Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Kumbe hata Agoro Anduru alishafariki, so sad. Hadithi za Kiswahili za magazetini zilizonivutia wakati huo ziliandikwa na huyu Anduru (RIP), Ben Mtobwa, Hammie Rajab, Sam Kitogo (napenda nisikie kuwa hawa bado wako hai). Siku hizi hakuna gazeti la kiswahili lenye hadithi nzuri, ule uandishi umeondoka na wahusika.
 
Jamani mnanikumbusha mbali mno gazeti la mfanyakazi na motomoto ila siku hizi tumebaki utadhani tumelogwa na hela na udaku magazeti yananunuliwa ovyo na wanahabari wanahongwa baadhi yao mpaka yanawakuta ya Jerry Muro. tuwaombee Mungu hawa wachache waliobaki wasije wakalogwa tukawa mamluki wa mafisadi
 
Kumbe hata Agoro Anduru alishafariki, so sad. Hadithi za Kiswahili za magazetini zilizonivutia wakati huo ziliandikwa na huyu Anduru (RIP), Ben Mtobwa, Hammie Rajab, Sam Kitogo (napenda nisikie kuwa hawa bado wako hai). Siku hizi hakuna gazeti la kiswahili lenye hadithi nzuri, ule uandishi umeondoka na wahusika.

Ben Mtobwa ni Marehemu sasa pamoja na Elvis Musiba, lakini Hamie Rajabu ni mkurugenzi wa Tollywood Movies inayoshughulika na filamu za Kibongo
 
hiyo kashafa ya loliondo nafikiri haimuachi mzenji mmoja alikuwa wizara ya fedha baadaye akahamia maliasili na utalii, anakwenda kwa jina la somebody hamadi omary, sikumbuki vizuri jina lake. na mzee ruksa, mgumia na ndolanga. hao ndo waliopata vijisenti vya wakati ule! na ndio tunaowaenzi siku hizi! shukrani sana kwa yule kijana kumzaba kibao mzee nanihii japo si uungwana kwa mtu wa umri wake kupata kibao live!
 
Gazeti lake liliitwa Mfanyakazi, kila wiki nilihakikisha napata nakala yangu. Humo ndani pia kulikuwa na hadithi za mtunzi maarufu Agoro Anduru, sijui kaishia wapi siku hizi. Na column fulani ndogo ya vichekesho iliyokuwa ikiitwa Nipashe, yenye picha ya sikio kuubwa.

Nilisikitishwa sana na kifo cha Stan Katabaro, Mungu amweke pema na aisaidie familia yake, Amen.
Agoro Anduru=marehemu
 
Hawa ndo walikuwa waandishi bwana, ila Kubenea naye namkubali, Mnamkumbuka Kabendera Shinani? Naye aliuwawa kule BK kwa kina IWE na alikutwa anaelea ziwani. Wanasema naye alikuwa akifuatilia kashafa moja ya utekaji wa magari mkoani Kagera ambapo kigogo mmoja huko mkoani alikuwa anahusika!
genekai,
Kabendela shinani hakuuwawa na yeyote bali ali commit suicide kwa kujitupa ziwani na watu waliona kile kitendo.

Alitoka nyumbani asubuhi akiwa ndani ya gari yake. akaegesha gari bandarini, kulikuwa na meli ya MV Victoria imetia nanga pale Bukoba, akaingia ndani ya meli na kujitupa majini kwenye maji ya kina kirefu.

Issue yake ni kwamba yeye ni mzaliwa wa Kagera ambaye aliamia Rwanda akaoa huko na kuchukua uraia na kuishi huko. Baada ya ile genocide ya Rwanda alikimbia kurudi huku kama mkimbizi. Lakini kwa kuwa alijua yeye ni mzaliwa wa hapa aliishi nje ya makambi ya wakimbizi na bahati mbaya sana alianza kujiingiza kwenye mambo ya siasa.

Wakati huo huo akiwa Rwanda alikuwa mtangazaji wa redio pale Rwanda, na mwakilishi wa BBC pia pale Rwanda. Lakini pia inaaminika alikuwa rafiki sana wa marehemu rais Habyalimana. Baada ya kifo cha Habyalimana kulitokea machafuko yaliyosababishwa na umwagaji damu sana. Na yeye alikuwa mmoja kati ya watu waliochochea sana through propaganda (kumbuka anayofanya yule Kibonde wa clouds?) mauaji katika radio na baadhi ya wenziwe walikuwa wameshakamatwa na kupelekwa Rwanda na wengine walikuwa Arusha.

Kwa kujihusisha kwake na siasa hapa kulimzalishia maadui na wakafichua siri kuwa pamoja na kwamba yeye alikuwa mzaliwa wa Tanzania lakini alishakana tayari uraia wa Tanzania na kupewa uraia wa Rwanda na kwamba alishawahi kumiliki passport ya Rwanda. Hilo lilifanya watu wa uhamiaji waanze kumuhoji na kumfuatilia sana na kutaka kujua kwa nini hakuwa anaishi katika makambi ya wakimbizi na kwa nini aliwahi kuomba passport ya Tanzania kwenda nje bila kusema ukweli kuwa yeye si raia wa nchi hii? Jambo hili lilimtia hofu sana.

