Spika Makinda Afafanua mvurugano kwenye mjadala wa Sheria ya Mchakato wa Katiba

naomba kujua kama joseph warioba ni cdm..na kama ni ccm je kwanini hakuzomewa jana..

Hata Anna Makinda Spika wa bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anajua jibu la hili swali ila kwa kiburi chake/chao hatataka kulijibu anabakia kuwalaumu baadhi ya watu(vyama vya upinzani) anatafuta pa kushika .je tutafika kwa hali hii?
 
Mojawapo ya dharau nayoongelea mimi ambayo inawekwa na CCM na Serikali yake ni kuandika huo muswaada kwa lugha ya Kiingeleza, then ijadiliwe na wananchi wote kuanzia ngazi ya Serikali ya vijiji tena kwa muda mfupi.

Hivi wananchi wangapi Tanzania wananjua lugha hii? hata wawakilishi wetu (Wabunge) karibu nusu ni (ma Maimuna) sasa tutegemee kitu gani hapa?.
 
Zitto alitoa mchango mzuri, hakuna haja ya kuwa na dharula kwenye hili. Wabunge wauchukue wapeleke kwa wananchi wakusanye maoni yao. Haya yote yasinge tokea

Sawa,
lakini,vipi wakiwaruhusu wabunge kweli waende majimboni kwao,wazungumze na wananchi wanavojua wao (au wasizunguke kabisa kukusanya maoni),...kisha warudi bungeni kusema hivi ndivyo wananchi wa jimbo langu wanavosema,...

Kwa wingi wa vilaza bungeni kuna kizuri unategemea au wewe na zitto mli maanisha kuruhusiwa kupiga kampeni?
kama ni hivi ni tume gani ya kukusanya maoni itunike NEC?
 
then wajue inavyoboa pale wanapozomea wabunge wa chadema bungeni..mkuki mtamu kwa nguruwe..
 
Naamini kama CCM sio mazuzu, swala la katiba ni la wananchi wote na wala siyo la Chama fulani!!! Kwa hili nadhani wabunge wote wataungana!!!
 
Makinda alaani zomea zomea.
Asisitiza muswada sio sheria,
asisitiza kuchangia kwa amani.
Zomea zomea kwa viongozi walianzisa wao , nimeshuhudia sisiem wakizomea viongozi wa upinzani mara mbili wakati wakitoka nje ya bunge tena waliwasindikiza na maneno ya kashfa, Sasa leo zomea imekuwa chungu kwao.
-Ama kweli kunya anye kuku akinya bata anaambiwa ameharisha.
-Kama wewe kijana ama mtu mzima halafu uko ccm ni muhujumu uchumi unapaswa kushtakiwa kwa kufanya uhaini.
Nafikiri ccm ni moja ya kipimo kimoja wapo ukitaka kujua kama mtu ni fisadi ama atakuwa fisadi muhujumu uchumi muulize yeye ni chama gani :
Jibu:
ccm= muhujumu uchumi, tapeli na mpenda rushwa(kutoa or kupokea), mjinga,fisadi na yafananayo na hayo
cuf= kigeugeu/ njaa kali ama mtu asiyekuwa na msimamo, anaweza kuoa ama kuolewa haimpi shida(kisiasa)
chadema = mwanaharakati, mpenda haki na freedom fighter
 
yap yap, nakubaliana na wewe mama!!

Lakini Remmy ukumbuke kwamba "enjoy your right so as not to infringe the other person's right". Unachukuliaje kadhia ya Tambwe Hiza anatetea mamlaka ya Rais kwenye Mswada huu akijua fika kwamba rais akibaki na hayo mamlaka yatadhuru haki za raia wote, halafu anaambiwa kwa kufanya hivyo anawaudhi na kuwavunjia haki wananchi na yeye anaendelea kuongea tu as if wanaomsikiliza ni makondoo.

[/COLOR]

Hapo kwenye red, hii ndo kitu cha busara sana. Kila mtu ana haki ya kusikiliza bwana.... hata natural justice ina demand hivyo.
 
kwani sie wa mbali si watanzania ,kweli mikoa ya pembezoni imekuwa mingi siku hizi. dar na dom ndo tanzania basi hiyo katiba iwe yao sie tuanze mijadala ya katiba yetu. Na nakwmbia akija huyo taabu hizo anakula panga nyie wa mjini mnazomea tu huku atakula upinde na panga
 
naomba kujua kama joseph warioba ni cdm..na kama ni ccm je kwanini hakuzomewa jana..

Wananchi wameamka, hivyo wanaweza kuwapambanua wapenda maslahi ya nchi na wapenda mashabiki wa vyama. Warioba hakuzomewa kwa sababu amesha jipamba nua kuwa yeye ni mpigania maslahi ya taifa.

Huko CCM kuna watu safi, kuna wapambanaji wazuri tuu wa maslahi ya taifa, watu kama kina Warioba, Dr. Salim, Butiku, Peter Kisumo, na hata vijana kama kina Nape Mnauye ni watu wanaosimama na maslahi ya taifa.

Mimi binafsi siamini jana kuwa Tambwe Hiza ndiye aliyetumwa kuwasilisha maoni ya CCM kwenye Kamati ya Bunge, naamini kwa vile lengo la mkutano wa jana, ni public hearing kwa ajili ya wananchi, CCM iliupuuzia mkutano huo na Tambwe Hiza kwa kujipendekeza, alikuja kuhudhuria kama mwananchi tuu, ndio maana jina la mwakilishi wa CCM halikuwepo kwa Mwenyekiti wa kikao, ila Tambwe Hiza kwa kimbembele chake, akajipeleka jina lake na kupewa nafasi.

Sina tatizo na Tambwe na timu yake pale CCM Lumumba wakiongoza kitengo cha Propaganda, kwao propaganda ni kuwa mabingwa wa kupayuka au kujibu mapigo, na ndiocho alichokuja fanya pale jana, alipoanza tuu kupayuka, wananchi waliokuwepo pale wakamkataa na kuvurugika amani ndipo kukafuatia.

Ila pia lazima tufike wakati, viongozi waandilifu wa vyama, wanawajibiki kuwadhibiti wafuasi wao. Mkutano wa jana ilihusu wananchi, ila ile zomea zomea japo ilifanywa na wananchi, kulikuwa na kamkono kidogo ka ushabiki wa baadhi ya watu. Kuna watu walisimama, hata kabla hawajaongea, walishabikiwa kuliko mfano. Walipo changia vipenzi wao ni kushangiliwa tuu mwanzo mwisho hata kama hao vipenzi wao wamechangia pumba, walipigiwa makofi ya pongezi!

Lets be fair, watu wapewe uhuru wa kuchangia mawazo yao hata ziwe pumba vipi?.
 
CCM walivyo wanaweza kupitisha mswada huu kwa kukomoa Chadema na hapo ndipo watakipata cha mtema kuni. Kwa nini CCM wanatuma mamaluki kama Tambwe na Bagenda kukiwakilsha chama? Mambo ya kujitakia.
 
Watanzania tuko zaidi ya Milioni 42. Ni vyema zaidi kukawapo na wigo mpana zaidi wa kuwafikia Watanzania wengi kadiri inavyowezekana hii habari ya "ghafla" na "dharura" sijui inatokea wapi.

Sitegemei wabunge wa CCM walio wengi kuukwamisha Muswaada huo. Na ikitokea wakafanya hivyo, kwa maana ya Wabunge hao wa CCM wakaukwamisha Muswaada huo wa sheria, basi, Wabunge hao wa CCM watakuwa wameanza kazi ya ’ Chama kujivua magamba’ na baadhi yao kunusurika na adhabu ya wapiga kura ifikapo 2015.
 
Duuh Pasco hayo huwezi kuyakwepa ya kushangilia , ndio maana yeyote atakaye taka kuchangia lazima atangulize maslahi ya taifa kwanza,ngwe ya wananchi kubururwa na propaganda za CCM naona zimeshapita kwa sasa na hazitarudi kamwe
Nimesikiliza mijadala hii ya huu Mswada kwenye vipindi vya redio,television na simu za wasikilizaji ,n ule mkutano wa UDASA kweli kabisa Pasco amini usiamini enzi za ndio mzee naamini sasa zimeshapita, wananchi wanaufahamu sana na haki zao ,na kwa mantiki hiyo tunamuomba muheshima Spika na kamati yake ya bunge wawe imara kweli kutuletea mswaada utakao tupitisha kwenye ngwee ya uandikaji wa Katiba salama,kinyume cha hapo nina mashaka muheshimiwa Spika atakuwa wa kwanza kupopotolewa na mawe,
Pasco kuna siku ulitegemea CCM wangelalamika na kuogopa wapinzani manake sasa hivi unaona kabisa walivyojaa hofu kwa sababu wanajua kabisa wana nguvu kubwa ya kukubaliwa na UMMa,jinsi siku zinavyozidi ndio jinsi upinzani unavyopata kuungwa mkono.
 
CCM walivyo wanaweza kupitisha mswada huu kwa kukomoa Chadema na hapo ndipo watakipata cha mtema kuni. Kwa nini CCM wanatuma mamaluki kama Tambwe na Bagenda kukiwakilsha chama? Mambo ya kujitakia.

Aliwahi kuandika jenerali ulimwengu kwamba hulka ya mtu aliyehamia kwenye chama kutoka chama kingine ni kufanya kazi kwa unafiki na kujipendekeza kwa kiwango cha juu ili aonekane ana nia ya dhati na mapenzi kwa chama hiki kipya kuliko kile cha zamani alichotoka. Na kwa kuwa makada wengi wa ccm wenye akili zao wanaogopa kujiaibisha kwa kuongea mambo ambayo hayakubaliki na wananchi, basi wanasakiziwa hawa vibaraka waliohamia kwa sababu hawawezi kukataa.
 
Safi Ivuga, awali ya yote hawa viongozi walafi ni wangonjwa na magonjwa yao ni zao la ufisadi.
 
Mark,
Wanasiasa wana haki ya kuwazungumzia watanzania kuliko watu. Wanasiasa angalauuliowataja wanadhamana ya watanzania hivyo wanapozungumza hawazungumzi kwa ajili yao bali kwa ajili ya watanzania. Hoja yako ni ya kipropaganda na upotoshwaji. Wewe kama Mark, vinginevyo uwe jasiri utufahamishe jina lako kamili na nafasi yako katika jamii ili uwazungumzie watanzania. Ama sivyo jizungumzie wewe, na sisi ambao tuna ujadsiri na hatujifichi tuwazungumzie wale tunaowawakilisha. Hoja ya Katiba kimsingi ni hoja ya kisiasa, unless hujui maana ya siasa, mipaka ya siasa na maana ya uongozi wa kisiasa. Issue ya Katiba ni issue yetu kama wana siasa, na pia kama wananchi unless unatuambia kuwa wanasiasa wa Tanzania siyo Watanzania. Lets be realistic, na tuzungumze kama wazalendo kila mmoja kwa nafasi yake, ufahahamu wake na kwa kadiri na kiwango cha uchungu wake kwa Taifa lake. Anayechezea Katiba anacheza mchezo wa hatari sana

Dr. inawezekana huyu Mark ni Deo Filikunjombe, kwani ametumia maneno kama yale ambayo yalitumiwa na Deo Filikunjombe wakati wa kumtuhumu Mwanakijiji. Sababu pia alizotoa zinafananafanana
 
Mark,
Wanasiasa wana haki ya kuwazungumzia watanzania kuliko watu. Wanasiasa angalauuliowataja wanadhamana ya watanzania hivyo wanapozungumza hawazungumzi kwa ajili yao bali kwa ajili ya watanzania. Hoja yako ni ya kipropaganda na upotoshwaji. Wewe kama Mark, vinginevyo uwe jasiri utufahamishe jina lako kamili na nafasi yako katika jamii ili uwazungumzie watanzania. Ama sivyo jizungumzie wewe, na sisi ambao tuna ujadsiri na hatujifichi tuwazungumzie wale tunaowawakilisha. Hoja ya Katiba kimsingi ni hoja ya kisiasa, unless hujui maana ya siasa, mipaka ya siasa na maana ya uongozi wa kisiasa. Issue ya Katiba ni issue yetu kama wana siasa, na pia kama wananchi unless unatuambia kuwa wanasiasa wa Tanzania siyo Watanzania. Lets be realistic, na tuzungumze kama wazalendo kila mmoja kwa nafasi yake, ufahahamu wake na kwa kadiri na kiwango cha uchungu wake kwa Taifa lake. Anayechezea Katiba anacheza mchezo wa hatari sana
Ndiyo maana tunakupenda!.....meseji sent na ubarikiwe sana!
 
Back
Top Bottom