Stars hakuna jipya

Kijamani

Senior Member
Nov 10, 2009
159
9
Kufuatia kuboronga kwa timu ya taifa katika michuano ya kirafiki hoja mbalimbali za wadau wa soka zimekuwa zikitolewa karibu kila siku.Wengi wao wamekuwa mstari wa mbele kupeleka lawama zao kwa kocha Maximo.Ni kweli kwamba kila mtu ana utashi wake kutokana na kile alichokishudia.
Swali la msingi la kujiuliza Watanzania ni kwamba tangu uhuru timu yetu ya taifa iliwahi kushiriki na kuleta vikombe mara ngapi katika michuano mikubwa ya kimataifa?Je tuliwahi kujiuliza ni sababu zipi ambazo zinatufanya tuwe hapa tulipo hadi sasa na tulifanyia kazi mawazo yetu ambayo tuayatoa?
Suala la msingi kwa sasa ni kuweka tofauti zetu chini na kuanza kuwekeza kwenye soka la vijana ili miaka mitano ijayo tuweze kuwa na timu bora ya kuweza kupambana na timu kama Misri,Cameroon na nyingine kubwa ambazo ziliwekeza soka la watoto tangu mapema.
Hakuna sababu ya kushangaa matokeo mabaya ya Maximo na kusingizia kutokuwepo kwa Kaseja golini kwani kabla ya hapo Kaseja alishachezea timu ya taifa na bado matokeo yalikuwa mabovu.
 
mimi nafikiri watanzania tunamatamanio na ndoto kubwa sana, naelewa kua kutamani na kuota ndoto chanya sio dhambi wala sio tatizo.

ila unapo ota na kutamani zaidi ya uwezo wako ni tatizo, watanzania wanalaumu matokeo ya taifa stars na mchakato mzima wa uendeshaji timu kwa ujumla utafikiri timu ilikua inashinda vikombe na kufanya vizuri hapo awali kabla ya kuja maximo.

tumejisahau ya kua mpira wa miguu au jambo lolote lile iliuwe na mafanikio unaitaji matayarisho ya muda mrefu sana na kijipanga kwa mipango inayo tekelezeka na kueleweka kwa watendaji wenye nia ya kutekeleza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom