STAR TV Tuongee Asubuhi 24th July 2011 - Mjadala Nidhamu Bungeni Part 2

Mkuu asante kwa kutujali lakn nikushauri kwamba ingekua vema kama ukaleta mada mtakayoijadili siku moja kabla ya kupresent hiyo mada kupitia Tv ili watu waweze kutoa michango mingi binafsi nimekuta mnamalizia kipindi lakn ntajitahidi kufuatilia kama ulivyosema kua kipindi kinaweza rudia either J4 au J2.

But all in all thanks mkuu kwa kuleta mada kwa watz na ikibidi tuombe humu tuweka mada mbalimbali then chagua the best topic then ukapresent kwenye tv
 
Kweli watanzania tunapenda kushabikia mambo ya hovyo ndo maana hata baadhi ya viongozi wetu ni wa hovyo,inaonekana tutakuja kuwa wa hovyo tusipojiangalia!
 
Viti maalum havina manufaa yoyote sijawahi ona mbunge wa viti maalum ametoa hoja ya msingi
Hoja za Msingi wtazita wapi wakati ni ujanja uliotumika ili kuongeza idadi ya wabunge wa chama tawala kutoa sauti ya NDIYOOO Ili kupitisha hoja kwa kigezo cha sauti,ukweli ni mzigo mzigo mkubwa!
 
Viti maalumu wote wapo kwa maslahi ya vyama vyao tu na la tusitegemee kuona anaweza kuwa na mawazo yake binafsi.hii na kwa namna wanavyopatikana nika kundi la fadhila,wanafahiliwa kuongeza idadi tu hawana ubavu kwa wabunge wa kuchaguliwa.
 
Yahya,

Shukrani kwa kusoma maoni yetu na kuonyesha kuwathamini watanzania watumiao mtandao huu wa JF. Nimefahamishwa umeyasoma.

Shukrani Mkuu kwa kutambua jitihada zetu pia Mkuu. JF imekuwa kiungo na chachu muhimu kushape mada zangu katika mijadala ya LIVE on TV. So napenda pia kutambua na kuheshimu michango ya wanaJF
 
Tumeonelea ni vema tukaurejesha tena mjadala huu kutokana na kuendelea kuyumba kwa usimamizi wa shughuli za kila siku Bungeni na hivyo kupelekea mizozo na kurushiana maneno kwa wabunge mara kwa mara.

Tafiti za karibuni zinaonyesha kuongezeka watazamaji wa Bunge hata wale ambao walikuwa hawalitazami, wanafanya hivi si kwa kufuatilia masuala muhimu ya kitaifa bali kujua leo nani kapewa mipasho na mwenzie ( kama tujuavyo hulka ya watanzania wengi kushabikia mambo ya hovyo hovyo)

Michango iwasilishwe kupitia 0685 358973 (Live Text zitasomwa wakati wa Kipindi ) kipindi kinaanza saa 1 na DK 30 hadi 3 kamili asubuhi

Mnapo sema nidhamu bungeni kwanza laziama tujiulize twende mbele ila lazima turudi nyuma tujue chanzo chake ni nini haswa kuibuka kwa wimbi ati bunge halina nidhamu kivipi hivi mumeisha wahi ona Bunge la Uingereza waziri mkuu anazomewa na mtu anarusha kabisa kijembe kumbukeni Uingereza imeendelea sana pamoja na makelele yao bungeni hapa kwetu mwajifanya tai munataka nidhamu nidhamu gani kwanza viongozi wanapitisha Budget kumbe kuna posho imepita kwa chini then Warioba anasema bunge limekosa nidhamu gani ya kulopoka au Kupitisha rushwa watufafanulie wano sema bunge limekosa nidhamu.

Kwa hali alisi waziri anajibu jibu ambalo kabisi mtu wa kawaida akiliona jibu au kusikia jibu anajiuliza mara mbili hivi huyo kiongozi anajibu hilo jibu kweli kwanini asikalibishe vijembe na minong'ono bungeni wajibu wananchi kinachotakiwa kujibiwa sio bla bla tuuu ilimradi umejibu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom