StarTV Live: Mifuko ya hifadi ya jamii

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,638
68,576
Je hoja itapelekwa november au February? Hipi kauli tuichukue ya makongoro au masele?
wageni dsm:marcus na mnyika
 
warudishe haraka fao la kujitoa, waache kucheza na sisi. sio pesa zao, na HATUTAKI KUWAKOPESHA, kwani ni lazima???
 
warudishe haraka fao la kujitoa, waache kucheza na sisi. sio pesa zao, na HATUTAKI KUWAKOPESHA, kwani ni lazima???

Serikali inajichanganya waziri wa kazi amesema wataipeleka hoja February 2013, PIA kuna kipindi masele minister alishanukuliwa akisema kwamba wataileta nov 2012, hapo ndio mnyika anakomaa lazima isomwe nov kama walivyoahidi
 
Anasema tafasiri iliyopo kwenye KATIBA kuhusiana na hifadhi ya jamii ni ndogo sana na pia haiweki hifadhi hii Kama ni kitu cha lazima kwa mtanzania. Anawaomba watanzania waliongelee hili katika utoaji ww maoni ktk KATIBA mpya. Vile vile karudi a kauli yake kuwa udhaifu ww Bunge na WABUNGE kiujumla ndio inalifikisha Taifa hapa tulipo.
 
Mkuu acha haraka, elezea tuelewe basi , mara StarTV, oooohh Makongoro mara wageni DSM etc tunashindwa kukupata

Mh Mnyika anajaribu kuelezea umma kuwa serikali inajikanganya na kauli za watendaji wake, Mfano Naibu waziri wa kazi Makongoro Mahanga anasema marekebisho yataletwa mwezi wa pili, Wakati huohuo Naibu waziri Nishati na Madini Mh Masele anasema wataleta muswada wa madiliko mwezi Novemba.

Masele katimuliwa na Wafanyakazi wa migodini wanataka kujua hatima ya pesa zao karudi mbio kuja kutangaza muswada utaletwa mwezi novemba.

Huku si ndio kukurupuka kwa serikali ya magamba!

HAbari nilizo nazo ni kuwa wafanyakazi wa migodi ya Dhahabu watakua na kikao na kamati ya muheshimiwa Jenister Muhagama, jumatatu ya wiki ijao, jamaa hawataki kusikia chochote zaidi ya fao lao kurudishwa, swali ni hili, hivi wafanyakzi wa sekta zingine vipi? au tumeridhika na hiyo sheria?
 
Aisee sectors nyingine wamelala usingizi mzito sana labda watazinduka endapo marekebisho yasipofanyika November.
 
Hizi fedha wanampango nazo 2015 tunajua kila kitu! kinachotakiwa ni action plana kama vyama vya wafanyakazi vinaweza kutusaidia vipi twende mahakamani waache kula michango yetu bure, sijaona kauli yao nzito yenye maana!
 
Wafanyakazi wa sekta zingine wamefunga ndoa "Katoliki" na waajiri wao hawana cha kujitoa wakati wa utumishi wao kwa mujibu wa sheria au mpaka kifo kitakapowatenganisha.
 
warudishe haraka fao la kujitoa, waache kucheza na sisi. sio pesa zao, na HATUTAKI KUWAKOPESHA, kwani ni lazima???

Serikali haina fedha za kujiendesha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, sasa wameamua kukopa toka katika mifuko ya hifadhi ya jamii na wameshindwa kulipa. Wamekopa NSSF, PPF, PSPF na LAPF mabilioni ya fedha ambayo wameshindwa kuyalipa.

Kwahiyo njia pekee ya kujinusuru na aibu hiyo wakaona ni kwa kusitisha fao la kujitoa ili wajipange, kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo kwetu sisi wanachama wa hiyo mifuko ya pensheni.
 
Hizi fedha wanampango nazo 2015 tunajua kila kitu! kinachotakiwa ni action plana kama vyama vya wafanyakazi vinaweza kutusaidia vipi twende mahakamani waache kula michango yetu bure, sijaona kauli yao nzito yenye maana!

Mkuu, kama unampango wa kuvisubiri vyama vya wafanyakazi a. k. a Trade Union, naomba nikupe pole sana, utasubiri sana hadi jua lichwe, hao ndio chanzo cha haya matatizo na sheria hiyo, walipewa mlungula wa sigh na wao sheria hiyo, mi sina imani nao hata kidogo!
 
Serikali haina fedha za kujiendesha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, sasa wameamua kukopa toka katika mifuko ya hifadhi ya jamii na wameshindwa kulipa. Wamekopa NSSF, PPF, PSPF na LAPF mabilioni ya fedha ambayo wameshindwa kuyalipa.

Kwahiyo njia pekee ya kujinusuru na aibu hiyo wakaona ni kwa kusitisha fao la kujitoa ili wajipange, kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo kwetu sisi wanachama wa hiyo mifuko ya pensheni.

Serikali mufirisi, wafanyakazi tuamke tukiamua tuaweza tusimuachie mnyika peka yake
 
wamenikata maini kabisa hawa jamaa, mbona wanapiga danadana?
au wanataka tusahau.

wafanyakazi naomba tuungane tulianzishe wasichezee pesa zetu
 
wamenikata maini kabisa hawa jamaa, mbona wanapiga danadana?
au wanataka tusahau.

wafanyakazi naomba tuungane tulianzishe wasichezee pesa zetu

Wafanyakazi kuungana ndio soluhisho pekee mnyika alilolisisitiza
 
Huu mtindo wa kuungana humu kwenye mitandao halafu hatuchukui hatua nimechoka,
natamani nikaungane na watu wa madini niunganishe nguvu huko ili nidai haki yangu kwa
hawa mafisadi wanaonilazimisha kuwakopesha mpaka nifikie huo umri ambao sina waranty nao.
 
Hivi sheria mpya inapoanzishwa makali yake yanaanza toka sikuile iliporasimishwa "effective date" au inaenda mpaka nyuma "retrospectively"? Kwa maana wafanyakazi walishaingia mikataba ya ajira nawaajiri ambayo pia ilihusisha mafao yao chini ya sheria ya zamani za mifuko hiiikiwemo na fao la kujitoa. I thought yale mafao ya kujitoa kabla ya sheria kuwa effective ni stahili halali ya wafanyakazi. Kwa mfano kama wewe ulifanya kazimiaka kumi kabla ya sheria hii basi wasitahili fao lako kabla ya kuanza kwa sheriahii. Hebu "our learned brothers" tupeni somo kwenye hili suala.
 
Watingaji tuna sema, wasipopeleka muswada mwezi november watanzania kwa mara ya kwanza mtashuhudia serikali inaua wananchi wake kama ilivyotokea marekana-kwa makaburu.

Hakuna faida ya kuishi kama mtu unadhurumiwa hata kilicho chako-it is better to die fighting for our right rather than long living as a fu*ck*en slave!-serious no joke!
 
Huu mtindo wa kuungana humu kwenye mitandao halafu hatuchukui hatua nimechoka,
natamani nikaungane na watu wa madini niunganishe nguvu huko ili nidai haki yangu kwa
hawa mafisadi wanaonilazimisha kuwakopesha mpaka nifikie huo umri ambao sina waranty nao.

Kuungana na wamadini inabidi muanze na sehemu zenu za kazi na kuwabana mameneja rasilmali watu kuwaita na kupata tamko na msimamo wa wafanyakazi. Sekta ya madini walikuwa tayari kugoma ili kieleweke, na hata chama cha wafanyakazi TAMICO sauti yao ilikuwa ni moja. Solidarity....
 
Back
Top Bottom