Spika Amuonya Waziri Mkuu Bungeni

Mkuu sijui kama Pinda atamuachia tena 6 uwaziri mkuu. 6 naye si haba anaweza akang'ang'ania u PM!!

Mkuu jamaa alivyondoka kwenda Brazir, huku nyuma 6 akavurunda ndio maana akamteua Marry Nagu kukaimu alivyoenda Moro siku ya alhamisi.
 
Mbona haja wakemea wanao sinzia bungeni na kuchafua ukumbi....Ning'e mpongeza kama ang'e muonya kwa kutumia bunge kuwadanganya watanzania mara kwa mara...

Yess!! Na pia kumtaka athibitishe anachokisema Bungeni -- kama vile alivyosema kwamba waliokufa kule Arusha mapoema mwaka huu kulisababishwa na CDM.
 
Magamba ni magamba tu siku zote. Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
 
Pinda ndio anatabia ya kuwaita ita anajifanya yuko serious kumbe wapi... Tunamumic Ngoyai kwenye u-PM huyu kapwaya kama mkulu wa ikulu.
 
Heshima kwako Tatanyego.

Naomba kumpongeza Mheshimiwa Anna Makinda hakika amenifurahisha akiendelea na mwenendo huu atalijengea bunge letu heshima iliyoanza kufifia tangu aliponyakua mikoba ya uspika.

Spika wa Bunge la Jamhuri Mh. Anna Makinda amemtaka Waziri Mkuu kutoongea na wabunge pamoja na mawaziri wakati kikao kinaendelea ndani ya bunge. Spika amesema kwa kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kusikiliza na kufuatilia mijadala kwa makini. Amesema kama hali hiyo inaendelea hakuna maana kuwa na kiongozi wa wa shughuli za serikali bungeni.

Katika siku za hivi karibuni wabunge na mawaziri wamekuwa na tabia ya kwenda kunong'ona na waziri mkuu wakati kikao cha bunge kinaendelea. Hata hivyo wakati Spika anatoa onyo hilo, Mh. Mkulo alikuwa anaongea na Waziri mkuu na baadaye Mh. Wasirra akajisogeza na kuanza kuongea na Mh. Pinda.
 
Bora. Binafsi huwa inaboa sana. Unakuta wakati mwingine wabunge wanachangia (hasa wa upinzani) lakini waziri muhusika anapiga soga.. Hii ni dharau nafikiri MSG sent & delivered.
 
Pinda ni waziri mkuu kimeo kuliko wote waliotokea tanzania
Asikilize nini wakati hatumii ubongo kuchambua???
bora asafiri nje ya nchi amwachie mnafiki Sitta usukani atukane tena
Hata ww hutumii ubongo kuchambua unasema bora ya 6?
 
Nadhani amesoma alama za nyakati, na amejaribu kuwabeba lakini hawabebeki. Pia amesha enda safari za nje kama mara tatu hivi, atakuwa amekutana na Maspika wenzake na wakati wa faragha zao za kushare experience, atakuwa ameelimika kidogo. Nakumubuka hata Jmosi mara baada ya bajeti ya Nishati kupita, alitoa angalizo kwa Serikali, sasa wende wakafanye kazi na sio kupepeta maneno, akaongeza pia kuwa, wapo wengi mle mjengoni wanaotaka nafasi hizo za Uwaziri, kwahiyo wasilete longolongo zao tena. Nadhani anaanza kuifahamu kazi yake.
 
Pole sana mama; mtu akudharaye hakuchagulii tendo!!!

Sisi wengine huku mitaani tunasikitishwa sana na hizo tabia lakini ndio kam hivyo Bunge tukufu limeshageuzwa sehemu ya minong'ono na mi-dili tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wapiga kura sasa tukimbilie wapi wa kutusemea kwa mtaji huu wa tabia ilioibuka bungeni ya KUTOKUFUATILIA WALA KUTILIA MANANE mijadala muhimu kwetu kule Mjengoni Dodoma????????

Anyway, makosa ni yetu sisi wenyewe wapiga kura na jinsi tunavyotekeleza hili jukumu la ki-katiba nchini kila wakati wake unapojiri.

Spika wa Bunge la Jamhuri Mh. Anna Makinda amemtaka Waziri Mkuu kutoongea na wabunge pamoja na mawaziri wakati kikao kinaendelea ndani ya bunge. Spika amesema kwa kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kusikiliza na kufuatilia mijadala kwa makini. Amesema kama hali hiyo inaendelea hakuna maana kuwa na kiongozi wa wa shughuli za serikali bungeni.

Katika siku za hivi karibuni wabunge na mawaziri wamekuwa na tabia ya kwenda kunong'ona na waziri mkuu wakati kikao cha bunge kinaendelea. Hata hivyo wakati Spika anatoa onyo hilo, Mh. Mkulo alikuwa anaongea na Waziri mkuu na baadaye Mh. Wasirra akajisogeza na kuanza kuongea na Mh. Pinda.
 
juzi alimtuliza ngeleja kama katoto. Makinda alisema kwa mamlaka 'waziri kaa chini'. Ukiona hivyo ujue kagundua hana tena minyororo
 
Kwa kuwa mama huyu anaonekan kulitetea HESHIMA YA BUNGE LETU TUKUFU basi yeyote atakayemgusa ama gizani au kwenye mwanga basi atakua ametugusa sote tunaolithamini sana taasisi la bunge na shughuli zake KI-KATIBA katika maendeleo ya taifa letu.

Ajiandae kuonywa kama kathubutu
 
Spika wa Bunge la Jamhuri Mh. Anna Makinda amemtaka Waziri Mkuu kutoongea na wabunge pamoja na mawaziri wakati kikao kinaendelea ndani ya bunge. Spika amesema kwa kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni anapaswa kusikiliza na kufuatilia mijadala kwa makini. Amesema kama hali hiyo inaendelea hakuna maana kuwa na kiongozi wa wa shughuli za serikali bungeni.

Katika siku za hivi karibuni wabunge na mawaziri wamekuwa na tabia ya kwenda kunong'ona na waziri mkuu wakati kikao cha bunge kinaendelea. Hata hivyo wakati Spika anatoa onyo hilo, Mh. Mkulo alikuwa anaongea na Waziri mkuu na baadaye Mh. Wasirra akajisogeza na kuanza kuongea na Mh. Pinda.

Hivi kupindisha ukweli kunakusaidia nini?

Mimi nilikuwa nasikiliza Bunge leo hii, na Makinda aliwaonya wabunge wasimfate Pinda na si kama unavyotaka wewe ieleweke.
 
Tatizo yule mama unafki unamsumbua hata huko kumkemea pm imekuwa danganya toto, wangekuwa cdm angewatoa nje. Uongozi wa magamba huwa haupo fair na wanajisahau kama ndani ya bunge kuna wapinzani ambao huwezi kuwaendesha kwa kutaka wafwate matakwa ya magambazi.
 
Back
Top Bottom