Star TV LIVE: Mapitio ya Mjadala wa Bajeti

Wabunge wengi wa ccm wamekuwa na tabia ya kuipongeza na kuiunga mkono bajeti kwa 100%, halafu kwenye mchango wao wanaiponda bajeti kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Hii tabia ya kuwahadaa wananchi ni mbaya sana kwa mustakbali wa taifa. Kinachoonekana ni kujipendekeza kwa rais kwa kuitetea chama badala ya wananchi waliowatuma bungeni.

Another silly season.
 
Kama alivyosema mchangiaji wa kwanza hapo juu, elimu katika bunge letu ni tatizo nafikiri tunatakiwa kubadilisha sheria zinazotawala huu mhimili badala ya kuwa anajua tu kusoma na kuandika anatakiwa kuwa angalau na degree moja.

Fursa hii tunatakiwa kuitumia katika katiba mpya ambayo inakuja. Wakenya wenzetu wameshapeleka hoja binafsi tayari bungeni kwa ajili ya kuwashawishi wabunge wao kuwa katika bunge lijalo mbunge atakwenda mjengoni tu akiwa na degree moja.

Nafikiri na sisi kunahaja ya kulitazama upya hili ili kuboresha huduma katika bunge.
 
Nafikiri Wataalamu waliobobea katika maswala ya Bajeti wajitokeze ili waweze kuwapatia Wabunge elimu na kuwapiga msasa jinsi ya kujadili Bajeti Bungeni:

Tumeona jinsi Wabunge wengi wanavyoshindwa kabisa kuchanganua mambo mazito na ya msingi katika jamii wanabakia tu kuunga mkono hoja basi. Kama vipi Bajeti iwe inapelekwa Bungeni kwa taarifa tu majadaliano na mapitisho yafanywe na Wataalamu kwa kuwashirikisha wananchi wa kawaida kwenye majadiliano ya wazi. .
 
Yahya M, Mnyika alichozungumza kiko sahihi tatizo ni tafsiri ya watu! Na tafsiri aliyotoa ilikuwa precise. Tatizo ni Ndugai ana jazba na yuko kichama zaidi.
 
Naomba nianze kuchangia mawazo yangu kwa kusema kuwa, CCM imekuwa ikituburuza wananchi kwa kupitisha mambo yanayowapendeza wao, na anapotokea mbunge wa chama chao kusema tofauti na mipango yao wanamuwekea vikwazo na vitisho. Mfano, Mbunge Ester Bulaya wa viti maalum Bunda aliposema kuwa wananchi wa Bunda wamemtuma kupinga bajeti Mbunge mwenzake (WASSIRA) na zaidi Waziri akamtisha huyu Dada ati kuwa nani kamtuma kusema hayo wakati sio maoni ya wakazi wa Bunda.

Jambo lingine ni hali ya wabunge wa CCM kutokuwa wakweli na wenye huruma kwa watanzania, na sikushangaa kuona baadhi ya wabunge wa CCM kukimbia wakati wa kupiga kura, hii ni dalili kuwa walikuwa wanaogopa vitisho vya watawala wao.

HITIMISHO:
Kwangu mimi mjadala wa bajeti haukuwa na manufaa kwa bajeti yenyewe, yaani kulikuwa hakuna constructive inputs toka kwa wabunge. Mfano mbunge anatumia dk 8 kati ya 10 anazopewa kuchangia kusema umaskini wa jimbo lake, na mwisho anaunga mkono kwa asilimia 500. Jamani hii ni dharau na kutowajali watanzania.
 
Spika wa Bunge, Naibu Spika, Lukuvi na Wenyeviti wakiacha upendeleo wakati wa vikao vya bunge basi hapatakuwa na shida. Mara nyingi miongozo ya wabunge wa CCM inakubaliwa lakini ya Upinzani hayasikilizwi kabisa. Tuliona mzee wa kufumaniwa alitoa kejeli bila kusimamishwa na Lukuvi, Kapt Komba na wengine. Kweli bungeni kuna upendeleo mkubwa.
 
Naomba kumuuliza huyo Willium Malecela:

Naona anamjadili sana Mnyika, naomba aseme ubaya wa kauli ya Mnyika.

Mnyika kasema "TUMEFIKA HAPA KWASABABU YA UDHAIFU WA RAISI, UZEMBE WA BUNGE NA UPUUZI WA CHAMA CHA MAPINUDZI. Hakuna tusi hapa.

Namshauri huyu William aache siasa za umaarufu kwasasa, asitafute umaarufu wa siasa kupitia mgongo wa Mnyika. Na kama mawazo ya kurekebisha mambo wapinzania wametoa sana na bado CCM imekuwa ni chama kisichotaka kusikia ni kama SIKIO LA KUFA LISILO SIKIA DAWA.
 
Kiti hakiwezi kuwa na heshima kuliko wanaokikalia, sote tunaangalia bunge na tunaona upendeleo wa kiti kwa wabunge wa upande fulani,vimetokea mbuge wa chama fulani anasema maneno yanayoudhi upande fulani na mwenyekiti anaomba mbunge husika arudie alichokisema.

Wananchi tunaangalia na tunajua nani anaharibu bunge, katika hili hatuhitaji kuelimishwa na kina Deus Kibamba na kina Willy hayo wanayoyasema ni mission yao tu na itawasaidia kwenye kupata vyeo ndani ya chama na serikali
 
CCM inalinda maslahi ya wabunge wake na si wananchi na ndio maana inapitisha bajeti ya kujineemesha zaidi wao na si wananchi wengi.CCM iache ushabiki na kebehi.
 
Jembe Zitto limenena. Wapinzani siyo tu wanaikosoa serikali, bali pia wanaishauri serikali.
 
Ebu watanzania tusijifanye hatuoni kinachotokea kwenye mabunge mengine huko duniani, Huko wanapigana watu wakiongea ujinga, siyo maneno tu. Silly Season siyo tusi ni ukweli unaotakiwa ueleweke kwa CCM na Serikali yake walotifikisha hapa kwa mda wa miaka hamsini na kila mwaka tunakutana Dodoma kupitisha bajeti amabyo haijatatua matatizo ya msingi ya watanzania.

Udhaifu wa Rais na Wabunge wa CCM siyo tusi, ni ukweli mchungu ambao watanzania wanatakiwa wausikie. Wezi na wahujumu uchumi wa nchi hii wanafanywa nini na Serikali ya CCM ambayo Rais wake ni Kikwete na wabunge wengi ni wa CCM.

Mambo ya kinafiki yamepitwa na wakati.
 
Mheshimiwa Kebwe utuambie kwa nini mliunga mkono hiyo budget ambayo kwa macho ya wengi inaonekana ni kiini macho. Na utuambie ni kweli chama kinawalazimisha kusema ndio hata sehemu ambayo wananchi tuliowatuma tulisema hapana.
 
Wabunge wengi huokoteza mlemle bungeni hoja zao na wengine husubiri wabunge wa CHADEMA waongee kitu then wapate cha kusema,ama wapate cha kubeza, Kama mbunge angetumwa kwenda bungeni kuwasilisha kile alichotumwa na wananchi kusingekuwepo na malumbano ya maneno ya hovyo bungeni,
 
STAR TV kwanini muifanye issue ya Mnyika kuwa maada kiasi hicho?....mbona Mhasibu wa CCM ndugu Mwigulu aliwaita wana pepo na mapendekezo yao ni rubbish?akaitupa na akatuzwa pesa na Wassira na Chikawe?Vp Yahya hili mbona halizungumziwi?.....
hayo ni mawazo ya mchangiaji katika mjadala, mbona mada yetu inajieleza vela hapo juu.
 
Mchungaji Msigwa:
Hatuwezi kuwa na sura mbili kama ya tikiti, ndani nyekundu nje kijani. Mbunge hapaswi kuwa hivi.Huu ni ujumbe mzuri kwa Le Mutuz
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Fair ground ndio tatizo kubwa ndani ya bunge, Lukuvi akiomba mwongozo anapewa nafasi mara moja lakini chadema wakiomba spika anajishauri.

kwa Deus Kibamba, kiti hakiwezi kupewa heshima kama hakijiheshimu na kutoa usawa. Je unadhani kiti kama kinamtaka mbunge arudie tusi alilotamka, huoni kiti chenyewe kinajidharau??

Namshangaa sana william J Malecela anapokosoa upande mmoja tu yaani CHADEMA tena kwa hoja nadharia ya UMAARUFU, kwa mawazo kama ya malecela Tanzania itabaki kuwa masikini na itaendelea kutegemea misaada.
 
ZittoKabwe: Kuna faida kuwa na chama cha upinzani ambacho sio tu kinalalamika, sio tu kinakosoa lakini pia kinapendekeza nini kifanyike #BRAVE!
 
Mch. Msigwa:
Siasa za tanzania watu wamejijenga katika taswira mbili kama tikiti. Ndani mwekundu na nje kijani. Watu wenye tabia hii ya uwoga hawafai katika jamii. Hii ni kutokana na baadhi ya wabunge wa ccm kukimbia kupiga kura, kabla ya kupiga kura walitoka nje bila taarifa. Mbunge anatakiwa kuonyesha msimamo wake!
 
Back
Top Bottom