Spika Job Ndugai afunguka, aahidi kukaa chini na UKAWA

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa Tanzania Job Ndugai, amesema anasikitishwa na Wabunge wa UKAWA na Tabia yao ya kutoka Nje. Japo ni haki yao kutoka nje lakini hivi karibuni imezidi. Japo itaendelea hivi tutakuwa hatujengi nchi amesema.

Ameahidi yeye mwenyekiti wa Bunge na naibu Spika watakaa na UKAWA wamalize hili tatizo kwani haipendezi spika unakaa mtu anatoka nje.

Amesema Sasa Nchi hii Migogoro, utengano umezidi, ni jukumu letu kama Viongozi kumaliza hii hali.

Kasema Wabunge waliofungiwa ilitokana na matomeo ya sintofahamu. Kwani kabla ya kufungiwa tunaomba Mbunge afute kauli yake, arekebishe au alete ushahidi. Pale anapokaidi huitwa kutoa ushahidi lakini saa nyingine hukataa. Mfano kuna Mbunge alisema polisi wameleta Magari ya Washawasha 700. Tulipomwambia alete ushahidi akasema alisoma Kwenye JamiiForums. Kama bunge hatuwezi fanya kazi kwa kutengemea Mitandao

Anasema hii hali inayoendelea bungeni inachochea chuki na Migogoro. Ni bora sasa tukaa nchini kama taifa ili tumalize hii hali.

Anasema kama Spika hatavumilia vijembe na kejeli kuendelea Bungeni

Ni haki ya mbunge kutoka nje. Lakini wale waliobaki nao wanawashambulia waliotoka, hili nalo ni tatizo. Wabunge wakitoka nje mambo mengi huharibika. Inachafua hali ya hewa. Uchaguzi unapoisha, siasa huhamia Bungeni.

Tunachukulia Mbunge kama mtu mzima. Chama tawala na UKAWA na sisi tukae chini tuongelee hili swala.

Wabunge wamezoea kuona Spika na Naibu wake wakiwa wabunge wa kuchaguliwa, hii ya naibu Spika kuwa wa kuteuliwa wanahofu kwamba atakuwa anapokea maelekezo kutoka Sehemu Fulani. Naomba niwahakikishie kwamba, sisi hatupokei maelekezo kutoka sehemu yoyote bali tunatoa maamuzi yetu tunavyoona inafaa. Hivo watuamini.

==========

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amekiri bunge hilo kusambaratika na kuwa vipandevipande kutokana na vurugu za mara kwa mara zilizopelekea wabunge wa upinzani kususia vikao hivyo anawaalika wabunge hao kwenye mazungumzo.

Ndugai amesema ili bunge lifanye kazi yake yake, linahitaji kuishinda changamoto iliyopo ya bunge kutokuwa kitu kimoja, huku akielezea wazi kuwa chanzo kikuu kinachosababisha bunge hilo kusambaratika ni pamoja na "u-vyama" kuzidi na wabunge kutojali maslahi ya taifa.

Sababu nyingine aliyoitaja Ndugai, ni ugeni wa wabunge ambapo kila unapofanyika uchaguzi sehemu kubwa ya wabunge huwa ni wageni hivyo wengi wao wanakuwa hawajaelewa kanuni na tamaduni za kibunge.

Amesema yanayotokea sasa kwa kiasi kikubwa siyo mageni, yalikuwepo tangu wakati wa bunge la 10. "Hali hii imeanza zamani kidogo tangu enzi za spika Makinda, wabunge walikuwa wakitoka nje, wakigomea vikao, wakiadhibiwa n.k.

Ugumu ambao tunaupata ni kwamba kila baada ya uchaguzi wanakuja wabunge wengi wageni ambao hawajui mambo mengi na mfano ni bunge hili ambapo karibu 70% ya wabunge ni wapya" Ameeleza Ndugai na kuongeza kuwa hata suala la kumsusia Rais anapokwenda kuhutubia bungeni, limewahi kutokea katika bunge lililopita.

Pamoja na hayo, Spika Ndugai amesema kuwa hakuna kanuni inayomzuia mbunge kutoka nje ya bunge kwa kuwa ni haki yake "Hakuna kanuni inayomkataza mbunge kutoka nje, ni sehemu ya demokrasia yao, lakini hii ya sasa imezidi, ni jambo lisilopendeza... maana watanzania wamewatuma kwenda kuwakilisha hoja zao, wanapotoka inakuwa haipendezi".

Amewasihi wabunge wa Upinzani kurudi bungeni na kueleza mambo yaliyowaudhi ili wakae wajadili na watafute ufumbuzi badala ya kuendelea kususia. Amesema "Wabunge kutoka nje ni jambo ambalo halipendezi hata kidogo, nisingependa niendelee kuliona".
"Nawaomba katika bunge lijalo kama wanahisi tunakosea watueleze, na sisi tuwaeleze wanakosea wapi ili twende sawa"

Kuhusu malalamiko ya wapinzani dhidi ya Naibu Spika, amekiri kupokea malalamiko hayo kupitia kwa mbunge james Ole Millya, na yeye aliyawasilisha kwenye kamati husika lakini hoja zote ambazo walikuwa wakizilalamikia zilizonekana hazina uthibitisho, hivyo maamuzi ni kwamba Naibu Spika Dkt Tulia Ackson hana hatia yoyote.

Kuhusu hoja ya Naibu Spika kuendelea kukalia kiti kwa muda wote Ndugai anasema " Uongozi ndiyo unapanga nani akae pale, sioni tatizo la mtu kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu, lakini kama mtu anakosea, zipo fursa za kupeleka jambo kwenye kamati badala kulalamika bila kufuata kanuni"

Amesema haoni tatizo la Naibu Spika na hajui ni mambo gani amewaudhi ila anadhani kinachowasumbua wapinzani ni hisia za jinsi Naibu Spika alivyopatikana
Wabunge wa upinzani wanapitia changamoto nyingi kabla ya kuingia Bungeni, wengi wao wanahangaika sana kupata ubunge hadi kufikia hatua ya kulala sana selo (polisi) kwaiyo namna ya 'kudeal' nao inahitaji uvumilivu kidogo.

Naibu Spika siyo mbunge wa jimbo, na wao wamezoea mbunge wa jimbo ambaye anafanana nao, Naibu Spika ni mbunge wa uteuzi kwahiyo wanahisi anafanya kazi kwa kufuata maelekezo kutoka nje ya bunge au anatumikia mabwana wawili jambo ambalo siyo kweli. Pia adhabu zilizokuwa zinatolewa zinawafanya wahisi wanaonewa kila wakati"

Pia Spika amekemea tabia ya baadhi ya wabunge wa CCm kutumia muda mwingi bungeni kurusha vijembe kwa wabunge wa upinzani
"Kwa wabunge wa chama tawala siyo jambo zuri kurusha vijembe, tukienda bungeni nitakaa nao, na nitawaeleza kuwa siyo jambo jema kuwa na bunge la vijembe, nawaasa tubadilike, tuheshimiane ... matusi kelele vijembe kanuni haziruhusu na haipendezi"

Kuhusu mwenendo wa baadhi ya wabunge kutoheshimu kanuni, Ndugai amesema "Kanuni zimetungwa kwa watu wazima, lakini tatizo wabunge wanaokuja sasa hivi wengi ni vijana, na wako chini ya kiwango cha kanuni. Bado sijajua nini cha kufanya ili hali hii isiendelee, kwenye bunge la katiba angalau kulikuwa na kitu kinaitwa kamati ya maridhiano, nafikiri inabidi tuige kitu hicho tupate watu hata wastaafu watakaokuwa wanakaa kuyaweka mambo haya sawa"

Kuhusu sakata la Lugumi, Ndugai amesema kuwa kamati ndogo iliyoundwa kufuatilia suala hilo itatoa taarifa yake katika mkutano ujao wa bunge.

