Spika: Milipuko ya mabomu Gongo la Mboto sio jambo la dharura!

Mh ! Spika tunaye

Lazima aseme hivyo kutokana na ukweli kuwa tatizo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara hivyo nahisi ameona ni jambo la kawaida !!!! Nadhani huyu mama anahitaji maombi ili mungu ampe hekima maana kazi/nafasi aliyonayo inahitaji hekima na busara za hali ya juu vinginevyo atakuwa anatoa matamshi/maamuzi ambayo hayaeleweki kwa jamii.
 
Sikuwahi kusikia ameolewa huyu Mama ingawa ana watoto. Ni mbabe kuliko hata Anna Abdallah. Amejiunga na wale wanaoibomoa CCM unconsciously.

kaka usimpe sifa ya bure - huyu mama si Mbabe bali ni mbumbumbu amewekwa hapo ili kupangua hoja zote zinazokandamiza serikali nani asiyejua mchezo uliyofanyika ndani ya CCM hadi akapatikana?

akiendelea na mchezo wake wa kupangua hoja muhimu atawekwa na yeye kwenye kundi la kutetea mafisadi kwa hiyo akubali zomea zomea mtaani ha hata akienda kanisani kwake tunamsuburi mlangoni akitoka tu tunaanza kunamzomea. hii miaka mitano ya uspika wake ataiona karne kwa style hii ya uongozi.

Tunaoma ajirekebishe haraka, sisi watanzania si wale wa mwaka 47, tunaelewa na tunafuatilia hoja za msingi.
 
huyu mama mhhhhh...........tatizo kabisa. Let me count and speculate

Mbagala ilipuke
Mgulani (opposite chuao cha uhasibu) ilipuke-though sidhani kama kuna silaha pale
Navy kigamboni ilipuke
Ubungo kibangu ilipuke - Juzi gongo la mboto ilivyolipuka wanajeshi wa kibangu walipakia familia zao na kutoweka kambini
Lugalo ilipuke
Changanyikeni ilipuke
Gongo la mboto ilipuke
Kazi mzumbwi kisarawe ilipuke
kibamba/kiluvya nayo iitike.

Huyu mama haoni wakati umefika jambo hili kuangaliwa upya na ikiwezekana kuhamisha baadhi ya kambi za jeshi maana zimekaribiana sana na makazi ya watu yameongezeka?

Mkuu nimeambiwa ikilipuka NGERENGERE ndo itakuwa mwisho wa uhai ktk mkoa wake
 
Kwa kauli hiyo, hafai kuwa Speaker, na hana budi kujiuzulu sawia kwa manufaa ya umma!
 
Define Dharura katika bunge.

Dharura ktk bunge ni pale mtoto wake supika akifariki ambapo vikao vya bunge vita ahairishwa kwa siku 3 kuomboleza kifo cha mtoto wa supika
 
Mwanakijiji na wewe unataka uitwe redio mbao na mkuu wa nchi yako?? Unadhani kuna ugaidi Tanzania?? Unadhani Mkuu anafikiri kama wewe unavyofikiri??

Ugaidi upo. Tatizo tu ni kuwa waliofanya ugaidi sio magaidi a.k.a waislamu kama terrorist act 2002 inavyosema.
Ugaidi huu ni wa lile Jeshi lililo ndani ya jeshi ambalo Serikali haijatolea ufafanuzi uwepo wake kama waraka wa waislamu ulivysema hapahapa JF.
 
Dharura ktk bunge ni pale mtoto wake supika akifariki ambapo vikao vya bunge vita ahairishwa kwa siku 3 kuomboleza kifo cha mtoto wa supika

Niongeze hapo juu kidogo kwenye tafsiri ya dharura....na sio watanzania karibu 200 wanapokufa vifo vilivyosababishwa na uzembe usiomithilika wa serikali ya kifisadi ya ccm isiyojali wala kuthamini maisha ya walalahoi walioiweka madarakani kwa kura zao walizouza kwa bei ya khanga, tshirt na pilau.

Kwangu, mimi mgao wa umeme, milipuko ya kijinga ya mabomu, mifumuko ya bei isiyo na kichwa wala miguu, zero za kumwaga za form iv, akina mama kujifungulia sakafuni n.k n.k si matatizo bali ni dalili/ishara (symptoms) za tatizo tulilonalo. Tatizo letu ni ukosefu wa serikali makini ambayo ni matokeo ya ukosefu wa rais makini kwa kuwa serikali inaundwa na rais period.
 
Kamanda lisu usiwe na wasiwasi kwani, nimekuja kuangalia hili jambo kwa makini nimegundua spika yupo sawa kwani hili jambo siyo la dharura, kwa sababu alikuwa analifahamu litatokea, anatakiwa abanwe awaeleze watanzania kwa nini hakutoa tahadhari kwa raia wanaoishi eneo hilola gongo la mboto, huku akijua mapomu yangelipuka juzi? .Na alieleze bunge taarifa hizi alizipata wapi?AKISHINDWA AJIUZULU MARA MOJA Kwani dharura nia jambo amabalo linaotkea pasipo kutegemewa. Sasa huyu mama amesema hili siiiiiiiiiiii la daharura kwa sababu alitegemea litatokea na ndiyo maana amemwambia lisu halina haja ya kulujadili KWA SABABU SI JAMBO LA DHARURA KWAKWE. Lakini kwetu siss wananchi ni ladharura kwani hatukujua kama lipo, au laja, au kuna lingine. Huyu ni killlllllllllllllllllllllllaza
 
Huyo mama kiazi kweli.......muone sura kavu kaa ndimu...yangetokea ikulu yaha tungeona jinsi ambavyo wangehaha...kwasababu limetokea kwa mtanzania maskini..ni poa tu
 
jamani kwa sababu za kiusalama si sahihi kujadili hili suala bungeni,kuna siri zaweza wekwa wazi wakati wa kujibu ambazo hazipaswi kuwa wazi,si kila kitu kinajadiliwa ovyo nyie watu,lazima wafanye uchunguzi na waweke mambo sawa kwanza(hata kama lilipangwa kuna namna ya kuwasilisha jambo kwa umma na international community inachukua muda).....heeeeeee,kuna haja ya watu kusoma somo la Usalama wa nchi......yaani hamna tofauti na Kikwete ambaye jana karopoka kuwa lile lilikuwa hiyo kati ya maghala makubwa,kwa usalama wa nchi ile si sahihi na hata wakuu wameshamwambia amechemka,leo mnataka lijadiliwe bungeni???mnafikiri nyie zaidi ya ushabiki wa vyama na chuki kwa huyu mama???
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom