Spika wa DARUSO ajiunga CCM

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Wana JF, napenda kuwafahamisha kuwa sasa wasomi wetu wanaanza kuja na mwelekeo tofauti na tunavyoweza kudhani. Spika wa Bunge la chuo kikuu cha Dar es salaam Daruso ambaye amemaliza muda wake Bwana Mwangomango amejiunga na Chama cha mapinduzi na kukabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa CCM Jumapili mchana tar 17 kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya CCM Dar es salaam
Wasomi wetu wamejivua gamba ama sasa wanavaa magamba??
 
bora huyu ameamua kutenganisha pumba na mchele......na bado the list is long........!
 
Wana JF, napenda kuwafahamisha kuwa sasa wasomi wetu wanaanza kuja na mwelekeo tofauti na tunavyoweza kudhani. Spika wa Bunge la chuo kikuu cha Dar es salaam Daruso ambaye amemaliza muda wake Bwana Mwangomango amejiunga na Chama cha mapinduzi na kukabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa CCM Jumapili mchana tar 17 kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya CCM Dar es salaam
Wasomi wetu wamejivua gamba ama sasa wanavaa magamba??

sasa bibibata wewe, kwa tafsiri yako kuvua gamba ni kujiunga na cdm ama? acha mtu ajiunge na chama anachopenda ikizingatiwa tz hamjiungi na vyama kwa kuangalia itikadi, bali fursa za ulaji tu.
 
sasa bibibata wewe, kwa tafsiri yako kuvua gamba ni kujiunga na cdm ama? acha mtu ajiunge na chama anachopenda ikizingatiwa tz hamjiungi na vyama kwa kuangalia itikadi, bali fursa za ulaji tu.

Ukijiunga CDM kuna ulaji gani? Virungu vya polisi na mabomu ya kutoa machozi? Ukiniambia wanaojiunga na ccm ndio wanaotafuta kuganga njaa nitakuelewa.
 
Ukijiunga CDM kuna ulaji gani? Virungu vya polisi na mabomu ya kutoa machozi? Ukiniambia wanaojiunga na ccm ndio wanaotafuta kuganga njaa nitakuelewa.

Wabunge wa CDM hawakupokea milioni 90 za kununua magari? Acha kupoteza umma, wanasiasa wetu wengi wa sasa; wa CCM, CDM na vyama vingine ni ulaji kwanza.
 
Ni uamuzi wake. Ameamua fungu lake lakini si wasomi wote walioko Chadema. Nae ameamua kufanya uamuzi wake kwenda CCM kama walivyowahi kuamua akina Dk. Masumbuko Lamwai n.k sioni hoja wala umaarufu wa huyo mtu. Msomi mwingine kama Mtatiro alijiunga na CUF n.k
 
Njaa inaweza kumfanya mtu akachukua uamuzi wowote ule ikiwa ni pamoja na kuiweka rehani familia yake au hata kupiga mnada utu wake.

Halafu jamani hivi hata Spika Mstaafu wa DARUSO nae ni mtu maarufu wa kufanyiwa reference?
 
Wamechoka kuzomea zomea!

Nilidhani zomeazomea iko ndani ya bunge. Mwenzangu umeona wapi zomea zomea? Kwanza huyo jamaa ni nani hasa mpaka 'tumjadili'? Ni mtu wa kawaida sana. Na kaamua kujinyumbulisha, ama uko moto au baridi na sio Mlengo wa Kati. Mtu mwenye Mlengo wa Kati ni ndumilakuwili, hafai.
 
Njaa 2, hana uelekeo... namjua sana huyx dogo wa sheria, kwa taarifa yake nafasi ndani ya ccm ni kwa ukoo 2, si unaona leo january makamba.
 
Back
Top Bottom