Kuhusu uamuzi wa serikali kuzuia Bunge LIVE, Ndugai amesema uamuzi huo ni mzuri na anauunga mkono kwa kuwa unasaidia kupunguza vurugu kwa wabunge.
 
Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa Tanzania Job Ndugai, amesema anasikitishwa na Wabunge wa UKAWA na Tabia yao ya kutoka Nje. Japo ni haki yao kutoka nje lakini hivi karibuni imezidi. Japo itaendelea hivi tutakuwa hatujengi nchi amesema.

Ameahidi yeye mwenyekiti wa Bunge na naibu Spika watakaa na UKAWA wamalize hili tatizo kwani haipendezi spika unakaa mtu anatoka nje.
Huyo ndiye aliyetakiwa kukalia hicho kiti kuliko huyo mama
1471155840594.jpg
 
Aangalie mtego ulipo, kama anataka kukaa ili kujadili pamoja na ukawa Tulia asiwepo maana anaweza kususiwa kikao!!! Mbaya zaidi ikiwa tulia ndio anakuwa wa mwisho kufika kikaoni na ukawa wananyanyuka na kuwaachia ukumbi wa mkutano.

Maana wameapa kutokuwa mkutanoni na Tulia.
 
Namskiliza hapa NDUGAI anavomjibu TIDO, namuona kama anatumia hekma sana kujibu hoja za TIDO
 
Tactic ya wapinzani kutoka nje ya bunge imepitwa na wakati- Ndugai
 
Aangalie mtego ulipo, kama anataka kukaa ili kujadili pamoja na ukawa Tulia asiwepo maana anaweza kususiwa kikao!!! Mbaya zaidi ikiwa tulia ndio anakuwa wa mwisho kufika kikaoni na ukawa wananyanyuka na kuwaachia ukumbi wa mkutano.

Maana wameapa kutokuwa mkutanoni na Tulia.
Siyo mkutanoni wana ukawa wanampinga Tulia kuongoza kikao huo mkutano kasema nani?
 
Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa Tanzania Job Ndugai, amesema anasikitishwa na Wabunge wa UKAWA na Tabia yao ya kutoka Nje. Japo ni haki yao kutoka nje lakini hivi karibuni imezidi. Japo itaendelea hivi tutakuwa hatujengi nchi amesema.

Ameahidi yeye mwenyekiti wa Bunge na naibu Spika watakaa na UKAWA wamalize hili tatizo kwani haipendezi spika unakaa mtu anatoka nje.

Amesema Sasa Nchi hii Migogoro, utengano umezidi, ni jukumu letu kama Viongozi kumaliza hii hali.

Kasema Wabunge waliofungiwa ilitokana na matomeo ya sintofahamu. Kwani kabla ya kufungiwa tunaomba Mbunge afute kauli yake, arekebishe au alete ushahidi. Pale anapokaidi huitwa kutoa ushahidi lakini saa nyingine hukataa. Mfano kuna Mbunge alisema polisi wameleta Magari ya Washawasha 700. Tulipomwambia alete ushahidi akasema alisoma Kwenye JamiiForums. Kama bunge hatuwezi fanya kazi kwa kutengemea Mitandao

Anasema hii hali inayoendelea bungeni inachochea chuki na Migogoro. Ni bora sasa tukaa nchini kama taifa ili tumalize hii hali.

Anasema kama Spika hatavumilia vijembe na kejeli kuendelea Bungeni

Ni haki ya mbunge kutoka nje. Lakini wale waliobaki nao wanawashambulia waliotoka, hili nalo ni tatizo. Wabunge wakitoka nje mambo mengi huharibika. Inachafua hali ya hewa. Uchaguzi unapoisha, siasa huhamia Bungeni.
heading yako figganigga
Huyo ndugai unaibu spika tena inamaana kashushwa cheo?
 
Back
Top Bottom