Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 44
JANA Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akijibu swali bungeni lililotaka kujua ni lini viongozi wa kiserikali kama rais wataacha kutumia ziara za kiserikali kufanya shughuli za kichama, kama alivyofanya Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni huko Pemba, alisema rais ni mkubwa wake wa kazi na yeye asingeweza kutoa kauli ya kile kinachodaiwa kuwa alikisema, kwa sababu hakuwepo, na hajui ni nini rais alisema, zaidi ya kusoma tu kwenye vyombo vya habari.
Zaidi ya majibu hayo ya Pinda, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, aliingilia kati kumsaidia waziri mkuu na kusema kwamba hakukuwa na haja ya swali hilo kujibiwa, kwani liko wazi.
Kwamba haiwezekani kutenganisha kofia mbili alizonazo rais, yaani ile ya urais na ile ya kuwa mwenyekiti wa chama chake, na kusisitiza kuwa hata katika nchi zilizoendelea sana kama Marekani, rais wao hutumia ndege ya serikali Air Force One kufanya ziara ya kichama.
Kwanza, sisi tunasisitiza tena kuwa si sahihi kwa rais wala kiongozi yeyote wa serikali kutumia ziara za kiserikali ambazo kimsingi zimegharamiwa na kodi za Watanzania wote kutoa hotuba, kauli, kufanya shughuli au jambo lolote kwa masilahi ya chama chake cha siasa.
Si sahihi, kwa sababu mtu anapokuwa kiongozi wa kiserikali, wajibu wake ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali chama chake.
Pili, kiongozi wa kiserikali kufanya shughuli kwa masilahi ya chama chake cha siasa wakati akiwa kwenye ziara ya kiserikali, ni kuruhusu mgongano wa kimasilahi kati ya masilahi ya chama chake na masilahi ya taifa, ambayo ndiyo hasa anayopaswa kuyasimamia wakati huo akiwa kwenye ziara hizo za kiserikali.
Tatu, hatukubaliani na upotoshaji wa Spika Sitta kuwa haiwezekani kwa rais kutenganisha majukumu yake kama rais na kama mwenyekiti wa CCM, kwani sisi tunaamini kuwa inawezekana, kinachotakiwa ni kwa mhusika (Rais Kikwete) kuwa na utashi na utayari wa kutodharau misingi ya utawala bora wala kuwa mwepesi wa kubagua wafuasi wa vyama vingine vya siasa pindi awapo kwenye ziara za kiserikali.
Nne, Rais Kikwete anapaswa kupanga muda wa kufanya ziara za kichama ambao utakuwa ni tofauti na ule wa ziara za kiserikali, na anapaswa kutumia ruzuku ya CCM kwa ziara za kichama, badala ya kudoea usafiri wa kiserikali halafu anakwenda kuzungumzia mambo ya CCM kama alivyofanya Pemba hivi karibuni.
Akiona ni vigumu, basi aache ziara zake za kichama zifanywe na Makamu Mwenyekiti wake, Pius Msekwa, au Katibu Mkuu wake, Yusufu Makamba, pale inapolazimu.
Tano, kauli ya Pinda kuwa hawezi kutoa kauli kuhusu kile alichokisema Rais Kikwete, eti kwa sababu ni mkuu wake wa kazi, ni ya upotoshaji.
Pinda kwa nafasi yake kama Waziri Mkuu, ndiye mtu wa mwisho anayepaswa kujibu au kutoa ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu serikali na maadili ya viongozi wake, akiwemo rais.
Kwanini Pinda anasema hakuwepo na hajui alichokisema rais? Kama vyombo vya habari viliandika uongo kuhusu kile alichokisema Kikwete kule Pemba, serikali iliyo chini ya Pinda kama Waziri Mkuu, ilishindwa vipi kutoa taarifa ya kukanusha kile kilichoripotiwa kupitia mwandishi wake, Salva Rweyemamu?
Kwanini Pinda anaviamini tu vyombo vya habari pale vinaporipoti mambo mazuri ya viongozi lakini haviamini pale vinaporipoti kauli zisizofaa za rais?
Tunautaka umma wa Watanzania uelewe kuwa majibu yaliyotolewa bungeni na viongozi hawa ni ya upotoshaji, ni wajibu wa kila mwananchi kutochoka kuwarudisha kwenye mstari viongozi wetu pale wanapofanya ndivyo sivyo.
Chanzo: Tanzania Daima
Tafakari yangu:
Pongezi kwa mhariri kwa kuwazodoa. Ukweli ni kuwa kikwete alivunja katiba kwa kufanya ubaguzi wa kisiasa, lakini kubwa zaidi ni kuwa amekiuka sheria ya utumishi wa umma ambayo inawataka watumishi wa umma kufanya kazi bila kubagua au kuwanyanyasa wananchi kutokana na tofauti za kivyama kwa kutumia ofisi zao za umma. Sheria inawataka pia kutotumia ofisi za umma kwa manufaa ya vyama vyao. Rais ni mtumishi wa umma, ni wazi kwamba katika ziara hiyo ya Zanzibar ametumia fedha za ofisi ya umma na mikutano ya hadhara iliitishwa kwa kofia yake kama Rais lakini akafika na kuitumia kichama. Hii si mara ya kwanza, mtakumbuka Kikwete na mawaziri wake walipokwenda Kigoma na Rukwa wakafanya uharibifu mwingi kwa kofia ya umma ikiwemo kuwarubuni wenyeviti wa vijijini na vitongoji kutoka CHADEMA. Kwa hiyo Rais akaenda kuzivunja serikali ambazo alipaswa kushirikiana nazo katika ziara hiyo. Halafu Pinda na Sitta wanatetea huo uvunjaji wa sheria na wapinzani bungeni nao wanawaachia tu. Huu mjadala haupaswi kufungwa mpaka kieleweke. Kama executive imeshindwa kuitafsiri na kuheshimu hii sheria. Na legislature kwa maana ya spika na bunge lake wanachekelea tu. Inabidi sasa kupata judicial directives. Wakome kabisa hawa! Ni vizuri Tanzania tukaheshimu maadili ya siasa za vyama vingi na utawala wa sheria.
Asha