Stars yashindwa kuweka kambi Bulyanhulu

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
KAMBI ya timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’ iliyopangwa kuwekwa katika machimbo ya Bulyanhulu imehairishwa kutokana na matatizo ya hali ya hewa.

Kwa mujibu wa habari zilizotufikia kambi hiyo sasa itaendelea kuwa Dar es Salaam baada ya sehemu iliyopangwa awali kutawalia na mvua.

Stars inatarajiwa kucheza na Sudan mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu ushiriki wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) Desemba 13 mwaka huu huko Sudan.

Kutokana na hali ya joto ya Sudan, Stars inatakiwa kuweka kambi katika eneo lenye hali inayoshabihiana na huko.

Mwishoni mwa wiki Stars iliifunga Sudan kwa mabao 3-1 na kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika fainali hizo.

Habari zaidi nenda NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Ushauri wa Bure

Waende nchi za Kiharabu kuna joto kulee. Lakini mbona Dar kwenyewe kuna Joto la Kufa Mdudu
 
Back
Top Bottom