema cheche Bungeni akimtuhumu Dr Slaa kwa kuwafundisha wananchi wasifanye kazi wakati yeye amewahamasisha wananchi wa kijiji chake (hakukitaja) wajitolee kufanya kazi za maendeleo anasema ameudhiwa sana na kauli ya Dr Slaa kuwaambia wananchi wakisikia halufu ya chakula kizuri basi kinakuwa kimepikwa kwa mbunge,pia amemuonya anayeitwa Mchumba wa Dr Slaa kwa kumuandikia SMS za kumtukana,anasema eti alifuatilia hizo SMS akakuta zimetoka kwa Josephine Emmanuel
Najiuliza hivi wabunge wa CCM hawana mambo ya kuchangia zaidi yakuingiza personalities

Wavua magamba watasema haka kamama kanatafuta umaarufu kwa mgongo wa Dr.Slaa
 
huyu si ndiyo yule engineer mwanasiasa - au njaa ndiyo zinawapeleka huko? yaani unaitupa carrier yako ya ufundi unaingia kupiga majungu.
 
Shule za kudesa ni hatari sana!!!! Kama bi. Josephine anamuandikia sms kwa nini asimchukulie hatua za kisheria? Anasema hayo mambo bungeni ili iweje? Je hana mambo mengine yanayosumbua wananchi mpaka anachangia mambo ya kipuuzi kiasi hicho? Yes wabunge wengine inapaswa viti vyao ving'olewe bungeni kabisa!!!!!
 
Engeneer na politics wapi na wapi!! Inabidi akacheze na spana huyu mama.
 
Simple minds talk about people and their personality while strong minds discuss issues and visualize the future
Mwenye cv na academic competence ya huyu mama aijaze hapa
 
GreatThinkers,

Inaonekana Stella Manyanya hakumuelewa Dr Slaa, nashukuru sana wananchi wamemuelewa Dr Slaa.

Tunasumbuliwa na vilaza, wananchi wameamka sana saivi, kama unataka wachangie elimu au zahanati ni lazima mjenge majengo ya kudumu si haya miaka miwili yanabomoka.

Haiwezekani Mwananchi atoke jasho udai nguvu ya mwananchi kujitolea halafu wewe ukienda hata kuwatembea tu unataka ulipwe posho.

Wezi wanajifanya hawakuewi, Wananchi Wanakuelewa.

Dr Slaa Go, keep Moving.
 
Sio bure Stella Manyanya na Josephine kuna kitu!! Ilikuaje mpaka wakawa wanatukanana kwenye sms? Sisi wote ni watu wazima tafakari
 
Stella Manyanya atema cheche Bungeni akimtuhumu Dr Slaa kwa kuwafundisha wananchi wasifanye kazi wakati yeye amewahamasisha wananchi wa kijiji chake (hakukitaja) wajitolee kufanya kazi za maendeleo anasema ameudhiwa sana na kauli ya Dr Slaa kuwaambia wananchi wakisikia halufu ya chakula kizuri basi kinakuwa kimepikwa kwa mbunge,pia amemuonya anayeitwa Mchumba wa Dr Slaa kwa kumuandikia SMS za kumtukana,anasema eti alifuatilia hizo SMS akakuta zimetoka kwa Josephine Emmanuel
Najiuliza hivi wabunge wa CCM hawana mambo ya kuchangia zaidi yakuingiza personalities

Huyu injinia amechoka kiakili siku hizi yani hadi anajiaibisha mno.

Kwani wananchi wa kijiji cha Slaa wao si wananchi?? yani huyu mama amekuwa bogus sana kadri anavyozidi kukaa bungeni. Bila shaka hizo habari za Slaa kuhamasisha wananchi wasifanye kazi atakuwa amezipata kwenye saluni za wabunge wa ccm!!

Hii tabia ya wabunge mainjinia kuongea pumba bungeni naona inazidi kuota mizizi. Juzi mwalimu wangu Eng. Dr. Mahenge nae alimwaga upupu bungeni kama mtu asiyekwenda shule. Alianza kwa kuwaponda wapinzani eti wanapita kwenye barabara zilizojengwa na serikali ya awamu ya nne halafu wanasema serikali hiyo haijafanya kitu. Lakini kama kawaida ya wanamagamba nae alipoanza kuchangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu akageuka kuililia serikali imsaidie ujenzi wa barabara za wilayani kwake kwakuwa hazipitiki, kwamba halmashauri ya wilaya ya makete haina uwezo wa kifedha kuzikarabati.

Hivi kwanini hawa wasomi wetu wakiingia tu ccm wanakuwa wapuuzi kiasi hiki? utashangaa baadhi ya watu wasiokuwa na elimu kubwa sana ndio wanakuwa angalau na uwezo wa kujenga hoja na kuzungumza mambo ya maana kidogo kuliko hawa wasomi.

Shame on you Eng. Manyanya and Eng. Dr. Mahenge!!
 
Back
Top Bottom