STAR TV inafunika TBC

Godwishes

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
640
165
Wakuu,TBC ni channel ya Umma(Shirika la Umma)bt najaribu kukompea programme zake haidizevu kuitwa Channel ya Umma.Star,bg up hasa hiki kipindi cha BBC News kuanzia saa3 usku kwa lugha ya KISW..Mpewe ruzuku Za TBC.A.Diallo take 5.
 
Yaan binafsi sion channel inayoishinda Star Tv, kwa mambo mengi, vipind, ubunif(mfano pika bomu kwa sas)wafanyakazi angalia inavyowachukua ma underground na kuwapandisha chati
 
Mkuu Star TV wako juu sana, kwanza kuwapata online imekuwa msaada mkubwa sana kwa sisi tulio mbali na nyumbani safi sana, na inaonyesha wanavyoenda na wakati.Hao TBCCM wamekalia siasa badala yakwenda na mabadiliko ya Teknolojia.
 
Wanajitahidi pamoja na kwamba wanarusha matangazo yako directly from Mwanza maana tumezoea kila kitu kipo centralized Dar na coverage yao ni kubwa na kwa upande wa radio ukienda vijijini huko ukikuta RFA haikamati basi ujue zingine hushiki au labda watakuwa hawajaweka mnara wao. Wapo strategic sana tangu wameanza na wanarusha mpira live kama juzi Simba na Yanga (kibongokibongo japo facility chache uwanjani kama Super sport lakini mambo yalikwenda safi0
 
Mitangazaji ya TBCCM ukiitazama tu utauona unafiki ulivyo dhahiri nyusoni mwao, utagundua wanafanya kazi kimaelekezo kabisaaaaa.

yaani kila wakati wanaogopa kukosea maagizo, wanajituma kushabikia ccm ili kulinda viajira vyao vya upendeleo.
 
kweli kuna vitu wanaweza kuboresha lakini sijui ni uzembe au nini? Mfano kila mara utasikia tupate habari kamili halafu .................................ukimya tu na wala hiyo habari kamili ya picha haitoki, sasa kweli hiyo motto yao ya ukweli na uhakika ndio hayo?

Mkurugenzi akaze buti mawasiliano yaimalishwe kati ya waandaaji vipindi, wasoma taarifa na mafundi mitambo
 
TBC aliondoka nayo TIDO MHANDO,Siku hizi ni idara flani ndani ya ofisi za pale Lumumba.
 
TBC imerudi ilikotoka yaani TVT na kwasasa wameprove kuwa ni tv ya chama tawala wala si ya walipa kodi!!!!
 
Wakuu,TBC ni channel ya Umma(Shirika la Umma)bt najaribu kukompea programme zake haidizevu kuitwa Channel ya Umma.Star,bg up hasa hiki kipindi cha BBC News kuanzia saa3 usku kwa lugha ya KISW..Mpewe ruzuku Za TBC.A.Diallo take 5.

Star Tv kwa kias kikubwa wanajali nyakati, ubora na uwazi. Wengi wa watanzania wanatamani sana kujua yanayoongelewa kimombo kwenye chanel za kimataifa lakini ngumu.
Star tv wameliweza hilo..bonge la kipindi ANGA ZA KIMATAIFA.
kazeni buti
 
Halafu watangazaji wa TBC wanavigugumizi. Ukiwasikiliza Marin Hassan, Florence Dyauli, Gabriel Zakaria na wengineo kwenye vipindi wanavyoendesha utawasikia wakiuliza maswali kwa kunatanata. Mfano Mheshimiwa Waziri, na-na-na-nasikia u-u-u-umefanikiwa ku-ku-ku-ku-kuwashawishi wakezaji ku-kuja kuwekeza ka-ka-katika sekta ya u-u-usafiri, je hili unalio-o-o-ongeleaje?
 
wabnajitahidi sana star lakini kuna mara nyingine wanarudia vipindi wajaribu kubadilisha hilo kwakwei wapo juu tbccm wapotezee
 
Nakubaliana na wewe kuna kipindi nilikuwa na kazi nao hawa jamaa (ya kibiashara) sasa nikapata fursa ya kuzuru plant yao kule nyamagana baada ya kumaliza makubaliano pale ofisi zao opposite Mwanza Hotel kwa kweli wamejipanga sana hawa jamaa ninawakubali wana mitambo ya uhakika na Samwel Nyalla anajitahidi sana kuindesha kampuni ya kaka yake Diallo
 
Jamani mimi ninampenda sana samadu hassan katika anga za kimataifa 'kuvunjika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi pangu pakavu ntilie mchuzi' uko juu babaangu!
 
Jamani mimi ninampenda sana samadu hassan katika anga za kimataifa 'kuvunjika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi pangu pakavu ntilie mchuzi' uko juu babaangu!

dah, hata me huwa namkubali sana huyu baba. huwa anatoa habari kwa uhakika na masimulizi yake yanaeleweka. hongera zake!
 
Back
Top Bottom