Spika Sitta na Usiri wa Mikataba na majibu ya serikali

Invincible,
Mkuu nakubali maneno yako lakini hata hivyo ni lini kiongozi wa Tanzania amekuwa na mawazo tofauti na Malima.. labda wakati wa Nyerere!..
Nina hakika Mwinyi au Mkapa ndio waanzilishi wa fikra hizi..mikataba haikuanza kusainiwa wakati wa Kikwete..
Shina hili la Ufisadi na Ulimbukeni limeanzia mbali sana..
 
...ndumilakuwili, tofauti ya mbunge anapokuwa back bencher na anapokuwa kwenye cabinet.

No hope at all!
 
Cha msingi Malima asingetumia muda mwingi kuongea mambo yasiyokuwa ya msingi, Usiri wa mikataba ni hatari sana tena sana na hili halihitaji hata kwenda shule ndo ulijue.Inasikitisha sana kuona rasilimali tulizonazo lakini bado tunalia umasikini kila siku huu ni ujinga na upumbavu mkubwa sana.Tembelea migodini uone maexpertise waliopo utacheka na kugundua ni jinsi gani tulivyo wajinga.Inabidi na lazima mikataba iwekwe wazi na wizara ya kazi na maendeleo ya kazi lazima ijue na iwe inafanya auditing migodini kujua kama ratio ya maexpertise inazingatia ambayo ni atleast 1:6.
Hivi huu ujinga wetu utaisha lini jamani?
 
This is interesting!

Serikali kuu ya Tanzania inasema kuwa mhimili mmoja wa Serikali Bunge haina uwezo kupitia mikataba! Spika wa Bunge anaonekana kana kwamba anatoa rai (ombi) kuwa mikataba iwe wazi badala ya kutumia turufu ya mamlaka ya Bunge!

Serikali kuu inajibu mapigo na kusema kuweka mikataba wazi ni kuharibu ushindani!

Sasa najiuliza, tangu lini mkataba wa biashara ukawa siri kuogopa ushindani

Labda nitumie mfano hai uliotokea huku Marekani.

Benki yangu Wells Fargo na hata ile ya J.P. Morgan Chase, zimenunua benki nyingine ambazo zilikuwa zikisuasua.

Wells Fargo imempiku Citibank na kutoa dau kubwa zaidi na kujitwalia Wachovia. Bei ya manunuzi, mkataba mzima na vikolombwezo kibao havikuwa siri. Ni wazi kwa umma kujua, wana hisa na zaidi ni kwa zile mamlaka husika kama Wizara ya Sheria, Wizara ya fedha, SEC, IRS, FDIC, Bunge na kwa kurudia Serikali za Mikoa na Kuu.

Sasa inakuwaje Tanzania Mahakama na Bunge zinaweza kukataliwa kupitia mikataba na Waziri kwa kutumia kifua cha Serikali Kuu au kumlinda mwekezaji huku Mtanzania anayemlinda Mahakama na Bunge wanaambiwa eti hawana ubavu?

Nimuulize Augustoon wakili wetu, je kuna Sheria gani inayozuia Bunge na Mahakama au mwananchi mwenye kuonelea kuwa mkataba si kwa manufaa ya upande wetu kama inji? Je ni mamlaka gani yaliyo na nguvu kiasi hicho kuwa Waziri akiamua hakuna wa kusema?

Yona na Mramba wamefikishwa mahakamani kwa ajili ya kutumia "vizuri" madaraka yao. Walipopewa ushauri na TRA na taasisi nyingine walitumia madaraka yao kwa mujibu wa sheria (gani sijui) na kutoa mkataba kwa Alex Stewart na kuchapisha maamuzi yao kwenye Gazeti la Serikali.

Karamagi alipokimbilia Churchil Motell kuweka sahihi mkataba, alifanya kuwa ni siri na hata kudai kuwa Taifa (Watu, Bunge, Mahakama) kwa ajili ya kumliinda mwekezaji, halina mamlaka ubavu na lisithubutu.

Sasa naona Malima anaongea kitu kile kile, je kwa yaliyotokea na kuna Yona na Mramba, hatuoni kuwa kuna haja ya kuondokana na Sheria au Kanuni butu ambazo zinaishia kutumiwa vibaya na waliopewa madaraka?

Je leo TRA, TBS na Polisi(Takukuru pia) wakitaka kwenda kufanya uchunguzi Barrick na hata kupitia mkataba ili ama kuelewa ni vipi Barick wanakwepa kodi, wanachuja kiwango cha dhahabu au wanaharibu mazingira na barrick wakasema kwa walipewa ruhusa kwa mujibu wa mkataba, TRA, TBS na wengine watafanyaje kazi zao kumlinda Mtanzania huku Waziri kaficha mkataba nyumba ndogo na anasema ni "marufuk"(sic)?

Hapa ndipo tunapoona ubaya wa Executive Powers na priviledges ambazo huishia kuwa abuse of power na kutoa image ya corruption and uhujumu(Ufisadi)!
 
Kwa kuwa namuamini Zitto nitachukulia kauli yake kuwa kweli na nakubaliana na wale wanaosema amebadirika.
Na mimi natakiwa nibadirike.
 
Date::12/6/2008
Zitto amshutumu Waziri Malima kwa kumpinga Spika

Na Paulina David, Mwanza
Mwananchi

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, amesema kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adamu Malima, hakupaswa kutoa kauli ya kumpinga Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samwel Sitta, kuhusu uwazi kwenye mikataba ya madini.

Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alitoa kauli hiyo jana kwenye Viwanja vya Sahara, wakati akihutubia wananchi wa Jiji la Mwanza kwenye Operation Sangara.

Alisema Malima hakupaswa kumjibu wala kumpiga Spika Sitta kuhusu mikataba ya madini kuwekwa wazi na kupelekwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge, kwa sababu inahusu rasimali ya taifa.

Alisema kauli ya Malima juu ya mikataba hiyo kuhusiana na mambo ya biashara haina mantiki yoyote, kwa sababu wawekezaji wanaokuja kuwekeza wanawekeza kwenye ardhi ya Watanzania na wanachochuma ni rasilimali ya yao, hivyo wanapaswa kuijua mikataba inayotiwa saini na Serikali.

Zitto alisema Malima hakupaswa kumjibu Spika kutokana na umri wake na nafasi ya uspika aliyonayo katika nchi hii na kusisitiza kwamba, kwa kauli yake ameonyesha kushindwa kumheshimu spika na muhimili muhimu nchini.

"Spika anaongoza wabunge zaidi ya 360 na bunge ndicho chombo cha kutunga sheria na kuisimamia serikali, hivyo kauli ya Wziri Malima inaonyesha jinsi asivyoli liheshimu bunge ambalo ni muhimili muhimu katika nchi hii,' alisema na kuongeza:

"Hivi Malima ni nani katika nchi hii ambaye anaweza kupingana na kauli ya Spika ya kutaka mikataba ya madini inayotiwa saini na serikali kufanywa kwa uwazi na kupelekwa bungeni. Hivi jeuri hiyo ya kumjibu Spika ameitoa wapi?"

Alisema kuwa yeye binafsi anakubaliana na kazi kubwa inayofanywa na spika na anaiunga mkono, kwa sababu ameleta mabadiliko makubwa katika bunge hadi kufikia hatua ya Waziri Mkuu wa nchi kujiuzulu kutokana na kutowajibika.

Alisema kutokana na hali hiyo ni lazima suala la mikataba ya madini lifanyike kwa uwazi kwa sababu ni mali ya Watanzania, hivyo hakuna sababu ya kufanywa kwa siri.

Aidha, Zitto alisema kuwa inasikitisha kuona walimu wanalalamikia serikali kwa kushindwa kuwalipa madai mbalimbali yakiwemo malimbikizo ya mishahara, huku serikali ikisamahe mabilioni ya fedha kwa wawekezaji wanaomiliki kampuni mbalimbali za madini hapa nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo, ni wazi kuwa serikali imeshindwa kusimamia ipasavyo rasilimali za nchi na kuwafanya watu kutoka nje kunufaika na utajiri wa nchi wakati Watanzania wakiendelea kuwa masikini.

