"Stakabadhi ghalani zaiua CCM Kilwa'

mzee wa mawe

Senior Member
Aug 2, 2011
151
15
WANACHAMA 395 wa chama cha mapinduzi (ccm) wilayani Kilwa, mkoani Lindi wamejiunga na CUF baada ya kuchukizwa na mfumo wa stakabadhi ghalani katika ununuzi wa zao la ufuta. Akizungumza jana jijini Dar es salaam, Naibu mkurugenzi wa mipango, uchaguzi na Bunge wa CUF, Shaweji mketo, alisema zoezi hilo lilifanyika wakati wa ziara yake wilayani humo kuanzia julai 23 hadi 29, mwaka huu.

Mketo alisema jumla ya waliojiunga na chama hicho ni 1,108, huku 395 wakitokea CCM na ambao amewakabidhi za chama hicho. Alisema wanachama 675 hawakuwa na chama na 38 kutoka CHADEMA.

Mketo alisema wanachama wengi waliojiunga na chama hicho walisema kuwa walikasirishwa na mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umekuwa ukiwanyonya wakulima. Alisema kuwa kilio cha wakulima hao ni kutaka uhuru wa kuuza ufuta kwa wafanyabiashara ambao hununua kwa sh 1,700 kwa kilo badala ya vyama vya ushirika vinavyonunua kwa sh 1,000 kama vilivyo agizwa na serikali.
 
Asante kwa taarifa mkuu ila usitarajie kupata michango humu na hata kama utapata itakuwa ni negative contributions. Subiri mazezeta ya chadema yaione hii chokochoko niliyoianzisha.
R.I.P CCM very soon
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom