Stars vs Moroco in JF

CAF wangefikiria kujumuisha na "worst losers" huenda lngesaidia timu kama Taifa Stars kufuzu siku zijazo!
 
Nilikuwa naangalia comments za wale waliokuwa wanafuatilia mechi ya Taifa Stars. Wengi walionyesha imani kwa asilimia 100. Nilichogundua kuwa wengi wetu hatujui soka na tunacomment kwa kuwa sisi ni watanzania. Kwa ujumla taifa Stars haikuwa na hata asilimia 10 ya kuweza kufuzu kwa kuwa timu yetu haina uwezo.

Ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa Taifa Starz inaumizwa na wachezajiwetu wa "kimataifa aka wa kulipwa" ambao asilimia 75 yao wanapigwa benchi tu kwenye vilabu vyao kwahiyo wanapokuja nyumbani hawawezi kuisaidia timu. Nwapongeza sana wale walioonyesha kuwa kocha aanze kuzitazama vilabu vyetu nchini kwa kuwa wengi wa wachezaji hao wanapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwahiyo wako fit kuliko hao wanaotoka nje.

Naomba kuwakilisha
 
unachosema ni kweli mkuu,kwani wachezaji ambao wanacheza ligi za nje hudhani wa ka wao ndo kila kitu kumbe huko husgua benchi msimu mzima wakija hapa tunadhani ni wazuri kisa wapo nje,kumbe hamna kitu
 
Kwa mujibu wa Title yako ni kwamba unajiuliza, unashangaa au unatuuliza??!!!
 
unachosema ni kweli mkuu,kwani wachezaji ambao wanacheza ligi za nje hudhani wa ka wao ndo kila kitu kumbe huko husgua benchi msimu mzima wakija hapa tunadhani ni wazuri kisa wapo nje,kumbe hamna kitu

Kwa kweli ndugu Mikatabafeki hao wachezaji wanaotoka nje ni bomu kabisa. Kocha anatakiwa kuzingatia wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani
 
Leo vijana tuliowatuma Moroco wamerudi lkn safari bila shamlashamla za mapokezi. Jaman kwanini tusiwe tunashara furaha na huzuni?. Source: TBC
 
Kiukweli huwezi fiwa ukaonesha furaha,tatizo la watanzania mnaharaka sana ya kila kitu suala hapa ni kujipanga na sio kuhitaji furaha isiyoiwekeza,unawajua algeria walishirki kombe la dunia wapo hoi,misri,nigeria,cameron,africa kucn wapo wapi unavyofikiri unawashinda kwa uwekezaji wa ktk soka?mbona hawajafuzu?wanavilabu vizuri,viwanja vya kutosha,timu za vijana imara,wachezaji wengi wapo kwenye ligi kubwa ulaya stil wameangukia pua hatuna haja ya kulaumu vijana wetu tujipange ipo cku tutafika,tunahaki ya kufurahi cos tumeonesha upinzani but tuna safari fupi tu ya kuyafikia mafanikio na hili litawezekana kama kamati ya ufundi pale tff itaacha ubabaishaji
 
Back
Top Bottom