Spika Makinda Press Conference Live!.

[/SIZE]

Nami nashangaa kama kweli hili ni jambo la kujadili. Sheria inakitaja chama na siyo muungano wa vyama. Hata kama hao wengine wataungana, hiyo haitatambulika. Tunataka chama chenye viti vingi bungeni. FINITO.

Kanuni za kudumu za Bunge, toleo la 2007:

14.-(1) Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atachaguliwa
chini ya utaratibu ulioainishwa kwenye fasili za Kanuni hii
zinazofuata.
(2) Wabunge wote wa Upinzani wanaweza kuunda Kambi Rasmi
ya Upinzani iwapo idadi yao itakuwa si chini ya asilimia kumi na
mbili na nusu ya Wabunge wote.
(3) Chama cha Upinzani hakitakuwa na haki ya kuchagua
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, isipokuwa tu kama kina idadi ya
Wabunge wasiopungua asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge
wote.

(4) Endapo kutakuwa na Vyama vya Upinzani zaidi ya kimoja
ambavyo kila kimoja kina Wabunge asilimia kumi na mbili na nusu
au zaidi, basi Chama chenye idadi kubwa zaidi ya Wabunge kuliko
vingine ndicho kitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni,
lakini, ikiwa kutakuwa na vyama viwili
au zaidi vyenye idadi sawa ya Wabunge ambao ni zaidi ya asilimia
kumi na mbili na nusu, Wabunge wa vyama vinavyohusika
watachagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni chini ya utaratibu
watakaokubaliana wenyewe.

Sitaki kuamini kuwa Spika mpya anabisha kuwa CHADEMA hawastahili kuwa official opposition.

Kama anabisha kuhusu kiongozi wa upinzani hilo nalo ni kosa la wazi,
Siku moja makosa mawili, mwaka mmoja siku 365, miaka mitano siku 1865, siku 1865 Makosa 3650. Tutafika kweli???

Mbombo ngafu.
 
Nina wasiwasi kama ataweza kukabiliana vilivyo na changamoto za wabunge wa sasa bila kuadhiriwa na mawazo na matakwa ya chama chake
 
[/SIZE]

Nami nashangaa kama kweli hili ni jambo la kujadili. Sheria inakitaja chama na siyo muungano wa vyama. Hata kama hao wengine wataungana, hiyo haitatambulika. Tunataka chama chenye viti vingi bungeni. FINITO.

Sheria ipi hiyo?
 
Punguza huruma.
Kumbuka hata Idd Amin na Adolf Hitler walikuwa na familia zao. Vipi Sadam Hussein?


Well my brother Huwezi ukamlinganisha saadam hussein au Idi Amini na Anna Makinda....Anna Makinda hajamfanyia mtu yeyote kile kitu kibaya hadi mtu atokee kuanza kumtukana hivyo....Angekuwa amefanya what Iddi Amini,Hitler au Saadam hussein walivyofanya then mtu angekuwa na haki ya kufanya anachofanya yeye kuwa spika wa Bunge ndiyo inaleta chuki binafsi?....Kuna vitu vingi vya kujadili mtu anatoka from no where na kuanza kurusha maneno ya kashfa that is an acceptable.
 
mremamakinda.jpg



Chama Cha Majambazi kinatia aibu, hivi huyu spika kweli amechaguliwa kuona bunge linafanya kazi yake sawa sawa au ndio ameletwa kuona maslahi ya mafisadi yanaendelea kulindwa kwa nguvu zote? Is this the best CCM can come with? Wizi wote waliofanya bado wanatuletea mizoga kwenye mambo ya maana - kweli hatuwezi kuendelea hata siku moja kwa style hii.
 
Pasco ipi Batili?

Ya CHADEMA au ya CUF na Wabia wake?
Kanuni zinairuhusu Chadema kuwa ndio the main opposition lakini logic bado inagomba. Hivyo Mbowe ameshakabidhiwa ofisi,gari na watumishi ila kuna taratibu hawajakamilisha hivyo kukosa legitimacy.
 
Kanuni zinairuhusu Chadema kuwa ndio the main opposition lakini logic bado inagomba. Hivyo Mbowe ameshakabidhiwa ofisi,gari na watumishi ila kuna taratibu hawajakamilisha hivyo kukosa legitimacy.

