Spika Makinda ampiga Stop Stephen Ngonyani kumshambulia Dr Ulimboka

Mbunge wa Korogwe-CCM Stephen Ngonyani(Profesa Maji Marefu) amemshambulia vikali Dr Stephen Ulimboka na kuwataka madaktari wasimtibu.Spika Makinda ilibidi aingilie kati na kumuamuru Ngonyani kuacha mara moja kuzungumzia suala hilo ndani ya bunge kwa sababu liko mahakamani.Ngonyani akajitetea kuwa amechanganyikiwa kwa sababu aliumwa sana na watu wakamzushia kifo.Kabla ya kuwa Mbunge Ngonyani amewahi kuwa mganga wa kienyeji.

Kwani unganga ameacha lini?
 
Kwa bahati mbaya au nzuri, wakati Spika anamkalia Stephen Ngonyani kuongelea swala la Dr Ulimboka, tayari alishasema alichokusudia. Huyu mbunge alisema kwa kuwa madakatri wamegoma kutoa huduma kwa sababu ya kutoelewana na serikali basi wasiruhusiwe kumhudumia Dr Ulimbuka!.

Nitoe ushauri kwa wabunge wa ccm tena kwa moyo safi kabisa, wanapokuwa bungeni wasijisahau na kuanza kuongea kama wamepatwa na pepo mchafu. Wingi wao bungeni si chochote wala lolote kwa wananchi wa Tanzania. Hata kama wanalazimika kuisifia serikali maana ni ya chama chao watafute lugha ambayo haitatibua nyongo za wananchi.

Pamoja na kadhia ya mgomo huu bado public mood iko na madaktari, huu ndio ukweli, hivyo kutoa kauli za kulaani madaktari ni kujitakia kifo cha kisiasa. Use a more diplimatic language kama alivyofanya Dr Kingwangwala pale alisema anataka kuona pande mbili zinakaa mezani na kutatua hili tatizo. Lakini kauli kama za Stephen Nyongani ni kulewa madaraka, na sasa hivi ccm cannot afford kuonekana walevi wa maradara. Sikiio la kufa lina dawa?
 
ila komba hakukosea kuomba wabunge wapimwe akili. Si hawa tayar wanaanza kujieleza jaman au?
 
Hata hao waliomchagua mie sielewi vigezo walivyotumia! (Samahani simaanishi kuwatusi bali ninawasilisha unaive wangu katika hili maana niliamka tu na kusikia amekuwa Mbunge - Nadhani ninahitaji kuwa mwanafunzi mzuri wa siasa ya Tanzania)
 
Hivi huu prof wake kaupata chuo gani?maranyingi waganga wa kienyeji wanapenda kuijfungia kwenye majumba kama lile alikokutwa JOSEPHAT JOSEPH sasa hii shule ya uprof kaipata wapi?
 
Tokea lini mganga akawa mbunge basi na sisi watanzania ni Madhaifu,kutoka kupiga ramli hadi ubunge kweli waliomchagua nawapa pole

Tafadhali mkuu, sema wapiga kura wa Korogwe tena wengi wao wakiwa ni wa CCM ndio DHAIFU...huwezi tuweka siye Watanzania wa Ubungo, Kawe, Mbeya mjini, Arusha mjini n.k katika hilo kundi alaah!
 
[h=3]Hii ndiyo hasara ya kuchagua waganga wa kienyeji na matapeli kuwa wabunge[/h]

Profesa+maji+marefu.JPG

Nani angeamini kuwa mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi angeshangilia uvunjaji sheria na haki za binadamu? Imetokea tena bungeni ambapo mbunge wa Korogwe Vijijini Steven Ngonyani aka Maji Marefu kusema eti kipigo alichopata mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka kilistahili. Laiti bunge letu lingekuwa ni bunge huyu alipaswa kuwajibishwa mara moja. Maana hii si kashfa ya kawaida.
 
Hao ndio wabunge wa CCM wanaojali shibe. Tangu lini mganga wa kienyeji, mpiga ramli akawa mwakilishi mzuri wa wananchi. 'Mganga adai tembele, huwa adai vitu kama mbuzi, kuku, kanga, n.k.'
 
Mbunge wa Korogwe-CCM Stephen Ngonyani(Profesa Maji Marefu) amemshambulia vikali Dr Stephen Ulimboka na kuwataka madaktari wasimtibu.Spika Makinda ilibidi aingilie kati na kumuamuru Ngonyani kuacha mara moja kuzungumzia suala hilo ndani ya bunge kwa sababu liko mahakamani.Ngonyani akajitetea kuwa amechanganyikiwa kwa sababu aliumwa sana na watu wakamzushia kifo.Kabla ya kuwa Mbunge Ngonyani amewahi kuwa mganga wa kienyeji.

Kuepuka kauli na watu kama hawa inabidi tutengeneze sheria kama ya Kenya kwamba ili uwe mbunge lazima uwe na degree kuanzia moja dunia imebadilika siku hz!tutaondoa kero za namna hii mjengoni!
 
Wabunge ndio watunga sheria. Hata haiingii akilini kwa mbunge kuwapongeza watu waliojichukulia sheria mkononi. Hiki nacho ni kituko cha karne!!
 
Back
Top Bottom