Kwa hofu kwamba wangeweza kumrudisha makambini au kumrudisha Rwanda au kumkabidhi kwa makachero wa Rwanda waliokuwa wanamtafuta at that time, aliona bora ajiue na hivyo akafanya kama alivyofanya. Ilikuwa ni kuogopa mkono wa serikali ya Rwanda.
No body killed him but he killed himself. Familia yake wengine walirudi Rwanda wengine bado wako hapa Tanzania.
 
Jamani mnanikumbusha mbali mno gazeti la mfanyakazi na motomoto ila siku hizi tumebaki utadhani tumelogwa na hela na udaku magazeti yananunuliwa ovyo na wanahabari wanahongwa baadhi yao mpaka yanawakuta ya Jerry Muro. tuwaombee Mungu hawa wachache waliobaki wasije wakalogwa tukawa mamluki wa mafisadi

wasije wakalogwa?
 
Huyo bwana ndiye aliyekuwa mhimiri wa kashfa ya Loliondo kabla ya kutolewa Wizara ya Utalii na kupelekwa kuwa RC Singida. Hivi siku hizi yuko wapi huyo Mgumia?


RIP Katabaro.....Namkumbuka sana jinsi alivyokuwa mwandishi mzuri sana na asiye na woga.

Wadau naomba pia mkumbuke jamaa mmoja anaitwa Anthony Ngaiza ambaye aliwahi kuwa editor wa Family Mirror kwenye miaka ya 1992/93 kabla ya kuhamia MCT. Tunahitaji kweli kuwakumbuka hawa jamaa!

Mintaarafu tu, Anthony Ngaiza yupo, nadhani hapo hiyo post kama vile inamuonesha hatuko nae. Yupo Mwananchi ni Mshauri wa Kitengo cha Uhariri.
 
Alikufa ghafla!.
Kumfananisha Kubenea na Stan, ni kumpandisha tuu chati Kubenea, Stan alikuwa akiandika investigative journalism kwenye developing story, Kubenea anaandika udaku kwenye medani za siasa, sio uchunguzi in a really sense ya uchuguzi. Waliotaka kufuata nyanyo za Katabalo, ni This Day na Kulikoni, walioanza, wakati wakifuatilia story ya Rada.

Kubenea is an overrated semi-literate Katabalo wannabe kama alivyosema muandishi mmoja wa habari.

BTW, I believe the name is Stanley Katabalo, not Katabaro.

Enzi hizo Jumamosi asubuhi lazima ununue Mfanyakazi hata kwa foleni. Mfanyakazi used to be a hot paper (as hot as it could get under Nyerere) nakumbuka kusoma court proceedings za Kesi ya Uhaini na quips za Muccadam Lakha. Hata "Amini Usiamini" tu ilikuwa very interesting.
 
nani anakumbuka issue ya lolionda gate. ukiijua hiyo vema utakuwa unamjua katabaro tunayemzungumza. alikauka ghafla mpaka wa leo watu makini wanasikitika jamani katabaro. where is he We miss him so much. R.I.P

Je, mnakumbuka na ile kashfa ya RIO? Kwenye mkutano wa Mazingira Duniani ulifanyika BRAZIL (Rio de Janeiro)

Kwahakika hakuna kama STAN KATABALO.

Kashfa ya LOLIONDO ilimhusu sana sana ABUBAKAR MGUMIA......

Kubenea is an overrated semi-literate Katabalo wannabe kama alivyosema muandishi mmoja wa habari.

BTW, I believe the name is Stanley Katabalo, not Katabaro.

Enzi hizo Jumamosi asubuhi lazima ununue Mfanyakazi hata kwa foleni. Mfanyakazi used to be a hot paper (as hot as it could get under Nyerere) nakumbuka kusoma court proceedings za Kesi ya Uhaini na quips za Muccadam Lakha. Hata "Amini Usiamini" tu ilikuwa very interesting.

RIP....Stanley Katabalo

Je mnakumbuka kile kisa cha balozi wetu wa Ufaransa.....nafikir wakti ule alikuwa Mh Anthony Nyaki................na mazungumzo ya simu na Mh. Mustapha Nyang'anyi...........dah!
 
Napata tabu kumfikiria mwandishi wa Kitanzania mwenye ujasiri na anayefuata nyayo za mwandishi jasiri na mzalendo, Stan Katabalo aliyefariki/kuuwawa kwa kutetea ukweli, mzalendo halisi aliyeiibua kashfa ya Loliondo enzi ya utawala wa mzee Ruksa.

Labda wana JF mnaweza kunisaidia kuwataja waandishi wa Tanzania ya leo wenye ujasiri huu ili tuwape sifa ya mzimu wa Stan!
 
Back
Top Bottom