STARTV mbona mna upendeleo hivyo?

Benmpo

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
450
424
Nimekuwa nikifuatilia uchambuzi wa Magezeti kila siku asubuhi katika kituo cha televisheni cha STARTV.
Jambo moja ambalo limekuwa likinisikitisha ni kwamba inapokuja kwenye MAONI YA MHARIRI, mara nyingi wamekuwa wakisoma yanayotoka kwenye Gazeti moja tu la UHURU.

Hapa nimekuwa nikijiuliza, hivi maoni ya wahariri wengine hayana vigezo vya kuyafanya kusomwa kusomwa kwa undani? Je Topic zao hazina maslahi mapana kwa taifa? Je hayo ni matakwa ya mtangazaji mwenyewe au ni sera ya chombo husika?

Najua kuna watu watasema, kama nataka kujua kiundani basi ninunue gazeti nisome mwenyewe. Napenda watambue kuwa bila kuwepo kwa watazamaji, wasikilizaji au wasomaji vyombo hivi visingekuwepo. Na pia lazima watambue kuwa kuna sehemu magazeti hayafiki kabisa hivyo mtu akishataza au kusikiliza uchambuzi kwenye vyombo vya habari ndio imetoka.

Tambueni kuwa watazamaji wenu ni wengi, wenye interests tofauti. Ni vema mkanonesha ukomavu katika tasnia hiyo kwa kuweka mazingira sawa kwa wote bila kuangalia mhariri anatoka katika chombo gani (kwa maana ya Gazeti).

MADA AMBAZO ZINA MASLAHI MAPANA ZIPEWE NAFASI REGARDLESS ZINATOKA UHURU, TD, MWANANCHI, MAJIRA, MTANZANIA N.K
 
Yaani unapoteza muda wako na hyo TV? Hahahahahaha hyo umaarufu ulishaisha unebakia kwenye Tamthilia tuu za wafilipino, njoo TV 1 , Hao walijipotezea umaarufu wakati wa uchaguzi waliji egemeza zaidi katika chama Fulani.

Mambo yapo TV 1,
 
Back
Top Bottom