Startv tanzania live online

STARTV ADA ESTATE, DSM
30/08/2012

Ndugu Wapenzi wa Star Tv, tunaomba mtuwie radhi kwa kupotea hewani kwa masaa kadhaa.

Bado tuko kwenye majaribio, hivyo tunatatua hitilafu mbalimbali tunazokumbana nazo huku tukijitahidi kufanikisha dhamira yetu ya kurusha matangazo ya kudumu moja kwa moja kupitia mtandaoni.

Kunradhi kwa kupotea kwetu na shukrani kwa kutuunga mkono kuangalia matangazo haya.

Ndugu Watazamaji, La ziada ni kwamba; kwa majaribio haya, tunarusha picha za TV kwa quality ya chini ili kufanya tathmini mbalimbali. Tutaongeza quality mara tu baada ya kubainisha.

Ahsanteni.
Steve,
Tech.

source: Radio Free Africa Tanzania*|* STARTV LIVE
 
STARTV:NAWAPONGEZENI SANA KWA VIPINDI VYENU VIZURI SANA NA MPO KITAIFA(KUSIMAMIA MASLAHI YA NCHI HII) ZAIDI PIA HAMNA UBAGUZI WA KIITIKADI.MUNGU IBARIKI STARTV,KISSFM NA RFA MTANGAZE HABARI BILA WOGA KWA SABABU MKIFICHA UGONJWA KIFO KITATUUMBUA.NAPENDA SANA KIPINDI CHA 'TUONGEE ASUBUHI,BBC-SWAHILI na kila kipindi.AHSANTE SANA STAR TV.
 
nawashukuru sana kwa kuw ahewani
hata sisi wa madongo kuinama tunawapata vema
rekebisheni zaidi picha ikiwezekana tumieni ustreem kama wenzenu wa kenya
CITIZEN TV LIVE | KenyaMOJA.com.
big up na ni hatua nzuri na mfano wa kuigwa kwa Tanzania
 
Kabla sijaanza kuchungulia huko ninaomba mnitoe ushamba kidogo.Hivi nikiangalia TV online itakuwa Inakula ki-Bundle changu kwa kiasi gani? Ninahitaji kuwa na Bundle ya kiasi gani ili kufaidi matangazo ya TV Online ama inakuwa ni dezo bin free?
 
Aisee swafi sana sasa nikiwa JOIB ntapata taarifa ya habari na ile siku ya Alhamis pale saa nne kamili mpaka saa saba, ile miziki yetu ya zamamni ntaifaudu mnooooo kupitia radio RFA
 
Kabla sijaanza kuchungulia huko ninaomba mnitoe ushamba kidogo.Hivi nikiangalia TV online itakuwa Inakula ki-Bundle changu kwa kiasi gani? Ninahitaji kuwa na Bundle ya kiasi gani ili kufaidi matangazo ya TV Online ama inakuwa ni dezo bin free?

Jibu lake ni muhimu kwa watu wengi siyo wewe peke yako.
 
Kabla sijaanza kuchungulia huko ninaomba mnitoe ushamba kidogo.Hivi nikiangalia TV online itakuwa Inakula ki-Bundle changu kwa kiasi gani? Ninahitaji kuwa na Bundle ya kiasi gani ili kufaidi matangazo ya TV Online ama inakuwa ni dezo bin free?
Sijafanikiwa kuitizama kwani nipo kwa mobile...

Kwa mujibu wa mdau hapo juu amesema wameshusha upora wapicha ina maana hata ukiwa na package ya 50Mb na speed yake ikawa ya 150kBps unaweza kutizama kwa mda wa dakika 3 (haya ni makisio yangu tu) hivi bado kuna watu mnatumia internet ya kupimiwa?
 
Dr. A.M. Diallo (Chair & CEO, RFA) says: August 26, 2012 at 9:37 am

Napenda kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu za kufikisha matangazo yetu mahali pote hapa duniani kupitia masafa ya FM, AM (MW), na Internet (Mtandao), kwa njia iliyo bora zaidi.

Tunajitahidi tuwezavyo kuondoa dosari na changamoto zinazojitokeza, za kiufundi na kiteknolojia. Kwa wasilizaji wetu walio nje ya Tanzania, hivi karibuni tutaweka fomu ya kuwawezesha kutuma salamu au ujumbe kwa ndugu na marafiki walio mbali na nyinyi.

Salamu au ujumbe utasomwa hewani ili uwafikie wahusika; kwa hiyo tutaomba mtumie majina yanayojulikana kwa ndugu na marafiki zenu ili tuweze kuwaunganisha hususani wale ndugu/marafiki wasiofikika kwa simu, barua-pepe na njia nyingine za mawasiliano isipokuwa redio.

Nawatakieni usikilizaji mzuri na karibuni kwa ushauri, maoni kuhusu vipindi vyetu.

Anthony
Source: Radio Free Africa Tanzania*|* RFA Live
 
Kabla sijaanza kuchungulia huko ninaomba mnitoe ushamba kidogo.Hivi nikiangalia TV online itakuwa Inakula ki-Bundle changu kwa kiasi gani? Ninahitaji kuwa na Bundle ya kiasi gani ili kufaidi matangazo ya TV Online ama inakuwa ni dezo bin free?

Kwa internet ya kupimiwa bongo, nadhani inaweza kuwa expensive sana. Kwa sisi ambao internet hatupiwi na speed ni ya ajabu huku nje ni burudani tu!
 
STARTV:NAWAPONGEZENI SANA KWA VIPINDI VYENU VIZURI SANA NA MPO KITAIFA(KUSIMAMIA MASLAHI YA NCHI HII) ZAIDI PIA HAMNA UBAGUZI WA KIITIKADI.MUNGU IBARIKI STARTV,KISSFM NA RFA MTANGAZE HABARI BILA WOGA KWA SABABU MKIFICHA UGONJWA KIFO KITATUUMBUA.NAPENDA SANA KIPINDI CHA 'TUONGEE ASUBUHI,BBC-SWAHILI na kila kipindi.AHSANTE SANA STAR TV.

Nawapongeza pia ila kwa kuwa wameamua kutuuzia kingamuzi chao cha Continental kwa ghafla na kwa lazima, sisi tusio na fedha kwa sasa tutavikosa vipindi vyao. Sijaona shida kama wangekaa kwa muda startimes na kutahadharisha kwenye TV yao kuwa baada ya muda wataondoka. Badala yake waliondoa test sign kuonyesha kuwa wamekuja ki-ukweli kushangaa kuwa hatutaviona vipindi vyao kwa sasa. Well ni kuangalia priorities, kununua kingamuzi kwa sasa au kununua chakula cha familia, nitaamua baadaye. Mkae salama maana vipindi vyenu kwa muda huu. Alamsiki
 
Radio Free Africa Tanzania*|* STARTV LIVE STARTV LIVE ONLINE

RADIO FREE AFRICA TANZANIA IPO LIVE ONLINE KTK LINKI HAPO JUU, JE WEWE MWANA- JAMIIFORUMS POPOTE ULIPO DUNIANI UNAIPATA?

HABARI HII NZURI IMEPATIKANA KWA HISANI YA TOVUTI YA WAVUTI 01/SEPT/2012
SOURCE - WWW.WAVUTI.COM

Habari za asubuhi,
Mwanajf yoyote anayeweza kujua kama star tv wanapatikana online tafadhali anisaidie link.Niko nje ya Tz na ningependa kupata japo habari kutoka nyumbani. Nimejaribu link hapo juu lakini haijaweza kufungua.

badala yake inanipa majibu haya...

[h=1]This account has been suspended[/h]If you manage this site and have a question about why the site is not available, please contact NetFirms directly.

thanks!
 
Habari za asubuhi,
Mwanajf yoyote anayeweza kujua kama star tv wanapatikana online tafadhali anisaidie link.Niko nje ya Tz na ningependa kupata japo habari kutoka nyumbani. Nimejaribu link hapo juu lakini haijaweza kufungua.

badala yake inanipa majibu haya...

This account has been suspended

If you manage this site and have a question about why the site is not available, please contact NetFirms directly.

thanks!
Kwa muda kama wa wiki moja hii website inatoa ujumbe huo huo wa "This account has been suspended"
 
STARTV ADA ESTATE, DSM
30/08/2012

Ndugu Wapenzi wa Star Tv, tunaomba mtuwie radhi kwa kupotea hewani kwa masaa kadhaa.

Bado tuko kwenye majaribio, hivyo tunatatua hitilafu mbalimbali tunazokumbana nazo huku tukijitahidi kufanikisha dhamira yetu ya kurusha matangazo ya kudumu moja kwa moja kupitia mtandaoni.

Kunradhi kwa kupotea kwetu na shukrani kwa kutuunga mkono kuangalia matangazo haya.

Ndugu Watazamaji, La ziada ni kwamba; kwa majaribio haya, tunarusha picha za TV kwa quality ya chini ili kufanya tathmini mbalimbali. Tutaongeza quality mara tu baada ya kubainisha.

Ahsanteni.
Steve,
Tech.

source: Radio Free Africa Tanzania*|* STARTV LIVE

[h=1]This site is temporarily unavailable[/h] If you manage this site and have a question about why the site is not available, please contact NetFirms directly.
 
STARTV ADA ESTATE, DSM
30/08/2012

Ndugu Wapenzi wa Star Tv, tunaomba mtuwie radhi kwa kupotea hewani kwa masaa kadhaa.

Bado tuko kwenye majaribio, hivyo tunatatua hitilafu mbalimbali tunazokumbana nazo huku tukijitahidi kufanikisha dhamira yetu ya kurusha matangazo ya kudumu moja kwa moja kupitia mtandaoni.

Kunradhi kwa kupotea kwetu na shukrani kwa kutuunga mkono kuangalia matangazo haya.

Ndugu Watazamaji, La ziada ni kwamba; kwa majaribio haya, tunarusha picha za TV kwa quality ya chini ili kufanya tathmini mbalimbali. Tutaongeza quality mara tu baada ya kubainisha.

Ahsanteni.
Steve,
Tech.

source: Radio Free Africa Tanzania*|* STARTV LIVE

Hii post mlitoa tar 30/08/2012. Lakin leo may 12, 2015, nilijaribu ku-watch start tv online bado quality ni ndogo sana mtaongeza lini.
 
Back
Top Bottom