Star TV LIVE: Mapitio ya Mjadala wa Bajeti

Ni kweli kwamba uongozi ni karama lakini uwezo wa kuielewa budget na kutoa mchango kuiboresha ni zaidi ya karama, unahitaji elimu.
 
Wana CCM wanapenda sana kusifiwa hata ktk mambo yasiyo ya msingi na Hawataki kuambiwa ukweli. Hivi JJ Mnyika alisema Uongo? mbona liko wazi sana Serikali ya CCM na Viongozi wake ni Dhaifu mno? Dhaifu si tusi
 
Willy,

Kuna taarifa kwamba wale wabunge wa CCM waliokataa kuiunga mkono bajeti watawajibishwa, wakiwepo wale waliotoka nje; unasemaje?
 
Kuna haja ya Bunge kurejea kanuni zake ili kumpa mzungunzaji nafasi ya kumaliza changio lake kabila ya kuzingatia Muongozo au kumtaka mtu kuondosha maneno kabla hajamaliza hoja yake.

Watu tunamlaumu John Mnyika [MB] lakini kimsingi hakupewa nafasi kumaliza ufafanuzi wa kauli zake, pengine angepewa hiyo nafasi leo hii tusingemsema ametukana
 
Nina mashaka kama baadhi ya wabunge wanaelewa maana ya bajeti. Inashangaza mtu anasimama kukashifu, kukebehi na kufanya personal attacks. Sasa huko ni kuchangia bajeti kweli?
 
Tumefika hapa tulipo kwa udhaifu wa rais kikwete.
Tumefika hapa tulipo kwa uzembe wa bunge
tumefika hapa tulipo kwa upuuzi wa ccm. By JJ Mnyika

Silly season. By TL
 
Ni kwanini Naibu Spika hakutaka Mnyika aweke wazi UDHAIFU wa Rais na na Upuuzi wa CCM? ama Alizuiwa kwa sababu iko wazi kwamba Rais ni Dhaifu na CCM ni wapuuzi, Au inamaanisha hawakutaka ukweli huu ukae kwenye Kumbukumbu za Bunge?
 
Baruany Muhuza yuko biased. Maswali yake yanaonekana wazi kupendelea CCM
 
William Malicela ni dhaifu, Star Tv. William hana hoja anataka kujipendekeza tu kwa uongozi wa CCM, Mnyika alikuwa sahihi na alitakiwa kupewa muda wa kujieleza na kufafanua haki ya kujieleza William nakuhakikishia hautapata umaarufu kwa umma bali kwa uongozi wa CCM.
 
Unaona sasa, mada inasema mjadala wa bajeti lakini base kubwa ya nukuu hii ina-base kwa Mnyika kutuonyesha kwa jinsi alivyotolewa bungeni, si vibaya lakini Yahaya kwanini agenda ya Mnyika inakula muda mwingi kuliko kusikiliza hoja zingine?

Infact alichokisema Mnyika si kauli yake bali ni kauli ya waTZ walio wengi, yako wapi maisha bora kwa kila MTZ? WaTZ wamechoshwa na ugumu wa maisha unaosababishwa na CCM kwani ni mara ngapi watu wanaongea mitaaani vijiweni na hata majumbani kuwa JK ni dhaifu...? CCM ni hovyo na Bunge limekuwa ni kama Kariakoo, NAungana na Mnyika kuwa JK ni dhaifu na CCM ni UPUUZI kwani ni kweli hayo na hata mengi matusi ndio lugha ya walala hoi siku hizi hivyo mnyika amewakilisha kundi kubwa sana la wakesha njaa.

NA huyo willy ni Hovyo kwanza namuona kama hana hoja badala ya kunyoosha hoja anatumbukiza mno kujiremba kwa kuchanganya maneno. Nasikitika kusema siasa si fani yake.
 
Nakubaliana na William Elimu si kigezo cha uongozi mzuri, Kusoma ni Kalamu akili ni kitu kingine na Utendaji wa mtu haupimwi kwa elimu yake, Mi nadhani tutafute viongozi walionania ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli na walio na utashi wa kweli wa kuleta maendeleo.

Shida iko kwenye Ubinafsi wa viongozi wetu,
 
Yaaani huyu Malecela yupo hapo kwa ajili ya Kumponda Mnyika tu, nadhani Ukada wake wa CCM umemtia Upofu, Mnyika hajatukana, Mnyika ameusema Ukweli Mchungu!! Kama wao walimwona Karopoka walitakiwa wampe Nafasi athibitishe, angeshindwa angalau wangekuwa na Haki ya Kumhukumu!!

Isitoshe huyu Malecela anajishauashaua saaana kutia bidii kuonyesha kwamba Kiswahili kinampiga chenga akidhani kuna fahari katika kujua kuongea Kiingereza!!!
 
Wiliam Malecela, usichokubaliana nacho ni nini? Kauli ya Mnyika kuwa rais wetu ni dhaifu au ukweli kwamba nchi hii imefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa rais wetu?
 
Budget is professional wanabodi na kama wataendelea kuweka siasa mbele katika hili jambo basi na tutaendelea kurudi nyuma as wengi tuliowaona wakichangia ni kama wako kwenye kutetea maslahi ya kichama na hasa hao wa kuteuliwa.

Wananchi wenzangu kuwe na kipengele cha mbunge kuvuliwa madaraka yake mid termly kama hatakuwa na masilahi kwa taifa hili litawafanya wawe makini
 
Back
Top Bottom