StarTV Live: Mjadala Bungeni Kielelezo cha kukomaa Demokrasia?

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
hii mada iko live StarTV.

Studio Mwanza: Yahya
Mgeni Mwanza: Jimmy

Studio Dodoma: Faraji Charles
Wageni Dodoma: Job Ndugai, Tundu Lisu, Moses Machali

Karibuni
 
Jimmy hajaelewa ule utafiti ulilenga kitu gani, lengo la utafiti ule ilikua kuangalia uwezo wa viongozi kusimamia mijadala bungeni, ndio maana ulilenga kwa spika, naibu wa spika na wenyeviti.

Mjadala bungeni sio kielelezo cha kukomaa demokrasia, kanuni zilizopo spika anao uwezo wa kulazimisha nini kijadiliwe na nini kisijadiliwe, Pia spika anao uwezo wa kuamua nani ampe nafasi na nani amnyime nafasi.

Wabunge pia wamekua wakijadili kwa maslahi ya chama, ni mpaka maslahi ya umma yatapoanza kuwekwa mbele kabla ya maslahi ya chama tunaweza kusema demokrasia inakomaa
 
Bunge letu sasa hivi limekuwa kama tamthilia mijadala mingi imejikita katika ushabiki mkubwa wa kisiasa sio kwa maslahi ya Taifa, nalikumbuka bunge la mwaka 2010 chini ya spika Sitta, bunge likuwa na changamoto nyingi wabunge walikuwa wanachangia kwa hoja, ili bunge la sasa limekuwa bunge la muongozo spika...unashangaa mtu kama Tundu Lissu anasimama na kutumia data za magazeti ya udaku kama reference.
 
Jimmy hayaelewa ule utafiti ulilenga kitu gani, lengo la utafiti ule ilikua kuangalia uwezo viongozi kusimamia mijadala bungeni, ndio maana ulilenga kwa spika, naibu wa spika na wenyeviti.

Mjadala bungeni sio kielelezo cha kukomaa demokrasia, kanuni zilizopo spika anao uwezo wa kulazimisha nini kijadiliwe na nini kisijadiliwe, Pia spika anao uwezo wa kuamua nani ampe nafasi na nani amnyime nafasi.

Wabunge pia wamekua wakijadili kwa maslahi ya chama, ni mpaka maslahi ya umma yatapoanza kuwekwa mbele kabla ya maslahi ya chama tunaweza kusema demokrasia inakomaa

Jimmy yuko sawa mkuu
Mimi naongozea kuhoji; Hiyo Citizen Parliamentary Watch ni nini na imefanya survey lini, wapi, sample ipi, methodology gani na kwa nini? Significance ya survey nini?????

1. Nini lilikuwa lengo la utafiti huo???
2. Vigezo gani walitumia as ni tofauti from day to day na mijadala husika
3. Kama tunatumia mijadala ya bunge kama kipimo cha kukua kwa demokrasia hili si sawa as tumeona hawa wawakilishi kwa sasa wako kichama zaidi kuliko maslahi ya wapiga kura......mfano angalia miongozo yao ni kama wanataka kukomoana mimi najiuliza hii miongozo na utaratibu ina tija gani kwa matatizo kama maji, umeme, na barabara

Je mnadhani kama bunge ni kipimo cha demokrasia sisi kama wananchi wengi hatupendi jinsi mijadala inavyokwenda kwa sasa......do we have any option to intervene immediately hata kama tunaona hakuna tija????? Is this democracy we are aiming to see its growth and development????
 
Job Ndugai kwa kiasi kikubwa analimudu Bunge.
Haoneshi upendeleo wa chama.
Yule mwenyekiti Mabumba hayuko fair kabisa.
Alafu hawa wabunge wanaokomaa na miongozo, taarifa wanatu'bore sana hasa Mnyika, Lisu wanatuondelea utamu wa Bunge.
Makinda apunguze hasira ndiyo tatizo lake.
 
