Spika Amuonya Waziri Mkuu Bungeni

Kimoyo moyo alimwambia

acha ujinga bana embu jiheshimu hata kama waziri mkuu haapa mi ndio rais m ndio waziri mkuu tafadhali
unakuwa huna adabu hivi kwa familia unakuwaje??
 
Nataka kuona next step ya Anna Makinda ...ya kijasiri kabla ya kumsea lolote la ujasiri na kubadilika kwake!
 
Mama anaelewa somo taratibu,tutafika hiyo mizee iliyoko bungeni haibebeki kabisa.
 
Hakumuonya waziri mkuu bali aliwaonya wabunge na mawaziri yanaoenda kuongea na waziri mkuu na kuwataka waache tabia hiyo na badala yake wamfuate ofisini.
 
Yup,ni kweli Spika amesisitiza kuwa, kama hali hiyo itaendelea basi ni heri waziri mkuu huyo asiwe anaingia kabisaa bungeni,abaki ktk ofisi zake za nje ya bunge hali akiendelea kutatua matatizo hayo matatizo ya wabunge!
Saiz,Imekuwa kama ni utamaduni kwa wabunge na mawaziri kwenda alipokaa Mh. Pinda na kuanza kusema nae wakati sessions za bunge zikiendlea mpaka ina-bore......na ndo maana imefika hatua baadhi ya wabunge wamefikia ata kughushi sahihi ya Pinda kwa kuandika messsages za uongo kwa wabunge wenzao zinazosema kuwa mbunge fulani anahitajika haraka sana na W/mkuu kuna jambo mhimu la kuongea nae na wakati sivyo!!. Hayo yamemtokea kwa Mb. Selasini hivi juzi......
Ukweli Kwa leo Makinda ameonyesha kuwa meno anayo!
 
Mwenyenzi Mungu tunusuru sisi Watanzania na viongozi Wanafiki kama Kikwete,Sitta,Ngeleja,Anna Makinda,Pinda na Mkullo.Asante baba kwa kutusikiliza.Mungu Ibariki Tanzania.AMEN
 
Tatizo huwa wanakuja bungeni wakiwa hawajajiandaa. Hivyo huwa wanashauriana na kutunga uongo upi wautoe kwa wakati huo kuwahadaa watz. Ndiyo zao hizo vilaza wakubwa!!

Na mimi nilikuwa napata picha hiyo hiyo. uongo wa dakika ya mwisho kabla ya kitimoto.
 
Kamuonya pinda maana yeye ni kiongozi wa wabunge wa ccm. Makinda ni kiongozi wa wabunge wote bungeni. Pinda mambo na maamuzi yake yako pindapinda tu kumbe chanzo ni pinda mwenyewe kuruhusu umbea na wasiofikilia kwa kutokutumia ubongo.
 
Jana nilishuhudia kwenye taarifa ya habari ya TBC1 wakati mama anatoa cheche!! Akasema unaona mwingine yuko pale na kapigwa picha, mara inasogezwa picha namuona Mkullo yupo na PM macho yamemtoka pima ilibidi PM ainamishe uso lakini wapi mama akaendelea kuchana live. Mkullo mara atabasamu mara ainame lakini mama yuko nao tu anachana!! Kweli jana alionesha makucha. Baada ya juzi kusema kuwa hakuingizwa na mafisadi naona sasa ameamua. Mama kama yule asipofanya kazi yake kwa umakini ili watanzania wote wamuheshimu atakuwa amekosa fursa ya kujiandikia kahistoria kwenye nchi hii maanake sioni akienda zaidi ya uspika.
 
Huyu mama ameanza kutoa kauli ambazo sikuzitarajia zitoke kwa mtu kama yeye.
Hivi majuzi alilaani wabunge wanaochapa usingizi bungeni ambao ni wazi ni wabunge wa CCM.
Sasa kamkataza waziri mkuu ambaye pia ni CCM aache kuligeuza bunge kijiwe cha porojo.
Siamini mtu yeyote wa CCM kama anaweza kufanya jambo zuri kwa nia njema,huenda kajisahau au kuna kamchezo.
 
Back
Top Bottom