Star TV LIVE: Mapitio ya Mjadala wa Bajeti

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Karibuni kwa mjadala ambapo Leo tunaangazia mjadala mzima kabla ya kupitishwa kwa bajeti

Dar yupo Baruani Muhuza, William Malecela LE MUTUZ, Deus Kibamba, na Mza Yahya M na Donald Kasongi

Dodoma yupo faraji mwagoha na mh.Zito, Msigwa na Mh.Stephen Kebwe

Karibuni
 
vitu viwili,

Moja, Kiwango cha Elimu
Bunge ni sehemu wanafanya maamuzi muhimu sana kwa taifa, wabunge hupitisha bajeti ya serikali, wabunge hutunga sheria, wabunge husimamia serikali, ni muhimu kupandisha kiwango cha cha chini cha elimu kwa mtu kuwa mbunge, labda kiwango cha chini iwe degree moja.

Kutanguliza maslahi ya chama kuliko maslahi ya taifa
Wakati mchumi daraja la kwanza wa BOT (kama anavojiita mwenyewe) anasema bajeti ni nzuri sana na imeandaliwa kitaalam ikizingatia viwango vya kimataifa labda ndio maana watu wengine wanashindwa kuielewa, Waziri mkuu akaunda tume kuangalia vyanzo mbadala vya mapato na kuongeza pesa kwenye development budget (ambayo yalikuwa mawazo ya shadow budget). Ukiangalia elimu na uelewa wa mwingulu ni wazi alikua anasimamia maslahi ya chama chake
 
Inakuwaje wabunge wa CCM walitumia muda mwingi kuijibia serikali badala ya kuichambua bajeti? Mbunge anasimama na kuipongeza bajeti kuwa imeandaliwa kiufundi na utaalam, halafu anaanza kueleza matatizo kibao na wala haelezi bajeti iliyopita ilitekelezwa kwa mafanikio kiasi gani?
 
Ahsante mkuu,

Nasikitishwa sana na wabunge wa CCM kuunga mkono kila kitu hata kama ni kibovu mradi kiwe kwa maslahi ya chama.

Nadhani umefika wakati sasa bajeti lifanywe kuwa ni tukio maalumu ambalo litawashirikisha wataalamu mbalimbali bila kujali itikadi zao kisiasa. Suala la bajeti liwe linaundiwa tume maalumu kama ilivyo tume ya katiba ili kufanya bajeti isiwe ya mtazamo wa upande mmoja ki itikadi. Baada ya jopo hilo kutengeneza bajeti hiyo ndipo ipelekwe bungeni kwa ajili ya mjadala.

Kwa kufanya hivyo bila shaka tutakuwa na bajeti bora zaidi na yenye manufaa kwa wananchi.
 
Nilichokiona mimi ni baadhi ya wabunge wa CCM kutumiwa na chama kuwa provocative kwa wabunge wa upinzani ili wabunge wa upinzani wakijibu Mapigo kuonekane hakuna tofauti kati ya CCM na Upinzani. CCM tunajua walishapoteza heshima ndani ya jamii wanachokifanya ni kuwaudhi wapinzani ili nao wapoteze hiyo heshima.

Wabunge kama Lusinde au Mwigulu tunajua ni wabunge walio na septic mouth ambao siku zote wakiongea tunategemea watatukana tu. Wabunge wa chadema kwepeni mtego wa akina Mwigulu, tunawategemea onyesheni tofauti.
 
Le Mutuz, Mnyika hakupewa muda wa kufafanua kwanini alitoa kauli ile, wewe unawezaje kumhukumu kuwa alikosea sana?

Nakushauri acha ushabiki wako kwa CCM. Chambua hoja bila upendeleo. Kama rais ni tatizo kwa nini watu wasiseme?
 
Le Mutuz naona na ww usiwe taken up na itikadi za chama chako, kulaumu upinzani tu bila kuwa mkweli kwamba zile fujo zilianzishwa na CCM ni kuegemea upande mmoja kitu ambacho nadhani tunarudi kule kule kwenye malumbano yasiyo na msingi.

Willy unatakiwa uitumie hiyo nafasi kuonyesha kwamba uko tofauti na wanaCCM wenzako ili ujenge heshima yako na labda ung'arishe nyota yako kisiasa ukizingatia nyota ya CCM au Mvuto wa CCM umekwisha
 
Yahya, huo utaratibu mpya wa kutumia pushmobile gharama zake kwa mteja kwa msg ni sh ngapi?

Naomba utupe twitter account
 
Tuna jadili bajeti ya 2012/2013 wakati hatujui bajeti ya 2011/2012 ilitumika vipi...bunge lingepata muda mdogo wa kujadili bajeti iliyopita iliwaweze kupendekeza mambo mazuri kwenye bajeti mpya inayokuja. T 2015 CDM.
 
Tatizo pia ni uwezo wa spika, Mama Makinda anaonekana ameshindwa kuliongoza Bunge, heshima ya bunge inashuka siku baada ya siku.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Spika anatakiwa kuwa fair na sio kupendelea upande wowote, hiyo ndiyo inatengeneza chuki na hasira!
 
Kitendo cha wabunge wa ccm kuanza kuchangia hoja ya bajeti kwa kuiunga mkono 100% halafu wanaanza kulalamika majimboni mwao hakuna maji, barabara au zahanati huku wakijiua majibu yanapatikana kwenye bajeti ambayo haitakidhi matakwa imeonyesha jinsi walivyo wadhaifu kwa kutokuwajali wananchi na kutetea maslahi ya chama chao kilicho shindwa.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
STAR TV kwanini muifanye issue ya Mnyika kuwa maada kiasi hicho?....mbona Mhasibu wa CCM ndugu Mwigulu aliwaita wana pepo na mapendekezo yao ni rubbish?akaitupa na akatuzwa pesa na Wassira na Chikawe?Vp Yahya hili mbona halizungumziwi?.....
 
Mwanachama mwenzetu Le Mutuz naona ameegemea kwenye ushabiki. Kwanini hutoi karipio kwa wabunge wa chama chako ambao wanaongoza kwa kutoa matusi na kebehi? Umejivika yale yale ya kina Mwigulu?
 
Licha ya kiwango cha elimu,ni vema pia wabunge waweke maslahi ya taifa mbele kuliko tu kuangalia maslahi ya chama chao.Kuna watu wana elimu kubwa lakini bado wanapinga tu mawazo mbadala hata kama ni mazuri.
 
Le Mutuz yupo kichama zaidi, naona anatetea sana lishe! Sijaona kosa kwa Mnyika kusema ukweli kuwa Rais ni DHAIFU. Nashauri Spika awe Neutral na hao CCM waache ushabiki usio na faida!
 
Asante mkubwa ila nasikitika sina acess ya star tv. Hii ni kwa wengi wa nyanda za juu kusini watu wa ufundi watutendee haki. Tunakosa mijadala mizito kama hiyo. Basi msaada wa updates please.
 
Mimi nafikiri hicho kiti cha Spika kisiwe na nguvu kuliko sauti wa wakilishi wa wananchi! Pia kanuni za bunge ziangaliwe kama zinafaa kwasasa, kuna kanuni,ambazo zimepitwa na wakati, Spika hawezi kusema kauli za kuudhi zinazosemwa na wabunge wa CCM zirudiwe huku akiwaambia wa upande mwingine wakae! Huu ushabiki wa kiti nao ushughulikiwe.
 
Back
Top Bottom