Bunge la sasa hivi limekuwa dhaifu kutoka na uongozi wa bunge kuwa dhaifu..wanaegemea sana chama tawala..limekuwa bunge la vijembe..binafsi namkubali Tundu Lissu kwa sababu anaongea facts..Ndungai kubali kiti chenu kimepwaya tofauti na bunge la kipindi cha mh. Sita.
 
swali kwa Ndugai:
kwa nini ulimwita mbunge wetu kituko? Ina maana na sisi tuliomchagua ni kituko? Nampongeza Lissu na Machali kwa uvumilivu
 
Bunge letu sasa hivi limekuwa kama tamthilia mijadala mingi imejikita katika ushabiki mkubwa wa kisiasa sio kwa maslahi ya Taifa, nalikumbuka bunge la mwaka 2010 chini ya spika Sitta, bunge likuwa na changamoto nyingi wabunge walikuwa wanachangia kwa hoja, ili bunge la sasa limekuwa bunge la muongozo spika...unashangaa mtu kama Tundu Lissu anasimama na kutumia data za magazeti ya udaku kama reference.

nashukuru kwa kukumbuka uwezo mkubwa wa Mh.Sita sasa umeonyesha kuwa huyu mama anayeongoza bunge pamoja na Jenister Mhagama hawana lolote wako dhaifu sana ktk kuliongoza bunge hili, bora Ndugai kwa kiasi flan kuliko hawa akina mama wawili. Wewe una ushabiki wa ukada kwa kuwa yale wanayoyaongea akina Mwigulu, komba, na wengine unawaacha ila umemwona Tundu lissu, acha ukada na majungu hayatakusaidia kitu.
 
Hiyo Combination ya aawageni waalikwa hapo Dodoma nimeipenda hebu nisikilize ntapata cha kuchangia muda unavyozidi kwenda
 
Kwanza nioneshe masikitiko yangu makubwa jinsi viongozi wetu wa bunge wanavyoliendesha kidikteta, au labda kwa kutojua kanuni kwa ufasaha. Upendeleo wa wazi kwa chama tawala, huko ni kukiuka misingi ya demokrasia. Kuna suala la kura za ndiyo au siyo kwa kutamka kwa mdomo. Hili nalo ni kichekesho kwa bunge la kisasa, linalokaa ndani ya ukumbi wa kisasa kama ule. Mara nyingine wanaosema 'siyo' sauti zao husikika zaidi lakini spika hufukia na kufunika kombe mwanaharamu apite. Imefika wakati sasa kura zipigwe kwa siri kisha zihesabiwe kama ulivyo uchaguzi wa kawaida. Mwisho ni suala la kukatika umeme bungeni, hiyo ni aibu kubwa. Tatizo ni nini? Hakuna wataalamu, hujuma, au uzembe? Kwa ujumla utawala wa bunge hili ni ovyo kabisa, tofauti na jinsi Samuel Sitta alivyokuwa akilimudu wakati ule.
 
Bunge la sasa hivi limekuwa dhaifu kutoka na uongozi wa bunge kuwa dhaifu..wanaegemea sana chama tawala..limekuwa bunge la vijembe..binafsi namkubali Tundu Lissu kwa sababu anaongea facts..Ndungai kubali kiti chenu kimepwaya tofauti na bunge la kipindi cha mh. Sita.

Tena useme dhaifu tu sema Hafifu sanaaaa!
 
nashukuru kwa kukumbuka uwezo mkubwa wa Mh.Sita sasa umeonyesha kuwa huyu mama anayeongoza bunge pamoja na Jenister Mhagama hawana lolote wako dhaifu sana ktk kuliongoza bunge hili, bora Ndugai kwa kiasi flan kuliko hawa akina mama wawili. Wewe una ushabiki wa ukada kwa kuwa yale wanayoyaongea akina Mwigulu, komba, na wengine unawaacha ila umemwona Tundu lissu, acha ukada na majungu hayatakusaidia kitu.

KISAKA MORIS,
Kweli mapenzi yamekufanya mpaka uoni ukweli Tundu Lissu kutoa ushahidi kupitia magazetu yetu wewe unaona ni sahihi...labda nikuulize gazeti gani Tanzania linaaminika kwa Watanzana? Kila gazeti lina upande wake.
 
Last edited by a moderator:
Hili ni eneo lako Yahya, hebu tusaidie Mwanahalisi ni tabloid? au sijamsikia vizuri naibu wa spika?
 
Ndungai anambana Lissu kuhusu kutumia gazeti kama ushahidi bungeni.
 
Demokrasia inaminywa sana na hawa wabunge wanaotetea maslahi ya chama (ccm) kwa mfano walipomnyima mnyika kutoa sababu za kumkashfu mh rais wa jmt wangemuacha aeleze pengine asingetolewa nje ata hivyo nataka kumuuliza ndugai komba alivyosema cdm ni vichaa na hakuchukuliwa hatua yeyote kwa maana hiyo ni kweli kwamba cdm ni vichaa? ndugai atuthibitishie hilo
 
Ndugai mwache kamanda Lissu aongee muda wako ukifika utaongea kumbuka haupo bungeni hapo.
 
Back
Top Bottom