Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,277
- 9,912
Serikali kupitia Tume ya Mawasiliano nchini imesema kuwa ifikapo Disemba 31 mwaka 2012 ndiyo itakuwa mwisho kwa vituo vyote vya televisheni kurusha mawasiliano yake katika mfumo wa analogy na kujiunga na mfumo wa digitali, hivyo basi kwa msingi huo kampuni ya Sahara Media Group na wadau shirika wako kwenye mchakato kuharakisha zoezi la kusimika minara na mitambo kwaajili ya kuingia kwenye masafa bora ya kisasa.
Mkurugenzi wa Sahara Media Group bw. Anthony Dialo akiongea na waandishi wa (habari wataonekana katika picha nyingine) ambapo amesema kuwa kuanzia mwezi Septemba 2012 minara na mitambo ya king'amuzi kipya itawashwa rasmi kwaajili ya kuanza kufanya kazi. Star Tv pamoja na televisheni zote za IPP zitaingia katika mfumo wa digitali kupitia king'amuzi hicho.
"Jumla ya leseni tatu zilitolewa na TCRA kwa ajili ya kurusha matangazo ndani ya mfumo wa digitali, TBC wakishirikiana na Star Media wanakingamuzi chao kiitwacho Startimes, Makanisa wakishirikiana na Agape wanaking'amuzi chao kiitwacho Ting, na leseni ya tatu ilitolewa kwa Sahara Media Group wakishirikiana na IPP, hivyo kaa tayari kujionea mapinduzi mapya ndani ya mfumo wa Digitali" Aliongeza Mkurugenzi huyo wakati wa mahojiano yaliyofanyika kwenye minara ya urushaji wa matangazo iliyopo katika vilima vya Nyanshana wilaya ya Ilemela jijini Mwanza..
Mkurugenzi wa Sahara Media Group bw. Anthony Dialo akiongea na waandishi wa (habari wataonekana katika picha nyingine) ambapo amesema kuwa kuanzia mwezi Septemba 2012 minara na mitambo ya king'amuzi kipya itawashwa rasmi kwaajili ya kuanza kufanya kazi. Star Tv pamoja na televisheni zote za IPP zitaingia katika mfumo wa digitali kupitia king'amuzi hicho.
"Uzuri wa mfumo wa digitali kupitia kingamuzi unakupa fursa ya kupata chanel nyingi zaidi katika frequency moja, Inakupa afya ya macho kupata picha safi kwa matukio na taarifa mbalimbali" says Mr. Dialo.