Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Zitto ameshauri watanzania wawanunie viongozi wanaoshabikia posho akiwemo spika makinda kuonesha kwamba haturidhiki na mtindo wa kujilimbikizia. Wewe unadhani kununa kutawapa ujumbe kwamba watanzania hawawaungi mkono?
Source: Zitto twitter account
Tuwanunie wabunge wote hadi wazikane hizo posho na kuzirudisha na kupitisha zifanye kazi nyingine za jamii. Hivi hizi posho zinaweza kuongezwa bila kupitishwa kwenye budget? Jamani wabunge si ndio wanapitisha budget na hakuna pesa ya serikali inayotumika bila kupitishwa kwenye budget! kwa hiyo ina maana wabunge walipitisha nyongeza ya posho zao kwenye budget iliyopita. Sikusikia hata mbunge mmoja akitoa shilingi ili posho zisipite zikiwa na nyongeza. Spika ametekeleza tu maamuzi ya wabunge wenzake.
Wabunge wa nchi kweli wanatufanya sisi hamnazo kweli!!