Spika wa bunge (Anne Makinda) akiri posho kuongezwa!

Hili tatizo la kupinga pinga, linazidi kukomaa miongoni mwa magamba, Wabunge walisema zimeongezwa, katibu akapinga, leo Maddam speaker anakiri zimeongezwa! sasa yule Kashilila sijui anajiskiaje huko alipo, maana hatutarajii Dr. mzima kudanganya kitoto toto namna hiyo
The Hunter, jana nikichangia kanusho la Kashilila kuhusu kupanda kwa posho zawabunge nilisema "Kashilila kapewa kozi na Nape ya kubadilisha ukweli kuwa uwongo na uwongo kuwa ukweli".
 
Mshahara na posho ya mbunge kwa mezi 12,000,000 + 10,230,000 = 22,230,000 (millioni ishirini na mbili laki mbili na elfu thelathini)
 
Spika Makinda kasema Wameongeza Posho kwa wabunge kwa sababu moja tu, "hali ya maisha katika Mji wa Dodoma imepanda" sasa sijui na wafanyakazi wote wa Dodoma mslai yao yatafikiriwa? Na kama hali ya maisha imepanda, sijui wamegundua katika Mji wa Dodoma tu...! Jamani Wanasiasa mmeonyesha wazi kuwa mnajali maslai yenu kuliko Wananchi wenu. Kwa hali hii hatutafika popote.
 
Mungu atunusuru sikujua kama mambo ndio hivi spika wazaiwazi anasema wabunge ndio wenye maisha magumu na ndio waondezewe posho. Kuanzia sasa hivi namuombea laaana spika na wabunge wote na familia zao wanaopokea ongezeko hilo maana sina la kufanya ila Mungu anaona hali halisi. Kwa mtazamo wangu naomba watanzania wenye kuitakia mema nchi yetu wasijitokeze kwenye hii ishu ya kusheherekea miaka 50 kwani dhihaka na uzalilishaji mkubwa ambao haujawahi kufanyika duniani kote. Naomba tuwaache viongozi na waalikwa wao wakisheherekea jinsi walivyotuibia kwa miaka 50. Na mwanzo wa miaka mingine 50 spika anatutangazia mwanzo wa miaka mingine ya kutuibia kwa kutuaminisha kuwa maisha magumu ni kwa viongozi peke yao. EEE MUNGU NAOMBA UMALAANI KIONGOZI YOYOTE WA TANZANIA ALIEWAHI KUTUIBIA NA AMBAE AMEJIPANGA KUENDELEA KUTUIBIA KAMA SPIKA MAKINDA WAWE MATAAHIRA PAMOJA NA FAMILIA ZAO. MAANA KATIKA BIBILIA UMESEMA MENO YAO YAMETIWA CHACHU KWA VYAKULA WALIVYOKULA BABA ZAO.
 
Halafu naomba ieleweke kwa siku wanalipwa posho sh laki 3 na 30.Yaani sitting allowance laki 2,per diem elf 80 na mafuta ya gari elf 50
 
Maisha ya Dodoma naona yamepanda kwa waheshimiwa wabunge tu, wafanyakazi wengine wanaoishi huko maisha yao hayajapanda?
 
Ndio tabu ukiwa na kiongozi mkenua meno system nzima inaharibika, huyu mama nae.. mh
Katika ukurasa wake kwenye facebook mh Zitto ameandika ya kuwa "Nchi zinazoendelea haziwazi posho kwa viongozi, bali kujiuliza maswali wamefikia hatua gani kuondoa mlindimo wa umaskini na kufanya uchumi wa nchi kuwa imara".
 
Tugome kushiriki maadhimisho ya uhuru, tubaki majumbani mwetu kupinga dhuluma inayotekelezwa na watawala wetu.
 
tbc wamemuonesha pia bibi akitangaza ongezeko hilo,toka elfu 70 mpaka laki mbili ni ongezeko la zaidi ya asilimia 170! Ni sawa na mshahara wa wafanyakazi wengi wa serikali kwa mwezi,mbona vijana udsm waliambiwa serikali haina pesa?

zipo za kulipana maposho wanalipana hadi 3m kwa cku
 
Tugome kushiriki maadhimisho ya uhuru, tubaki majumbani mwetu kupinga dhuluma inayotekelezwa na watawala wetu.
Ntemi K hiyo ijumaa asbh ukitaka karaha pita mitaa ya taifa uone dada zetu na vilemba vya njano wakijishebedua.vijana rijali wakiwa kwenye mafuso kama mihogo..hakika tz hatuishi ujinga!
 
watu wanasikia lakini siku ya kura wanasahau baada ya kuhongwa na pilau bia na kanga
mm nadhani sii bure kuna namna inatumika kama sio uchawi
yaani unajua maendeleo hakuna miaka 50 bado tu unachagua magamba,lol poleni
 
Back
Top Bottom