Heshima Mkuu Pasco!...Kwa faida ya wasomaji wengine pamoja na Mimi binafsi naomba uvavadue taratibu ambazo zinainyima Chadema kuwa Chama Kikuu cha Upinzani Bungeni?Hivi vitu vipo kwenye Katiba na kupindwa kwa namna yoyote ni kuinyima Chadema haki yake ya msingi ya kuunda Timu ya Upinzani Bungeni.Tunaomba maelezo ya kina!
 
kambi rasmi ili isiwe batili inatakiwa iweje?
Chadema wanazo sifa zote za kuwa chama kikuu cha upinzani. Hii maana yake ni Chadema pekee ndio wataunda serikali kivuli. Pia Chadema ndio wataongoza zile kamati 3 za PAC, LGAC na Parastal.inamaanisha UDP, CUF, NCCR na TLP vinakuwa jobless.
 
Well my brother Huwezi ukamlinganisha saadam hussein au Idi Amini na Anna Makinda....Anna Makinda hajamfanyia mtu yeyote kile kitu kibaya hadi mtu atokee kuanza kumtukana hivyo....Angekuwa amefanya what Iddi Amini,Hitler au Saadam hussein walivyofanya then mtu angekuwa na haki ya kufanya anachofanya yeye kuwa spika wa Bunge ndiyo inaleta chuki binafsi?....Kuna vitu vingi vya kujadili mtu anatoka from no where na kuanza kurusha maneno ya kashfa that is an acceptable.

Anna Makinda anachokonoa watu kwa kusema kuwa Sitta alirefusha mjadala wa Richmond un necessarily which is not true; in fact Sitta aliufupisha ule mjadala kwa kutokuuruhusu ufikie rightful conclusion na hiyo sasa ndio imemfanya aadhibiwe kwa kupokonywa uspika because of double dipping!! Anna will be well advised not to try and bully the opposition to please his masters; it is a fact that ALI KWINA has been planted as a speaker to serve a particular purpose of protecting FiSADI interests period!! Binti Maringo by the way, in your last sentence did you mean "UN ACCEPTABLE"!!
 
Namtakia kila la kheri jamani tumtendee haki hajaanza kazi akianza ndio marungu yaanze ila kwasasa hivi it is not fair. Kuhusu kumsema Mh Sitta nadhani anajipalia mkaa maana watu nao watampima utendaji wake (inawezekana pia ikawa anajiamini atafanya kazi nzuri hilo litamsaidia pia). Ila tumpe muda wa kumpima ila namuonea huruma kwani anakutana na wabunge wanaojua sheria hawachelewi kumpa vote of no confidence bunge la mwaka huu litawaka moto!!!
 
Ni muda tu utatuambia katika utendaji wa speaker wetu mpya. Mara nyingi,mkutano wa kwanza utatupa mwanga hasaaa kuhusu madame. Anatakiwa asome alama za nyakati na atekeleze nini Watanzania wanataka na si watu fulani wanataka.
 
kambi ya upinzani iliyotangazwa bado ni batili, haijatambulika rasmi. Upinzani ni shaghala baghala,

yaani cuf..... Cuf..... Cuf ......wananiudhi sana and this time i'm fed-up with them!!!!!!!!!!!. Yani baada ya mgogoro wa muda mrefu kule znz kumalizwa juzi kwa kuitwa dinning table na ccm ili wale wote keki ya taifa la znz, basi wameona ni dili na wameonelea waje huku bara waanzishe mgogoro mwingine bungeni ili waitwe na chadema wapewe vyeo. Hawa watu mbona waroho sana wa madaraka??????????
 
Mimi ninawasiwasi na uhuru wa mazingiza atakayokuwa anafanyia kazi. Pia ni mwoga kwa statement yake kuwa hatagombea 2015 inanipa mashaka juu ya kujiamini kwake katika kazi hii......This sentence was not supposed to be made at this time when she is just starting ....it made me feel kuwa hana confidence. Amenivunja moyo zaidi
 
Watanzania watakuwa hawamtedei haki Anna Makinda kabla kipenge hakijapulizwa tayari malalamiko kibao ebu tumpe muda tumpime utendaji wake anaweza kuwashangaza mafisadi wakajuta kumtosa Six.
Mkuu Ngongo, muda tuliompa unatosha au tuendelee kumpa zaidi?.
Pasco.
 
wapi na wapi yle mama ni mbishi sana na huwa anaongea kama anaongea na watot wa shule yaani ni kama

headmistress vile
anaongopa! mbona watammaliza fasta.

hatamaliza miaka 5 kama ndo hivyo
Mkuu Edson, nafanya rejea kupima kama hii miaka mitano mama atamaliza, I wish aondoke kwa amani na sio kwa pressure!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom