Staili inayokubalika pasaka hii

Ninja

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
348
535
WAKUU WANA JF JINA LA BWANA YESU KRISTO LITUKUZWE

Yoh 3:16 inasomeka hivi ' kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwana wake wa pekee ili kila amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele.'

Ni vizuri pasaka hii tukaisheherekea kwa kukumbuka kwamba Mungu kwa kutupenda, alimtoa mwana wake pekee kwa ajili ya dhambi zetu yaani Yesu Kristo(Math 1:21).

Unaposhawishiwa na shetani kufanya maasi wakati huu wa pasaka, kumbukumbu hii ya upendo wa Mungu kwetu na ikuzuie wewe ili usimwasi Mungu.

PASAKA NJEMA KWENU NYOTE NA BWANA AWABARIKI SANA!
 
thanx Ninja baraka za bwana ziwe nawewe katika kipindi chote cha pasala na ha milele
 
WAKUU WANA JF JINA LA BWANA YESU KRISTO LITUKUZWE

Yoh 3:16 inasomeka hivi ' kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwana wake wa pekee ili kila amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele.'

Ni vizuri pasaka hii tukaisheherekea kwa kukumbuka kwamba Mungu kwa kutupenda, alimtoa mwana wake pekee kwa ajili ya dhambi zetu yaani Yesu Kristo(Math 1:21).

Unaposhawishiwa na shetani kufanya maasi wakati huu wa pasaka, kumbukumbu hii ya upendo wa Mungu kwetu na ikuzuie wewe ili usimwasi Mungu.

PASAKA NJEMA KWENU NYOTE NA BWANA AWABARIKI SANA!

Bwana Yesu atujalie amani na upendo kipindi chote hiki. Ee Bwana wetu Yesu Kristo tunakusihi kusiwepo na ajali kipindi hiki na sote tusherehekee kwa amani, utulivu, upendo na furaha.
 
Kweli kabisa ajali hizi Mungu aziepushe.
 
Na mwana wa Mungu afufuke moyoni mwetu ili damu yake iliyomwagika iweze kutuweka huru
 
Bwana atubariki na kutulinda, aendelee kutuongoza katika njia itupasayo na muhimu zaidi afufuke mioyoni mwetu katika pasaka hii ili tuweze kubadili mienendo yetu na kufanya yote yanayompendeza yeye.
 
Back
Top Bottom