Star TV LIVE: Mapitio ya Mjadala wa Bajeti

kibamba anawachana live. kikwete dhaifu, bunge la magamba wazembe. udhaifu, uzembe siyo matusi.
 
Deus Kibamba:
Kazi ya bunge ni kuhakikisha bajeti imejadiliwa na kupitishwa kwa umakini.
Wabunge kwenda kwenye shughuli au kwenda kulala hotelini wakati wa kupiga kura ni tatizo. Kura ya mtu ineweza kuleta mabadiliko.
Wabunge wengi ninaowaangalia bado hawajajifahamu.
Mbunge akishachaguliwa anavua uchama, na kuvaa sura ya kiongozi wa kitaifa.
Lugha za matusi imekuwa tatizo kwa vyama vyote.
Wabunge bado wameshikilia mno umaarufu wa kichama.
Ukiukaji wa makusudi wa kanuni za bunge. Wabunge wanaoongoza kukiuka kanuni za bunge ni wasomi na uelewa, hivyo kigezo cha elimu sikubaliani.
Naungana na Mnyika kwa kauli yake ya udhaifu wa rais, na uzembe wa bunge, lakini siungi mkono upuuzi wa CCM.
Kitendo cha Mnyika kuhukumiwa kwa kulitaja jina la rais siyo fair kwasababu wapo waliotaja majina ya viongozi wa upinzani hawakuwajibishwa.

Willy anasisitiza kusema rais wa jamhuri ni dhaifu haikubaliki.
 
Le Baharia Mutuz ni dhaifu sana. Hawezi kujenga hoja, anaonesha grudges na either Mnyika or CHADEMA!
 
Kibamba Huo ndo udhaifu wa wabunge, kama bunge likishindwa kutimiza wajibu wake, wabunge wa CCM kujipendelea ni udhaifu, kupitisha bajeti Dhaifu ni Udhaifu pia.

Pia Kuacha kujadili bajeti na kuanza kumtukana JJ Mnyika Ni Udhaifu pia na Ni Upuuzi wa wa bunge wa CCM kushangilia MIPASHO ZAIDI kuliko mambo ya Msingi ni Upuuzi na Udhaifu Mkubwa.

Tukubali CCM na Viongozi wake Ni dhaifu na ndio walitufikisha hapa tuendelee kuwa Maskini huku tuna utajiri wa Mali asili
 
Degree sio solution kwa wabunge, tatizo ni kuwa wabungenwengi wanaendekeza itikadi za chama kwa masuala ya kitaifa, wabunge wapewe seminar za kutosha kutofautisha jukwaa la bunge na jukwaa la chama
 
Baruani acha kujipendekezapendekeza kwa Ccm!! Halafu Yahaya,balance mjadala kwa kuwapa nafasi akina Zitto na Msigwa Fursa ya Kuzungumzia Issue ya Mnyika!!
 
Ahsanteni sana Wadau kwa michango yenu na niombe radhi kwa michango ambayo hatujaisoma hewani ila bado ni ya Afya kwa maendeleo ya Taifa hapa JF.

Niwatakie JUMAPILI njema na ahsanteni sana
 
kosa kubwa sana katika mjadala wa bajeti ni kitendo cha kipuuzi cha Mwigulu Chemba kutupa bajeti na kuiita rubbish! A problem is Ndugai Job
 
Hongera Mh Zitto wape Hekima zako, nikweli wengi wanapenda mijadala ya mambo ya hovyo wakati CDM wamezungumza mambo mengi ya manufaa ya kwa nchi ktk Bajeti hii , tuzungumze yote ambayo Wabunge wetu Makamanda wetu Wanavyopigania Nchi yetu.
 
ndugu Yahya natoa ushauri wa bure. Bituro Kazeri wa Pizzeria anaitumia star tv kwa ajili ya kampeni. Mwanza is the 2nd city with a lot of potential people. Take care
 
Mch. Msigwa:
Siasa za tanzania watu wamejijenga katika taswira mbili kama tikiti. Ndani mwekundu na nje kijani. Watu wenye tabia hii ya uwoga hawafai katika jamii. Hii ni kutokana na baadhi ya wabunge wa ccm kukimbia kupiga kura, kabla ya kupiga kura walitoka nje bila taarifa. Mbunge anatakiwa kuonyesha msimamo wake!


Hali hiyo inasababishwa na mtu kutegemea kuteuliwa waziri, naibu waziri, mkuu wa mkoa au wilaya na kwenye bodi mbalimbali. kwa kifupi, ubinafsi badala ya msukumo wa kuwakilisha mategemeo ya wapiga kura.
 
Nimeuliza toka mwanzo kwani mjadala ni bajeti au JJ Mnyika?Yahya M'med akanijibu ni Bajeti...lakini Star Tv kwa makusudi wamegeuza kumjadili Mnyika...tena Baruani ndo anajipa mamlaka ya kuhukumu!ivi hawakusikia dharau za Mwigulu?matusi na upuuz wa kuitupa bajeti ya upinzani?
 
Kaka Willy nilikusikiliza sana ila noana bado uko kwenye enzi za chama kimoja aisee, Karibu kwenye siasa za maji taka za jijini Dar maana nasikia unaomba nafasi za Jumuiya wa wazazi
 
Kiukweli nimemshangaa sana william, nilikuwa na imani nae kuwa labda anaweza akawa wa tofauti ila nimegundua huwezi ukawa ndani ya CCM ukawa tofauti. Sijui alielewe ajenda ya leo au ndo kutaka uongozi kwa huruma za chama chake kwa kukandamiza wapinzani. Anyway the truth is already spoken JEYKEI NI DHAIFU.
 
Back
Top Bottom