Spika kuomba ulinzi kwake uimarishwe

Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,486
3,468
Sijui kama wana jamii walitafakari kauli ya spika jana akilalamika kuwa kuna watu wanajaribu kumchafua kupitia kwenye mitandao, magazeti na wengine kuingia jimboni kwake na kutoa zawadi kwa wapiga kura wake.
Mtanisamehe wana jamii kama ninawakwaza lakini mimi huota sana njozi za mchana na katika njozi hizi nilikuwa ninajiuliza huyu mwenye kigoda juzi juzi tu aliwaambia wanabunge kuwa katika zama hizi za demokrasia inabidi wawe na ngonzi ngumu kuweza kuhimili mikimiki ya siasa. Jee yeye hivi sasa bado ana ngozi laini?
Afadhali wenzetu hao wana jukwaa la kusikika Jee wale ambao hawanga jukwaa lakini husemwa katika jumba kuu la dodoma inakuwaje?
Hivi kusemwa kwenye mitandao na magazeti inatosha kuomba ulinzi uimarishwe kumlinda mzee?
Halafu hawa wanasiasa wetu ambao ni wabunge hivi hayo majimbo ni mali yao? Katika dahari hizi za demoghasia kila mtu ana haki ya kujiuza kwa wananchi sasa hawa wazee wanaogopa nini kama kweli wanaamini kuwa bado wanauzika kwa wananchi?
Mbona kuna mbunge amejitokeza waziwazi na kusema kwamba anatarajia kugombea urahisi mwakani lakini mzee JK ambaye kwa hivi sasa ndiyo mwenyenchi wala hakuonesha kupanick na kuweka mikwara?
Wanajamii kwa vile nilikurupushwa na mnyapara wa kazi ilibidi niamke lakini hata baada ya kuamka bado sijapata majibu pengine tafakuri zenu zinaweza kusaidia kueongeza uelewa wangu.
 
Goood Ideal! nakuunga mkono na mguu kuwa uliyosema yote yapo sahihi, labda niongezee kuwa, yawezekana jamaa zetu hawajajiandaa na maisha ya baadae baada ya ubunge! umenikumbusha ndugu yangu, SS aliomba wabunge wawe na ngozi ngumu yeye kuguswa tu kidogo kwenye mtandao karuuka! mkaaali! No nae twamuomba awe tu awe na ngozi ngumu Urambo watamuuliza kwa miaka karibu 30 aliyokuwa kwenye System ameifanyia nini urambo zaidi ya Bara bara ya mashimo tu toka Tabora hadi Urambo
 
Ni kweli kabisa hahitaji kuongezewa ulinzi wowote. Labda kama kuna tishio la mdomo ama maandishi. Lakini amezungumzia mitandao na magazi ya kina Rostam tu. Naamini ana wasiwasi wa kukosa ubunge mwakani.
 
Mimi nashangazwa na hawa MASHUJAA WETU WA KUPAMBANA NA UFISADI HASA KUTOKA CCM au ndio hayo tuliyoambiwa ndani ya huo waraka? Badala ya kujisafisha na shutuma huwa wanakimbilia kutafuta wachawi.
Hivyo ukiwa kiongozi unategemea nini? Lazima kutakuwa na watu wasioridhika na vitendo vyako iwe kwa chuki zao au kuwepo ukweli. Kiongozi alie msafi huwa hana woga na mambo kama hayo kwani rekodi yake inazihirisha uadilifu wake. Nilitegemea Mheshimiwa Spika angalau angetudanganya roho kwa kusema kuwa yuko tayari kufanywe uchunguzi wa tuhuma hizo lakini njia aliyotumia inanipa mashaka pengine kuna kaukweli fulani kwa hayo aliyosakaziwa.
 
Back
Top Bottom