Spika: Milipuko ya mabomu Gongo la Mboto sio jambo la dharura!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Spika wa bunge Anne Makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi Gongo la Mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura.

Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.
 
Spika wa bunge anne makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi gongo la mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura. Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani tundu lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

Kwa hiyo wanaona raha watu kupoteza maisha, viungo, mali na makazi.
 
Spika wa bunge anne makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi gongo la mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura. Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani tundu lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

Well,

Kwa sisi wenye akili timamu, tunafahamu kuwa "this was part of the plan"

Mtakuja kufahamu baada kwanini baadhi ya vifaa vipya vya kijeshi navyo pia viliteketea!!!
 
Hii yote ni kwa sababu Watanzania kufa ni jambo la kawaida (life is cheap Tanzania)...huenda Spika amejiuliza nini cha ajabu, ajali za barabarani zinaua makumi kila kukicha...!!!
 
Kama angekufa Fisadi Kikwete na au familia yoyote ya CCM ungesikia wanajadili. Huyu Mama nilishasema kuwa anahitaji mtu wa kumshughulikia mpaka akili zake zika sawa
 
Spika wa bunge anne makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi gongo la mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura. Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani tundu lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

Nimemsikiliza kwa makini sana, nilichogundua ni kuwa kwa sasa Bunge letu linafanya kazi kama idara ya serikali na si mhimili unaojitegemea. Anasema siyo dharura lakini shughuli zote za Bunge zilizokuwa zifanyike jana na leo hazipo na Bunge litaahirishwa baada ya kipindi cha maswali na majibu. Kwa ujumla mbali na kuunda kamati mbalimbali sidhani kama kikao hiki cha Bunge kimejadili jambo lolote lenye maslahi kwa Taifa
 
Sikuwahi kusikia ameolewa huyu Mama ingawa ana watoto. Ni mbabe kuliko hata Anna Abdallah. Amejiunga na wale wanaoibomoa CCM unconsciously.
 
Sijui dharura kwa huyu mama aliepewa uspika kiufisadi ni nini?!! lakini pia nawalaumu/ tujilaumu sisi wenyewe Watanzania hatuwezi kuwafanya viongozi watuogope na kutekelza majukumu yao kwetu wao wanaogopa mafisadi na sio sisi wenye nchi!!

Kama ingekua nchi ingine tungemfukuza huyu mama kwenye uspika maana hafai, kwa kuandamana mpaka atoke na waziri wa ulinzi na pia mkuu wa majeshi.
 
Spika wa bunge anne makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi gongo la mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura. Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani tundu lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

.....the truth will remain firms, now and forever!!! We don't have a speaker but rather a puppet!!! mropokaji mashuhuri!!!!
 
Sasa,

Kama vifo vya watu wote hao siyo dharura, ipi hasa wao wanaono inaweza kuitwa dharura. Tatizo hapa wala siyo hoja yenyewe. mnashangaa nini supika kuikataa hoja hii. TATIZO ni kuwa aliyeitoa ni wa chadema basi. Kwa sababu kwa jinsi bunge linavyoendeshwa safari hii, ni kwamba hoja yoyote ya upinzani kwa maana ya Chadema haiwezi kupewa uzito.

Hoja hii ingetolewa na mbunge wa ccm nina uhakika asilimia 100 ingejadiliwa. Lakini wako tayari kuunda tume nyingine wakati hata ile ya Mbagala mapendekezo yake hayajatolewa. Kama yalishatolewa nani anayajua. Atuambie.
 
Spika wa bunge anne makinda amesema hajaridhika kwamba suala la milipuko ya mabomu iliyotokea juzi gongo la mboto ni la dharura na lina maslahi kwa umma na kwamba halihitaji kujadiliwa kama jambo la dharura. Spika amesema hayo kufuatia hoja iliyotolewa na mnadhimu wa kambi ya upinzani tundu lissu aliyetaka kanuni itenguliwe ili jambo hilo lijadiliwe bungeni.

huyu mama mhhhhh...........tatizo kabisa. Let me count and speculate

Mbagala ilipuke
Mgulani (opposite chuao cha uhasibu) ilipuke-though sidhani kama kuna silaha pale
Navy kigamboni ilipuke
Ubungo kibangu ilipuke - Juzi gongo la mboto ilivyolipuka wanajeshi wa kibangu walipakia familia zao na kutoweka kambini
Lugalo ilipuke
Changanyikeni ilipuke
Gongo la mboto ilipuke
Kazi mzumbwi kisarawe ilipuke
kibamba/kiluvya nayo iitike.

Huyu mama haoni wakati umefika jambo hili kuangaliwa upya na ikiwezekana kuhamisha baadhi ya kambi za jeshi maana zimekaribiana sana na makazi ya watu yameongezeka?
 
katika hili nakubaliana naye; siyo jambo la dharura. hivi wanajuaje kuwa siyo ughaidi?

hili swali linapaswa kuelekezwa kwa mkuu wa nidhamu wa jeshi, si kwa waziri wala mtu mwingine. akishindwa kulijibu, aliyemweka pale ambaye ni Rais anatakiwa amwajibishe.bahati mbaya Rais hawezi kumwajibisha, ni swahiba na rafiki wake wa miaka mingi!!
 
Back
Top Bottom