"Ndugu zangu hakuna mtu anayekataa wawekezaji hata mimi nawakubali, lakini ambao hawalipi kodi na ambao wanaochukua rasilimali zetu bila ya taifa kupata chochote hawana faida kwetu na hakuna sababu ya nchi kuwa na wawekezaji wa aina hii," alisema Zitto.
 
Ndugu zangu hakuna mtu anayekataa wawekezaji hata mimi nawakubali, lakini ambao hawalipi kodi na ambao wanaochukua rasilimali zetu bila ya taifa kupata chochote hawanafaida kwetu na hakuna sababu ya nchi kuwa na wawekezaji wa aina hii," alisema Zitto.

Yah kwa misingi hiyo iwe wazi tujue kama inafaida au haina faida kwetu maana tuliowaamini wemekuwa wanatufanyia mambo ya ajabu kwa kuwa wao wanapata cha kupewa.
Sasa tuenda sambamba na tuta panda na kushuka pamoja kama taifa.
 
Mikataba ikiwa wazi, ushindani wa wawekezaji si utaongezeka? sisi itakuwa ni kuchagua waliobora zaidi, vile vile itaepusha rushwa kwa wale wawekezaji ambao hawana mvuto wanataka kupitia mlango wa nyuma.

Kama waziri hatumii common sense kama hii, nadhani inapaswa pia Kikwete kuwajibika au kuwawajibisha pindi wanapotoa comment za ajabu ajabu kama hizi,

wahenga walisema afadhali ukikaa kimya hutaweza julikana kama mjinga , una busara au la...

kama faida au uwajibikaji wa mawaziri au viongozi wa nchi ni aina ya malima wanaowaza kula,kuvaa, kutembelea magari mazuri ya kifahari kutibiwa nje na kujipendekeza kwa wawekezaji NAONA HAWANA TOFAUTI mbwa wa kizungu anayetunzwa vizuri, ambaye anapata kila kitu ikiwemo chakula bora zaidi ya Malima. MALIMA au kiongozi yeyote anatakiwa awe tofauti na mnachofanya sasa. mkiwa wabunifu,wawajibikaji , wenye kujali maslahi ya taifa ndiyo mtaleta tofauti kati yenu na mbwa wa kizungu.

waberoya
 
Zitto,
"Spika anaongoza wabunge zaidi ya 360 na bunge ndicho chombo cha kutunga sheria na kuisimamia serikali, hivyo kauli ya Wziri Malima inaonyesha jinsi asivyoli liheshimu bunge ambalo ni muhimili muhimu katika nchi hii,' alisema na kuongeza:

"Hivi Malima ni nani katika nchi hii ambaye anaweza kupingana na kauli ya Spika ya kutaka mikataba ya madini inayotiwa saini na serikali kufanywa kwa uwazi na kupelekwa bungeni. Hivi jeuri hiyo ya kumjibu Spika ameitoa wapi

Hapa mkuu wangu chukua zote sijui 10 au zaidi... duh yes yaani umeongea maneno mazito sana ambayo yatamfanya afikirie mara mbili..
Huyu jamaa ni sawa na Prosecutor anayefanya jeuri mbele ya Jaji mahakamani utafikiria sheria kazitunga yeye..
Ama kweli Kikwete ana wakati mgumu sana na hawa mawaziri wake uchwara maanake kila anyemweka ni Kabuntas...how come?
Sasa naanza kukubali maneno ya Invincible!
 
Mikataba ikiwa wazi, ushindani wa wawekezaji si utaongezeka? sisi itakuwa ni kuchagua waliobora zaidi, vile vile itaepusha rushwa kwa wale wawekezaji ambao hawana mvuto wanataka kupitia mlango wa nyuma.

Kama waziri hatumii common sense kama hii, nadhani inapaswa pia Kikwete kuwajibika au kuwawajibisha pindi wanapotoa comment za ajabu ajabu kama hizi,

wahenga walisema afadhali ukikaa kimya hutaweza julikana kama mjinga , una busara au la...

kama faida au uwajibikaji wa mawaziri au viongozi wa nchi ni aina ya malima wanaowaza kula,kuvaa, kutembelea magari mazuri ya kifahari kutibiwa nje na kujipendekeza kwa wawekezaji NAONA HAWANA TOFAUTI mbwa wa kizungu anayetunzwa vizuri, ambaye anapata kila kitu ikiwemo chakula bora zaidi ya Malima. MALIMA au kiongozi yeyote anatakiwa awe tofauti na mnachofanya sasa. mkiwa wabunifu,wawajibikaji , wenye kujali maslahi ya taifa ndiyo mtaleta tofauti kati yenu na mbwa wa kizungu.

waberoya


kweli kabisa hawa ni kama mbwa tu maana hata mbwa kiwaja ana pewa chakula bora na kikubwa daktari wake .Sasa hawa kwa watu wanao saini nao mikataba ya kusaliti nchi zao na wao kupewa kidogo kitu wanaonekana kama mbwa tu kwao tena zaidi ya hilo ni wanaonekana ni ma Traitor.Na traitor hasathaminiwi zaidi ya kutumiwa tu na kutoaminia .
 
Kama ni swala la ushindani, hata sisi tunatakiwa kuwashindanisha wawekezaji, ili kupata mwekezaji ambao anamaufaa zaidi. Kuweka mikataba wazi baada ya kusainiwa haina manufaa sana. Bali serikali inatakiwa itoe taarifa kwa umma "Public notice" ya kusudio la kuingi mkataba na mwekezaji fulani na vipengele vyote muhimu vya makubaliono viwekwe wazi ili wananchi watoe maoni yao. Hii pia itatoa mwanya kwa wawekezaji wengine ambao watakuwa tayari kuwekeza kwa vigezo bora zaidi kujitokeza. Ushindani ni double edged sword. Siyo kwa upande wa wawekezeja tu.

Pia ni vyema hii sheria ya kutangaza kusudio la kuingia mkataba na wafanyabiashara iwe kwa mikataba yote hata ya ununuzi wa huduma na bidhaa mbali mbali.
 
tatizo kubwa la watawala wetu (mawaziri na wengine) huwa hawako kwa ajili ya wananchi waliowafanya kuwa mawaziri na wabunge bali wapo kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na familia zao na wawekezaji ndio maana sio rahisi kwa waziri kuwa na ufahamu wa wananchi na mali zao.
bila hii hali kubadilika kina Maliamwataendelea kuwa wengi sana.
Wajinga sio wajinga, zezeta sio zezeta, inafikia mahali hata uelewi jibu limetolewa na mtu mwenye akili timamu au la.

Wamesha fanya mikataba mingi sana na matumbo yao , sasa tunataka nasi tujue hiyo mikataba inatufaa au tunaliwa.
 
Ujinga mwingine kutoka kwa mawaziri wetu vijana walio lewa madaraka. Tulisoma ya Mengi Vs. Mh Masha, sasa Mh Malima Vs. Mh Sitta.

Kumbukeni hawa ndio damu mpya hivyo mimi nilitegemea wawe wanajua hali ya halisi ya nchi. Yes, nina jibu, vijana wengi walio lelewa katika mazingira ya Masha na Malima hawajui hali halisi ya Tanzania, wote wawili wamekaa sana nje ya nchi hii hivyo wamepoteza maadili ya kitanzania.

Tuwe macho na kizazi cha mtindo huu vinginevyo huko mbele tutakuwa na matatizo sana na viongozi wa mtindo huu.
 
Njimba Nsalilwe,
Yes, nina jibu, vijana wengi walio lelewa katika mazingira ya Masha na Malima hawajui hali halisi ya Tanzania, wote wawili wamekaa sana nje ya nchi hii hivyo wamepoteza maadili ya kitanzania.
Mkuu sio kweli kabisa maneno yako kwa sababu wengi wachangiaji JF wameishi nje muda mrefu na ndio wao walitu amsha Wadanganyika. Miaka yote tulikuwa tukiburuzwa tu ndani ya kiza na hawa Waheshimiwa!
Kifupi huyo Masha na Malima wanafanya kama vichaa wengine waliolazwa hospital ya vichaa..
 

MHE. ZITTO Z. KABWE (December 5th, 2008):

"Spika anaongoza wabunge zaidi ya 360 na bunge ndicho chombo cha kutunga sheria na kuisimamia serikali, hivyo kauli ya Wziri Malima inaonyesha jinsi asivyoli liheshimu bunge ambalo ni muhimili muhimu katika nchi hii,' alisema na kuongeza:

"Hivi Malima ni nani katika nchi hii ambaye anaweza kupingana na kauli ya Spika ya kutaka mikataba ya madini inayotiwa saini na serikali kufanywa kwa uwazi na kupelekwa bungeni. Hivi jeuri hiyo ya kumjibu Spika ameitoa wapi?"

Mzizi wa fitina kati ya Zitto na Malima haujakatika, ulianza zamani:


MHE. ADAM K. A. MALIMA (August 14, 2007, kesi ya Zitto Bungeni):

...Mheshimiwa Spika, lakini tunachosema, umesema wewe imeathiri heshima ya Bunge. Sasa umenitangulia kidogo, lakini mimi nilitaka kusema wale wanaokwenda mbali huko Italy na Japan na Israel, Kenya tu hapa! Walikuja Wabunge wa Kenya kwenye Kamati ya Fedha wiki iliyopita, wamekaa kule juu. Tulivyokutana nao Dodoma Hotel jioni yake, wanasema your Parliament is very civilized, Wabunge wa Kenya tu hapo! Sasa sisi tunachosema ni kwamba ile civilized nature ya Parliament yetu inatokana na kuheshimiana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kaka yangu Waziri Mkuu anajua, katika watu wanaoihoji Serikali wanapopata nafasi, mimi ndiye ninakuwa wa kwanza. Lakini ukitaka kuihoji Serikali, uihoji kwa taratibu na nidhamu ambazo sisi katika Bunge hili tumejiwekea. Suala linaloingia hapa siyo kuihoji Serikali, suala linaloingia hapa ni kumvunjia heshima Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tunajiuliza je, yale maneno ya kumwambia
amelidanganya, amelipotosha na yeye ni Waziri, ana nafasi yake. Kwa hiyo, na magazeti yakalichukulia hapo na watu wengine na kusema kweli mimi naungana na Mheshimiwa Mudhihir Mudhihir anaposema kwamba Mheshimiwa Waziri amedhalilishwa na kauli hiyo na baada ya kudhalilishwa Mheshimiwa Waziri kwa nafasi yake na kwa kauli yake
kwa kuwa ameisema Bungeni, kumtuhumu kwamba amesema maneno yale ndani ya Bunge ni kulivunjia heshima Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nakubaliana na adhabu ya Mheshimiwa Mudhihir Mudhihir na naomba isiwe hiyo tu, kuna mwingine amenong'ona viwe vikao vinne.

Mheshimiwa Spika, lakini mimi ni katika watu ambao tutaathirika na kutokuwepo kwake kwa sababu tunamhitaji sana kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi. Lakini hatuhitaji watu ndani ya Bunge hili ambao watakuwa hawana nidhamu kiasi cha namna hii.

Mheshimiwa Spika, naomba niunge mkono hoja ya kaka yangu Mheshimiwa Mudhihir Mudhihir. Ahsante sana. (Makofi)
 
Halisi,
Mzizi wa fitina kati ya Zitto na Malima haujakatika, ulianza zamani:
Mkuu samahani, mimi sidhani kama kuna mzizi wa Fitna isipokuwa huyu jamaa Malima anabwabwaja ovyo utadhani hakwenda shule...
Rudia kusoma maelezo yake vizuri (uliyobandika) utaona kwamba hata Bungeni huyu mtwana anaona hoja hazifai kwenda ikiwa malalamiko yanamhusu waziri, ni kumwaibisha! then wapi hoja nzito za kitaifa kama mikataba zinatakiwa kupelekwa!..
kama kuna Fitna basi hiyo Fitna sidhani kama ipo upande wa Zitto kwa maelezo yake hapo juu isipokuwa amezungumza maneno yanayopimika hakuna pumba kama Malima..
 
Nashiwishika kuona umuhimu wa kile wanachofanya wanamgambo wa Nigeria kurudisha raslimali ya mafuta inayoibwa na makampuni makubwa kwa mgongo wa wanasiasa. Nilitegemea suala la usiri wa Mikataba liongelewe/litetewe na makampuni yanayowekeza kwenye madini. Anachofanya N/Waziri wetu ni sawa na kuajiri mtu akusaidie kuingia mkataba wa mali yako kisha akatae usione mkataba, tena kwa jazba na majivuno kwamba ukiuona utatoa siri ya mkataba!!!!! Huu ni upuuzi ambao tumekuwa tunaufumbua macho na sasa huyu kilaza anamwaga pilipili kwenye kidonda kibichi.

Haiingii akilini kama mwajiriwa wa namna hii hana maslahi ya pembeni tofauti na yale mwajiri wake anayoyafahamu, hapa lazima kuna kitu kinafichwa!!! Wito kwa wananchi, wanasiasa na vyombo vya habari kumuuliza huyu mtu nani kamwajiri mpaka aseme mikataba dhidi ya raslimali ya wananchi inakuwa siri kwa waajiri wake? Au anamaana ukichaguliwa kuwa Naibu waziri basi unakuwa si mwananchi wa Tanzania bali msemaji wa wawekezaji? Tumechoka kwa kweli!!!
 
Pole yake JK,Pole kwa watanzania wote na Pole kwa wote walioko Mkuranga,Huyu Malima kung'ang'ania kuwa mikataba ni siri nafikiri alifundishwa na baba yake marehemu hivyo akili zake pia ni marehemu na tumsamehe na kumpa haki yake wakati utakapofika
 
Toka lini mtoto wa NYOKA akaitwa SAMAKI?? Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Kitendawili......tega, Baba Kighoma alikuwa fisadi.........................
 
Ujinga mwingine kutoka kwa mawaziri wetu vijana walio lewa madaraka. Tulisoma ya Mengi Vs. Mh Masha, sasa Mh Malima Vs. Mh Sitta.

Kumbukeni hawa ndio damu mpya hivyo mimi nilitegemea wawe wanajua hali ya halisi ya nchi. Yes, nina jibu, vijana wengi walio lelewa katika mazingira ya Masha na Malima hawajui hali halisi ya Tanzania, wote wawili wamekaa sana nje ya nchi hii hivyo wamepoteza maadili ya kitanzania.

Tuwe macho na kizazi cha mtindo huu vinginevyo huko mbele tutakuwa na matatizo sana na viongozi wa mtindo huu.

Inasikitisha kijana kuboranga tena msomi.
Ila swala la kukaa nje , sidhani kama ni tatizo hawa jamaa wamekaa nje lakini hawakujifunza ustaarabu wa demokrasia wa nchi zilizokomaa na viongozi kuwajibika kwa maneno na matendo yao, nje waliokaa si jui ni ipi ama ni wale walikuja kusoma na kukaa mabwenini kisha kurudi nyumbani.
Wasomi na vijana hawa ni chukizo na si mfano wa vijana wa dunia ya sasa. Si wakuigwa wala wa kufuata kwani ni vigumu sana kwao kuendelea mbele kulitumikia taifa, wameshindwa kusoma hata ishara za nyakati. na dhani wote wanafedha za ufisadi hivyo hawajali yakesho.

Hili ni tatizo la viongozi wanaoingia madarakani na fedha ya wachache , hivyo hawajali ya wengi bali wanajali mabwana zao waliowapa fedha za kushinda ubunge. kazi ipo.....
 
Back
Top Bottom